Wanaume wawili wakiwa na gari aina ya Prado wakamatwa huko Mombo wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga ,katika jaribio la kumtapeli mfanyabiashara kwa jina maarufu Sheshe ,wakijifanya ni maafisa wa TRA. Matapeli hao wanaoishi Tanga mjini mmoja anafahamika kwajina la Erastho Eliud akiwa na mwenzake walifika nyumbani kwa mfanyabiashara huyo wakijifanya ni maafisa wa TRA,kwa bahati nzuri hawakumkuta nyumbani kwake bali walimkuta kijana.
Kijana akampigia simu baba yake ,nae akawajulisha Polisi kuwa kuna watu wako nyumbani kwangu wanasema ni maafisa wa TRA ,Polisi wa kituo cha Polisi Mombo wakawawekea mtego na hatimae wakawakamata baada ya upekuzi walikutwa na bendera ya bunge na vitu vingine ambavyo sio kawaida mtu wa kawaida kukutwa navyo.