Maafisa Sheria hawafanyi kazi hatarishi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maafisa Sheria hawafanyi kazi hatarishi???

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ngoshwe, Jul 23, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="colspan: 5"][TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="width: 13%, align: center"][​IMG][/TD]
  [TD="width: 87%"]Opulukwa, Meshack Jeremiah [CHADEMA]
  Meatu Constituency
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="width: 110, align: center"]Session No[/TH]
  [TH="width: 123, align: center"]Question No[/TH]
  [TH="width: 391, align: center"]To the Ministry of[/TH]
  [TH="width: 196, align: center"]Sector[/TH]
  [TH="width: 162, align: center"]Date Asked[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="align: center"]7[/TD]
  [TD="align: center"]25[/TD]
  [TD="align: center"]JUSTICE AND CONSTITUTIONAL AFFAIRS[/TD]
  [TD="align: center"]Justice/Constitution[/TD]
  [TD="align: center"]11 April 2012[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="colspan: 5, align: left"]Principal Question No[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 5, align: center"]Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Umma wa 2007 hauwatambui Mawakili wa Serikali walioajiriwa kwenye Wizara pamoja na Idara za Serikali kama Mawakili wa Serikali, bali Maafisa Sheria:¬

  (a) Je, Serikali itafuta lini Waraka huo wa kibaguzi na Mawakili wote walioajiriwa kama Mawakili wa Serikali kuendelea kuitwa hivyo na si Maafisa Sheria?

  (b) Je, Serikali itawalipa lini Maafisa Sheria posho, mishahara na stahili nyingine sawa na Mawakili wa Serikali waliopo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kama taaluma nyingine zinavyofanya Serikalini?
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="colspan: 5, align: left"]ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #25 SESSION # 7[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 5"][TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="width: 10%"][​IMG][/TD]
  [TD="width: 90%"]Answer From Hon. Kombani, Celina Ompeshi
  JUSTICE AND CONSTITUTIONAL AFFAIRS
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 5"]WAZIRI alijibu:-

  Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Meshack Jeremiah Opulukwa, Mbunge wa Meatu, napenda kutoa maelezo yafuatayo:-

  Mheshimiwa Naibu Spika, Wanasheria ni Wanataaluma waliohitimu shahada katika fani ya sheria katika vyuo vikuu vya Tanzania na vya nje vinavyotambuliwa na Serikali na kupata mafunzo ya vitendo katika Shule ya Sheria (The Law School of Tanzania).

  Wahitimu hawa wengi wao huajiriwa katika kada mbalimbali za ajira Serikalini kama vile Mahakimu, Mawakili wa Serikali, Waendesha Mashtaka katika Jeshi la Polisi, TAKUKURU na taasisi nyingine za Serikali

  Kutokana na taaluma yao, Wanasheria hawa wanaweza kuajiriwa na Wizara, Idara au Taasisi za Serikali kwa kuzingatia Miundo, kazi na mahitaji ya kila sekta husika. Wanasheria wengine huajiriwa katika sekta binafsi. Majina wanayopewa watumishi katika kada ya Sheria hutegemea sheria inayosimamia kada hiyo na aina ya kazi wanazofanya katika mashirika husika.

  Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2005, Bunge lako Tukufu lilitunga Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura ya 268, kwa madhumuni ya kuweka utaratibu wa namna ya kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali. Sheria hiyo, licha ya kuweka majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama yalivyoainishwa katika Ibara za 59, 59A na 59B za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeainisha utaratibu wa ajira na utendaji kazi wa Mawakili wa Serikali na Wanasheria wengine.

  Kifungu cha 24 na 25 vya Sheria hiyo, vinaeleza kuwa Afisa Sheria ni mtu aliye na Shahada ya Sheria kutoka katika chuo kikuu kinachotambulika aliyeajiriwa katika Utumishi wa Umma isipokuwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  Aidha, Wakili wa Serikali ni yule aliye na Shahada ya Sheria kutoka katika chuo kinachotambulika na kuajiriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali. Katika utendaji kazi, mtumishi huyo anapata maelekezo ya utendaji kazi kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema nieleze kuwa, Sheria hiyo pia inawazuia Mawakili wa Serikali kufanya kazi za Uwakili wa Kijitegemea.

  Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Meshack Jeremiah Opulukwa, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:¬

  (a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haina sababu za msingi za kuufuta Waraka wa Maendeleo ya Utumishi, Na. 12 wa Mwaka 2002, kama ulivyorekebishwa Mwaka 2007 kwa kuwa, si wa kibaguzi. Waraka huo umelenga kuimarisha Muundo wa Kada ya Mawakili wa Serikali na kuweka uhusiano uliopo katika ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi nyingine za Serikali zinazotoa huduma za kisheria. Waraka huu umezingatia dhamana, unyeti wa kazi na mazingira hatarishi ya Mawakili wa Serikali kama waendesha mashtaka, wasimamizi wa ushahidi mahakamani, uandishi wa sheria, majadiliano na uandaaji wa mikataba ya kiserikali, kuitetea Serikali Mahakamani na katika Mabaraza ya Usuluhishi. Maafisa Sheria hawafanyi kazi kama hizo na hawafanyi kazi katika mazingira hatarishi ikilinganishwa na Mawakili wa Serikali.

  (b)Mheshimiwa Naibu Spika, taratibu za kupandishwa vyeo watumishi wenye taaluma ya Sheria, mishahara na stahili zao nyingine, zinapaswa kuandaliwa na Ofisi zinazowaajiri na kuwasimamia Wanasheria hao. Kuwepo kwa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Mwaka 2002 uliofanyiwa marekebisho mwaka 2007 hakuzuwii Wanasheria wengine kupata maslahi wanayostahili kwa m
  ujibu wa majukumu wanayotekeleza katika maeneo yao. [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Hivi kwani Maafisa wa Sheria huko Serikalini wanafanya nini?? Nimesikia sasa kuna mvutano kati ya wanasheria wa Serikali walio katika Utumishi wa Umma (Wale wambao wapo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wale walipo katika Wizara na Taasisi nyingine hasa kuhusu maslahi na nafasi (kwa mfano wale walio kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wanalalamika nkutoruhusiwa kuapishwa kuwa mawakili wa kujitegemea (Advocates)) .

  Pia, pamoja na ukweli kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mujibu wa Ibara ya 59(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  ndiye mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo, atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria​
  zitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza, na pia kutekeleza kazi au shughuli nyinginezo zilizokabidhiwa kwake na Katiba au na sheria yoyote, kiutaratibu anaonekana hana mamlaka makubwa juu ya Wanasheria wanaoajiriwa kwenye taasisi nyingine za umma ikiwemo Bodi na Mamlaka mbalimbali. Ni kama vile hawezi kushughulikiwa masuala ya Kisheria ambayo yanaihusu taasisi fulani moja kwa moja. Hii inaleta upungufu mkubwa wa utendaji wa Ofisi yake, na ndio iliyopelekea sasa baadhi ya Taasisi kufanya madudu. Tumeona kwenye shauri ya Dowans na Tanesco jinsi Mwanasheria Mkuu wa Serikali alivyoshindwa kutekeleza majukumu yake vizuri ya kushauri kwenye mkataba na hata kwenye kusimamia Mgogoro ulipokuwa kwenye Usuluhishi na Hata Mahakamani.

  Labda kuna tatizo la yeye kuweza kuelekeza wale ambao hajawaajiri..nini maana ya kuwepo kwa Ofisi hiyon nyeti kama hana uwezo wa kuwadhibiti wanasheria waliopo nje ya Ofisi yake?? Nimesoma majibu yakliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Sheria Mhe. Celina Kombani alipoulizwa na Bungeni kuhusu hadhi za Mawakili wa Serikali na Maafisa Sheria. Kama mtu yupo makini ataona wazi kuwa majibu yaliyotolewa yanaonyesha ni ya kibaguzi kabisa.
   
Loading...