Maajabu ya awamu hii, CAG akabidhi ripoti ya ukaguzi March 28, 2019 kimya kimya na Ikulu haikutaka umma ujue juu ya makabidhiano kati ya rais na CAG

Hiyo ni kutoka zile mbwembwe za kutangaza mapato ya TRA toka awamu hii imeingia madarakani mpaka kupokea ripoti kwa kificho. Hii ni dalili kwamba mambo yanazidi kuharibika tofauti na zile porojo zilizokuwa zinapigwa huko mwanzo.
 
Chadema kama hamjapeleka mahesabu ya fedha za ruzuku hakika mtafutwa kimya kimya labda ndio maana CC ya Ufipa kesho inakutana!

Maendeleo hayana vyama
Maendeleo yapi? CCM hawajaleta maendeleo na CAG hajaikagua CCM hukwepa kuwakagua na hata akienda kuwakagua atakuta madiudu mengi akina polepole wamefuja pesa nyingi kienyeji kwa visingizio vya kuzitumia kudhoofisha chadema na kuua upinzani kwa ujumla, CAG hagusi hesabu za CCM kwa kuogopa kufukuzwa ama kutumbuliwa
 
Huyu CAG huwa hapangiwi vya kusema/kufanya. Nadhani ni mtu wa swala tano aliyezoea ukweli na itakuwa hawajataka kushtukizwa na makasoro kibao hivyo wameona waipitie kimyakimya kwanza ukizingatia Dotto boy huwa anajiamulia kutoa pesa anapoamuriwa bila kufuata taratibu husika, lazima waminye ripoti. Hili ni jambo la aibu na fedhehe kwa kiongozi anayejipambanua kutaka uwazi na udhibiti bora ya pesa/mali ya umma.
 
Hawa wanyama sasa hivi wanavuka mto mara kwenda Kenya,wengi wanaliwa na mamba

Sent using Jamii Forums mobile app

Nyumbu ni CCM kwani wanachama wa CCM ni wengi kama walivyokuwa nyumbu wengi kule mbugani pia CCM haijaleta maendeleo pesa nyingi wanakula viongozi wa CCM lakini cha kushangaza na cha ajabu huko huko CCM wapo mbumbumbu na wanawasifia viongozi wao kwa kutafuna trilion 1.5 kienyeji na pia kula 10% ununuzi wa ndege ujenzi wa reli, flyover, chato Airport na wizi mwingineo kibao ikiwemo kivuko feki na zile bilion 252 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa nk.
 
Sijui unataka nini?

Angalau ingekuwa taarifa ya bunge kugomea TAARIFA YA CAG bungeni.

Ungeeleweka
 
Huyu CAG huwa hapangiwi vya kusema/kufanya. Nadhani ni mtu wa swala tano aliyezoea ukweli na itakuwa hawajataka kushtukizwa na makasoro kibao hivyo wameona waipitie kimyakimya kwanza ukizingatia Dotto boy huwa anajiamulia kutoa pesa anapoamuriwa bila kufuata taratibu husika, lazima waminye ripoti. Hili ni jambo la aibu na fedhehe kwa kiongozi anayejipambanua kutaka uwazi na udhibiti bora ya pesa/mali ya umma.

CAG hayupo huru tokea aitwe Dodoma akadhalilishwa na Spika Ndungai amekuwa muoga sana, ni swala tano kweli lakini CCM ni shetani wanamkaba koo asipumue kabsa, Doto Katibu mkuu wizara ya Fedha ni mtoto wa nje wa magufuli ingawa huzuga ni mtoto wa Dada yake lakini DNA ni moja tu, mtu na baba yake mda wowote hata saa nane usiku wakitaka pesa wanachukua BOT hata zile pesa wamewapora kienyeji wamiliki wa maduka ya kubadili pesa wamejimilikisha kimya kimya kwa njia haramu , CCM ni C- chukua C- chako M- mapema kila mmoja kajichukulia vyake kabla ya 2020 kwani hawajui kitatokea nini huko.
 
Mtaji wa JPM sasa hivi ni kuhakikisha watu hawapati taarifa muhimu bali kulishwa watakacho ccm. Wanajua kabisa kuna mambo mengi hayaendi vizuri hivyo namna pekee ni kuhakikisha taarifa muhimu haziufukii umma.
Ndio maana amepiga nyumbo uhuru wa vyombo vya habari pamoja na kuleta sharia kandamizi ili kuziba midomo wale wote wenye ujasiri wa kuhoji na kudadisi.
 
Back
Top Bottom