Maajabu -Tuache kasumba masikini watanzania!

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Ndugu wana JF
Watanzania kwa ujumla tumekuwa na kasumba kubwa sana kwa kuwadharau na kuwaona wale wajengao nyumba zao kwa kutumia TOFARI za kuchoma eti ni masikini,na ili uheshimike na kudhaminiwa na mtanzania ni lazima utumie tofari iliyotengenezwa na cement(block)

Lakini kwa nchi zenye maendeleo ya hali ya juu Duniani wao hawana huo upuuzi tulionao sisi masikini wa kutupwa,watatu kwa kuomba omba duniani,kwani wao wanatumia TOFARI ya udongo iliyochomwa kwa kujenga majengo yaliyo imala zaidi ya yale ya block tuyajengayo sisi masikini wa kutupwa TANZANIA

Nimeleta post hii ilikuwa eleza wabongo,masikini wenzangu,mlio jaa dharau na kejeri wakati umasikini unatumaliza kwa kununua cement nyingi na kuwanufaisha mabwanyenye kwa kutaka ufahari wa kujenga nyumba za tofari za block.

Angalia picha hapa chini

1.Tofari ya kuchomwa ipo site tayari kwa maandalizi ya ujenzi

IMG_20120407_164334.jpg IMG_20120407_101529.jpg

2.tayari tofari ya kuchoma tunayo idharau watanzania imetengeza ghorofa kadhaa

IMG_20120407_163639.jpg

IMG_20120407_163528.jpg IMG_20120407_163617.jpg








3.baada ya ujenzi kuisha,waweza amini kuwa tofari ya kuchuma ndio iliyotumika hapo?​

IMG_20120407_164116.jpg IMG_20120407_163734.jpg
 
tena nyumba za tofari za kuchoma zinakaa miaka mingi kuliko block,

nakubariana na wewe mkuu,kwani kama tujuavyo udongo hauna expire date ukifananisha na tofari za cement,zinasaidia kupunguza joto ktk nyumba,hazina gharama kubwa na ni rahisi kupatikana
 
Mkuu nadhani watu wa DSM peke yao ndo wana hiyo dhana, lkn mikoa mingi ya hapa TZ wanajenga kwa kutumia tofari za kuchoma na zinapendeza sana. Hata mimi nikidondosha mjengo wangu hapa DAR ntatumia tofari za kuchoma.
 
Mkuu sio wa dharau ,watu wa wamekosa hiyo technologia.

mkuu

mbona tofari hizi zipo Iringa na morogoro,kinachotakiwa ni kuwaelimisha wapiga tofari kuwa wanahitaji kukanda udongo kwa mda mrefu hadi uive ipasavyo na wakati wa kuzichoma watumie moto ambao utasaidia tofari kuiva vyema

hapa nilipo,wafyatua tofari ni watu wa kawaida sana tena ni wazee,wanatumia nyenzo kama tutumiazo nyumbani,tofauti ni kwamba wao wanatumia makaa ya mawe ktk kuchoma tofari zao
 
Mkuu nadhani watu wa DSM peke yao ndo wana hiyo dhana, lkn mikoa mingi ya hapa TZ wanajenga kwa kutumia tofari za kuchoma na zinapendeza sana. Hata mimi nikidondosha mjengo wangu hapa DAR ntatumia tofari za kuchoma.

Nakubariana na wewe,lakini waliowengi wanaona kujenga kwa tofari za kuchoma ndio kimbilio rahisi sana ukilinganisha cement

hata ukiangalia ghorofa nyingi Tanzania huwezi kuta tofari ya kuchoma imetumika,hata nami nilikuwa na kasumba hiyo lakini baada ya kuwepo mazingira haya najionea maajabu ya tofari za kuchoma zinzvyo nyanyua ghorofa na siajawahi ona tofari ya block ikitumika mahali hapa zaidi ya slab ktk mataraja
 
Tatizo kubwa ni kwamba asilimia kubwa ya tofali za udongo zinazouzwa sehemu nyingi Tz hazina viwango. Za ughaibuni zina viwango tosha.hazitengenezwi kienyeji kama zetu. Yote kwa yote, naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom