Maafisa kilimo kupelekwa Jeshini kutaleta tija kwa mkulima?

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Waziri wa Kilimo Ndugu. Hussein Bashe akiwa Dodoma kwenye kongamano la wadau Kahawa amesema ili kuboresha ufanisi wa maafisa Kilimo anawasiliana na Wizara ya Ulinzi( JKT) ili maafisa kilimo wapelekwe kwenye mafunzo ya jeshi kupata "Military Discipline" Swali likanijia je hili ni hitaji la mkulima? Je vyuo vya kilimo vimeshindwa kuandaa wataalamu bora hadi jeshi kuingilia kati?

Kero za Wakulima ambazo kila mtu anazijua ni bei kubwa za pembejeo na mazao kukosa soko.Mfano bei ya parachichi msimu huu imepolomoka kutoka 2000 hadi 1000. Hili Waziri halioni? Korosho ni hivyo hivyo na mazao mengine ya kibiashara. Pia Wakulima wanakero ya kupoteza mazao baada ya kuvuna( Post harvest losses) kwa sababu ya ubovu na ukosefu wa miundombinu bora.

Wakulima wanahitaji teknolojia mpya ya uzalishaji na usindikaji wa mazao . Kukurupuka sijui kubuni sare za maafisa kilimo au kuwapeleka jeshini sioni km kunaenda kutatua kero ya bei kubwa za pembejeo.

Hakuna nchi yoyote Duniani iliyoleta mapinduzi ya kilimo kwa kutegemea mbinu za kijeshi. Marekani kwa mfano 3% hadi 4% ya wananchi wake ndio wanaojihusisha na kilimo lakini wanazalisha chakula cha kutosha nchi nzima na ziada wanatoa misaada. Wamefanikiwa hivi kwa kufanya uwekezaji mkumbwa na si vinginevyo.

Ufanisi wa maafisa kilimo utaongozeka kwa kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara na vitendea kazi. Haya mambo ya kuamini kila kitu lazima kifanywe na jeshi ni sawa na mwenda zake alivyoamini wachezaji mpira wa miguu wapelekwe jeshini ili kushinda mechi bila kujua kuwa mpira ni sayansi na ushindi utatokana na uwekezaji kwenye akademi bora za kisasa.

Viongozi wetu wamekuwa wakiamini katika kutumia nguvu kuliko akili matokeo yake Dunia inatuacha. Kenya wametuacha kwenye mambo mengi,Rwanda taifa lililokuwa limeparaganyika taratibu nao wanatuacha. Hizi si zama za kutumia nguvu nyingi kufanya jambo. Ndio maana mtu anaweza kuwa amelala kitandani lakini anaingiza pesa.

Kile kituko cha serikali kwenda kununua korosho bado nacho hatuja kisahau. Takribani Bil.200 zilipotea kisembe kabisa ikiwa ni madhara ya kutumia nguvu licha ya wataalamu kupinga serikali haikusikia.

Kabla ya wanasiasa kuleta mbadadiliko yoyote ni vema zikafanyika tafiti za kutosha ili kuona km kuna umuhimu au faida wa jambo husika.Yasije kutokea km ya Mungai kuchanganya Physics na Chemistry kuwa somo moja.
 
Sisi sera za nchi yetu huwa zinatokana na fikra za kiongozi mwenye dhamana. Nchi za wenzetu waliokwisha piga hatu mbele sera zao huwa zinatokana na tafiti za kitaalamu zilizofanywa.

Mtu kama waziri kwa wenzetu huwa anaangalia utafiti unasemaje kisha ndio wanatoa uelekeo wa sera za sekta yake. Wakati mwingine hutoa maamuzi baada ya timu ya wataalamu kukutana na kujadiliana kitaalamu changamoto zilizopo na kuzitafutia suruhu. Sisi kwetu zidumu fikra za kuongozi.
 
Form Six huwa wanapelekwa jeshini kila mwaka lakini matokeo baada ya mafunzo hayaonekani licha pesa nyingi kutumika. Mbaya zaidi hakuna anaehoji.
 
Form Six huwa wanapelekwa jeshini kila mwaka lakini matokeo baada ya mafunzo hayaonekani licha pesa nyingi kutumika. Mbaya zaidi hakuna anaehoji.
Kwani viongozi mafisadi nchini hawakupitia JKT?Tena walipitia enzi hizo JKT Ni mwaka mzima sio hii ya miezi michache tu.
 
Hili ni tatizo kubwa sana! Wakati mwengine hata bungeni tu hawapeleki wanaamua wao kama wao kmmk zao
Sisi sera za nchi yetu huwa zinatokana na fikra za kiongozi mwenye dhamana. Nchi za wenzetu waliokwisha piga hatu mbele sera zao huwa zinatokana na tafiti za kitaalamu zilizofanywa.

Mtu kama waziri kwa wenzetu huwa anaangalia utafiti unasemaje kisha ndio wanatoa uelekeo wa sera za sekta yake. Wakati mwingine hutoa maamuzi baada ya timu ya wataalamu kukutana na kujadiliana kitaalamu changamoto zilizopo na kuzitafutia suruhu. Sisi kwetu zidumu fikra za kuongozi.
 
Anaeshauri waende Jeshini Mungu amsamehe tu maana hajui atendalo, Taifa linajiingiza kwenye matumizi yasiyo na tija
 
Nchi haishi vituko. Naona basi wote tutaishia jeshini. Badala ya kuhuaisha malengo na vivutio (incentives) wewe unaleta za kuleta. Kwa hiyo hawa nao watakuwa wanajeshi?.
Tukiendelea hivi ujue kila kazi ya umma itaishia kuwa ya kijeshi na mwisho nchi nayo itaishia huko huko. Mawazo kama haya yanamea vizuri chini ya chama kimoja na sauti moja.
 
Ka video kenyewe haka hapa
 
Back
Top Bottom