Safari na maajabu ya Amboni

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,209
4,406
SAFARI NA MAAJABU YA AMBONI.

kwa miaka mingi nilikuwa nikitamani sana kuyatembelea maajabu na vivutio vya mapango ya Amboni yaliyopo mkoa wa Tanga hapa hapa Tanzania.
Mapango hayo ambayo kwa mujibu wa sayansi na historia yalianza kujiunda kwa jumla ya miaka milioni mia moja na hamsini iliyopita na mpaka sasa kuwa kivutio cha maajabu ndani ya mkoa wa Tanga.
Nenp amboni limetokana maneno mawili ambayo ni neno MAMA MBONI pamoja na neno CHIRAMBONI.

Ndani ya mapango ya Amboni,kuna jumla ya mapango mawili maarufu ambayo ni pango la SALE OTANGO na mwenzake PAULO HAMISI.
watu hawa wawili mashujaa walitumia pango la Amboni kama maficho yao.
Baada ya wao kuwa wakijificha katika mapango haya huku wakifanya kazi ya uhalifu wa kiwizi kwa lengo tu la kutetea wanyonge wenzao waliokuwa wakipatina eneo la Tanga kwa nyakati hizo.
SALE OTANGO na mwenzake PAUL HIMISI waliweza jificha ndani ya pangp hili kwa muda wa miaka minne bila ya kugundulika ama kukamatwa.
Hiyo ilikuwa ni mwaka 1952 hadi 1956 ambapo kutokana na giza nene ndani ya pango hilo,OSALE na PAUL HAMISI walitumia miaka ya moto wa makuti kama sehemu ya kujipatia mwanga
Mwaka 1958 PAUL HAMISI alipigwa risasi na kufariki dunia.
Pia kuna historia kwamba waliwahi kuja wazungu wawili watafiti ambao ni mtu na mke wake wambao walikuwa wakitaka kuingia ndani ya pango hili lakini wenyeji waliwasihi wazungu hao wasiingie bila ya mwenyeji wa kuwaongoza lakini wazungu hao waligoma kutumia muongozaji mwenyeji na hivyo kuingia wenyewe.
Hapo ndipo ilipokuwa mwisho wa wazungu hao kuonekana na hawakutoka tena lakini baada ya mwezi mmoja ,mbwa wao alipatikana eneo la Kilimanjaro.
Pia ndani ya mapango ya Amboni kuna taswira kadhaa za kidini kama sanamu la bikira Maria aliekaribu na malaika huku kitabu kikionekana kikiwa kimefunuliwa.
Kwa upande wa waislamu,kuna onekana Qibla ambacho kulingana na tafiti yangu ya haraka,nimegundua kuwa Qibla hiyo imeelekea upande sawa sawa na ule wa Qibla za mkoa wa Tanga na upande wa kulia wa Qibla hiyo panaonekana michoro ya neno ALLAH huku pia pakiwa na mchoro wa alama "M" iwakilishayo neno MSIKITI ama MASJIDI ama MOSQUE.
Pango langu la kwanza kiingia ni lile liitwalo pango la JINSIA ambalo ni pango dogo lakini lenye maajabi ya pekee ambalo ni mzizi wa mti wavule kuchora alama ya "V" ama mshale ili kumuelekeza mtumiaji wa njia ya pango hili kupata urahisi wa kutoka.
Ila usije kufikiri kuwa ni rahisi kutoka humu bila ya kuwa na muongozaji ama guide.
Pia kunaonekana Taswira safi ya muundo wa bara la Afrika likiwa limejichora katika maajabu ya kupendeza zaidi.
Huku pia ukionekana muundo wa mshumaa uloyeyuka ambao unazidi kufanya mapango hayo kuwa ya kustaajabisha zaidi hasa pale unapoupanda mlima kilimanjaro na kupenya katika njia nyembamba iliyopo ndani ya mapangp hayo.
Utastaajabu pia pale uwapo ndani ya Amboni kwa kupona mfano wa ukumbi wa sherehe ambao kwa juu kidogo kinaonekana chumba cha Dj wa sherehe huku upande wa kulia ikionekana njia ya kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro.
Pia kuna kituo au pango ambalo limekuwa likitumika na wazee au watu wa kawaida kufanya matambiko au maombi yao ya kawida na baada ya kumaliza maombi hayo watu hao hutoa sadaka mahali hapo.
Baada ya wengi kufanikiwa huwa wanarudi badae na kutoa sadaka nyingine kama ya fedha na uongozi wa hifadhi hiyo ya kale huzitumia fedha hizo kama sehemu ya kusaidia watoto yatima ama kazi nyingine za kijamii.
Katika upande mwingine wa pango hilo,kunaonekana mfano au muundo wa kiti cha enzi ambacho kilikuwa kikitumika zamani kama kiti cha heshima kwa machifu ama watawala wa zamani.
Pia utaweza kuyaona maficho ya Paul Hamisi na Sale Otango bila kusahau mapango mengi ya ajabu kama ile njia ianziwayo Ndani ya pango la Amboni mpaka Mombasa.

VIVUTIO VINGINE.
mbali na mapango hayo pia waweza kuona aina ya popo wajulikanao kama FRUIT BATS wakiwa ndani ya pango hilo.huku nao wakishiriki sana katika kuongeza michoro ya ajabu ya wanyama,na nyayo za binadamu ndani ya pango hilo kwa upande wa juu.
Kwa nje utaweza kuona aina mbalimbali za miti ikiwemp ile mianzi pamoja na kuona aina ya primate kama kima ama blue monkey na maajabu mengi sana ndani ya pangp hilo.
Naamini utafurahi pindi uwasilipo ndani ya mapango ya Amboni.
 
uploadfromtaptalk1461948392596.JPG
 
Shukran iddi kwa kutushawishi kufanya utalii wa ndani maana wengi wamejikita kufanya utalii wa ndani penye miili ya watu.
 
Shukran sana, nasikia kuna statue of liberty pia Je imetengenezwa zamani na wazungu? Maana waliliona hilo pango miaka ya 1800
 
Maajabu mengine ya hilo pango ulipopelekwa jana na kuona kesho ukipelekwa na muongozaji mwingine utapata vitu vingine zaidi me ilitokea hiyo kitu so nikazidi kuwa interested maana sio rahisi kukumbuka yote
 
Inaweza kukuchukua kama masaa mangapi kuweza kuyatembelea hayo mapango? Na je ndani ya mapango kuna joto? Idd Ninga
Kuna hari ya ubaridi muda wote ni mwamba wa chokaa so habari nzuri hakuna nyoka anaweza ishi as hakai kwenye chokaa so ni safe mwanzo niliogopa ila baada ya kuambiwa hivo nilikua huru na kuenjoy
 
Ooh asante sana nilikuwa sijui hilo, nikija tena Tanga itabidi nitembelee hapo
Katibu onggeza uelewa kwa nchi yako.iko poa Sana nzuri zaidi unaweza toka hapa alfajiri kwa public transport ukafika saa tano ukaenda amboni nauri 400 tu kwa daladala ila ukifika kituoni kuna bodoboda 1500-2000.nusu saa tu unakua umeenjoy sana tu unageuza na basi la saa tisa au nane
 
SAFARI NA MAAJABU YA AMBONI.

kwa miaka mingi nilikuwa nikitamani sana kuyatembelea maajabu na vivutio vya mapango ya Amboni yaliyopo mkoa wa Tanga hapa hapa Tanzania.
Mapango hayo ambayo kwa mujibu wa sayansi na historia yalianza kujiunda kwa jumla ya miaka milioni mia moja na hamsini iliyopita na mpaka sasa kuwa kivutio cha maajabu ndani ya mkoa wa Tanga.
Nenp amboni limetokana maneno mawili ambayo ni neno MAMA MBONI pamoja na neno CHIRAMBONI.

Ndani ya mapango ya Amboni,kuna jumla ya mapango mawili maarufu ambayo ni pango la SALE OTANGO na mwenzake PAULO HAMISI.
watu hawa wawili mashujaa walitumia pango la Amboni kama maficho yao.
Baada ya wao kuwa wakijificha katika mapango haya huku wakifanya kazi ya uhalifu wa kiwizi kwa lengo tu la kutetea wanyonge wenzao waliokuwa wakipatina eneo la Tanga kwa nyakati hizo.
SALE OTANGO na mwenzake PAUL HIMISI waliweza jificha ndani ya pangp hili kwa muda wa miaka minne bila ya kugundulika ama kukamatwa.
Hiyo ilikuwa ni mwaka 1952 hadi 1956 ambapo kutokana na giza nene ndani ya pango hilo,OSALE na PAUL HAMISI walitumia miaka ya moto wa makuti kama sehemu ya kujipatia mwanga
Mwaka 1958 PAUL HAMISI alipigwa risasi na kufariki dunia.
Pia kuna historia kwamba waliwahi kuja wazungu wawili watafiti ambao ni mtu na mke wake wambao walikuwa wakitaka kuingia ndani ya pango hili lakini wenyeji waliwasihi wazungu hao wasiingie bila ya mwenyeji wa kuwaongoza lakini wazungu hao waligoma kutumia muongozaji mwenyeji na hivyo kuingia wenyewe.
Hapo ndipo ilipokuwa mwisho wa wazungu hao kuonekana na hawakutoka tena lakini baada ya mwezi mmoja ,mbwa wao alipatikana eneo la Kilimanjaro.
Pia ndani ya mapango ya Amboni kuna taswira kadhaa za kidini kama sanamu la bikira Maria aliekaribu na malaika huku kitabu kikionekana kikiwa kimefunuliwa.
Kwa upande wa waislamu,kuna onekana Qibla ambacho kulingana na tafiti yangu ya haraka,nimegundua kuwa Qibla hiyo imeelekea upande sawa sawa na ule wa Qibla za mkoa wa Tanga na upande wa kulia wa Qibla hiyo panaonekana michoro ya neno ALLAH huku pia pakiwa na mchoro wa alama "M" iwakilishayo neno MSIKITI ama MASJIDI ama MOSQUE.
Pango langu la kwanza kiingia ni lile liitwalo pango la JINSIA ambalo ni pango dogo lakini lenye maajabi ya pekee ambalo ni mzizi wa mti wavule kuchora alama ya "V" ama mshale ili kumuelekeza mtumiaji wa njia ya pango hili kupata urahisi wa kutoka.
Ila usije kufikiri kuwa ni rahisi kutoka humu bila ya kuwa na muongozaji ama guide.
Pia kunaonekana Taswira safi ya muundo wa bara la Afrika likiwa limejichora katika maajabu ya kupendeza zaidi.
Huku pia ukionekana muundo wa mshumaa uloyeyuka ambao unazidi kufanya mapango hayo kuwa ya kustaajabisha zaidi hasa pale unapoupanda mlima kilimanjaro na kupenya katika njia nyembamba iliyopo ndani ya mapangp hayo.
Utastaajabu pia pale uwapo ndani ya Amboni kwa kupona mfano wa ukumbi wa sherehe ambao kwa juu kidogo kinaonekana chumba cha Dj wa sherehe huku upande wa kulia ikionekana njia ya kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro.
Pia kuna kituo au pango ambalo limekuwa likitumika na wazee au watu wa kawaida kufanya matambiko au maombi yao ya kawida na baada ya kumaliza maombi hayo watu hao hutoa sadaka mahali hapo.
Baada ya wengi kufanikiwa huwa wanarudi badae na kutoa sadaka nyingine kama ya fedha na uongozi wa hifadhi hiyo ya kale huzitumia fedha hizo kama sehemu ya kusaidia watoto yatima ama kazi nyingine za kijamii.
Katika upande mwingine wa pango hilo,kunaonekana mfano au muundo wa kiti cha enzi ambacho kilikuwa kikitumika zamani kama kiti cha heshima kwa machifu ama watawala wa zamani.
Pia utaweza kuyaona maficho ya Paul Hamisi na Sale Otango bila kusahau mapango mengi ya ajabu kama ile njia ianziwayo Ndani ya pango la Amboni mpaka Mombasa.

VIVUTIO VINGINE.
mbali na mapango hayo pia waweza kuona aina ya popo wajulikanao kama FRUIT BATS wakiwa ndani ya pango hilo.huku nao wakishiriki sana katika kuongeza michoro ya ajabu ya wanyama,na nyayo za binadamu ndani ya pango hilo kwa upande wa juu.
Kwa nje utaweza kuona aina mbalimbali za miti ikiwemp ile mianzi pamoja na kuona aina ya primate kama kima ama blue monkey na maajabu mengi sana ndani ya pangp hilo.
Naamini utafurahi pindi uwasilipo ndani ya mapango ya Amboni.
Duh jaman kweli Tanga raha
 
Back
Top Bottom