Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Habari Wenyeji wa jukwaa hili. Habari ilitawala mjini mara kwa sasa ni kuhusu Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Andrea Mjungu, mwenye umri wa miaka 26 kukutwa akifanya mapenzi na mbuzi (mnyama). Mwanaume huyo alikutwa akiwa uchi wa mnyama akiwa katika mihemko ya tendo haramu na mnyama wa jirani yake kabla ya kukurupushwa ambapo alikimbilia ziwa Tanganyika. Baada ya kukuru kakara za hapa na pale, mtuhumiwa alikamatwa na kurudishwa eneo la tukio.Mtuhumiwa alijitetea kwamba hali hiyo ilitokana na kuchanganyikiwa kisaikolojia kutokana na mwenza wake (mwanamke) kumnyima tunda la roho. Mwishowe mwenye mbuzi aliamuru alipwe fidia ya fedha, ila alikataa kurudishiwa mbuzi akidai hafai kwa kitoweo.Je, ungekuwa ndugu,mzazi,rafiki au mpenzi wa Mjungu ungejisikiaje? (Source:RFA-Matukio, 23.05.2013)