Maajabu ya Amboni

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,405
MAAJABU YA AMBONI.




1)ni ya ajabu mapango,kwa mipango ya pangika.
Na maajabu milango,iwezayo ingilika.
Anza kufanya mpango,nawe uweze kufika
Maajabu ya amboni,nawe enda tembelea.




2)shujaa wslijificha,kukwepa kudhulumiwa.
Pango ni usiku kucha,ajabu utavutiwa.
Kuondoka hutoacha,ngano kuzihadithia.
Maajabu ya amboni,nawe enda tembelea.




3)Afrika imejichonga,na nyayo zimejuchora.
Ukifika utaringa,ki kwelu utapata ra.
Wote tufikeni Tanga,tuende kila idara.
Maajabu ya amboni,nawe enda tembele.



4)Hamisi nae Osale,humu walijifia.
Wazungu wale wa kale,ndani walipotekea.
Mbwa bila ya kelele,mbali akaibukia.
Maajabu ya amboni,nawe enda tembelea.





5)waona kichwa cha simba,mlango kina ulinda.
Sauti kama marimba,popo wapiga kinanda.
Waruka huku waimba,pangoni wadunda dunda.
Maajabu ya amboni,nawe enda tembelea.




6)mchoro hadi wa chui,msikitini na kanisa.
Bila tochi hutambui,tembea uone sasa.
Mapango hayabagui,fika jipige msasa.
Maajabu ya amboni,nawe enda tembelea.




7)njia za chini kwa chini,hadi mombasa zafika.
Zimeanzia pangoni,na mipaka zikavuka.
Fahari yetu nchini,mkoa unasifika.
Maajabu ya amboni,nawe enda tembelea.




Shairi=MAAJABU YA AMBONI.
mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom