MAAJABU: hii ndiyo Tanzania toka 1961 hadi sasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAAJABU: hii ndiyo Tanzania toka 1961 hadi sasa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, Apr 22, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Tanzani mpaka sasa, Katika miaka
  hii ya nyuma hatukuwa tunajenga
  Ujamaa.
  Nchi yetu, uchumi wetu, na tamaa
  kubwa za watu wetu, ni tofauti
  sana na jinsi zilivyokuwa kabla ya
  ukoloni. Kwa jumla tumekubali
  mawazo na maisha ya mabwana
  zetu wakoloni. Ni kweli tuliweza
  kuondoa serikali ya Kikoloni; lakini
  hatujaondoa akilini mwetu
  mawazo ya ubinafisi
  tuliyofundishwa na wakoloni na
  ambayo ndiyo yaliyokuwa msingi
  wa ukoloni wenyewe. Ilikuwa ni
  kutokana na wakoloni ndiko
  tulikopata mawazo ya kwamba
  njia ya kujipatia starehe na mali
  ambayo kila mtu anataka ni
  uchoyo na tamaa ya ubinafsi. Na
  ni kweli kwamba kwa utaratibu
  wa kibepari na kikabaila
  inawezekana sana kwa watu
  wachache kujipatia mali nyingi
  nyingi na starehe kubwa ajabu.
  Hata katika nchi maskini kama
  yetu inawezekana, kama wote
  tuonavyo, kwa watu wachache
  kuwa na mali nyingi nyingi tena
  hasa wakiwa wengi wao ni
  viongozi serikalini, ingawa hali za
  wengine ni za chini kuliko
  zinavyostahili kuwa.
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  viongozi wetu ni mafisadi lakini tunawachangua! nani alaumiwe?!
   
Loading...