Maadili yanavyoathiri fikra zetu

gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
8,853
1,500
Habari za saa hizi waungwana
Maadili ni misingi ambayo jamii imejijenga na kujiwekea ya kwamba yanakubalika kwenye jumuiya ya wengi,ni yale matendo yaliyosahihi na yanayowapendezea weng.Wengi wanaambatanisha haya na misingi ya dini na hofu ya mungu lakini kwa mtazamo wangu ni fikra ambazo watu wamejiwekea mfano kuwa na mavazi yenye heshima,kuwa mkarimu na mwenye hekima,kuwa mcha mungu.Kwangu mimi imani ya mtu ni chaguo la mtu binafsi.
Lakini je tushawahi kufikiria kwamba maadili hayohayo yanatunyima uhuru wa kufanya yale ambayo yapo kwenye fikra zetu?ambayo ukiyafanya unakiuka maadili na jamii inakutazama kwa jicho la tatu?Je tumekuwa watumwa wa maadili ambayo tumejijengea kwenye jamii inayotuzunguka. Wengi wanatenda yale ambayo wanaona ni sawa kutokana na maadili na misingi walolelewa nayo lakini kuna wale ambao wanaogopa kufanya yanayowapendezea kwa kuhofia jamii au ndugu wanaowazunguka watawachukuliaje na kuwaelewaje!!Kwanini watu wanajali zaidi kufanya yale yanayowapendezea wengine na yaliyo ya fahari kwenye macho ya wengi kuliko kufanya yale yanayowaridhia?Je nitakosea nikisema tunazidhulumu nafsi zetu?Kama maisha ni yako,ishi unavyopenda ndio utafurahia maisha!Tambua yale yalo na umuhimu kwako na uyatendee haki.Umekuja peke yako kwenye dunia hii na utaondoka peke yako,"Be free" percieve your goals and dreams,"A true spirit will give you peace of heart and mind"
Rules-for-Free-Spirits-TG.jpg
Karibuni wapendwa!
 
Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
30,656
2,000
Wakati unatafuta kuiridhisha nafsi, inabidi kuwa kama umejitoa ufaham wa kile unachofanya. Ila moyo wako umenuia kufanya kile ambacho jamii inaonekana kutofurahishwa nacho
 
ruralofficer

JF-Expert Member
Apr 4, 2014
2,019
2,000
imebez zaid kiimani naona
mfno.dini znafundsha mambo 2tu.rewards vs punishment na pple weng wanapenda rewards hivo lazma wa pretend coz ya uoga.
 
Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
27,169
2,000
Wakati mwingine tunaishi kutokana na jamii husika, kuishi maisha huru sio rahisi hasa ukiwa katika jamii zinafuata maadili fulani. Nitoe mfano wa mavazi kulingana na mazingira; ukiishi nchi za kiarabu, kama mwanamke..utake usitake lazima uvae kutokana na mazingira, sidhani kuwa wanawake wote wanaoidhi nchi za kiarabu wanapendelea kujikanda nguo mwili mzima "wakati wote" lakini hawana uhuru wa kufanya hivyo. Lakini wale wanaoishi ulaya na magharibi wana uhuru, kwa hiyo inabaki uchaguzi wa mtu kufanya atakalo.

Wengi wangependa kuishi watakavyo, lakini sio rahisi kuishi utakavyo kwa sababu uko mwenye jamii, ingekuwa unaishi pekeyo, hapo sawa. Lakini ili ukubalike katika jamii Ni lazima uendane na nini jamii husika inataka, na ndio maana zikawekwa angalau kanuni, sheria zinazoiongoza jamii..
 
Hoshea

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,604
2,000
Kweli kabisa.
Haswa haya maadili ya hizi dini za wakoloni ndio zina athari kubwa sana, mtu ishi vile unavyotaka kuwa mfano mzuri kwa wadogo tenda wema basi, hizi imani imani kwa hawa mitume zinatugawa na kutufarakanisha tu wakt hakuna ukweli wowote.
 
Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,815
2,000
Labda kama sijakuelewa lakini kama nimekuelewa ni hivi huwezi kuishi unavyotaka ili nafsi yako iridhike kwa sababu umezaliwa na umeishi katika jamii inayokuzunguka,kuna kanuni na sheria za jamii husika kumbuka jamii inauhusiano na Mungu kwa wale wanaoamini Mungu,na kwa wasioamini Mungu nao pia kuna miungu wao sasa huwezi kuishi unavyotaka inje ya misingi ya jamii yako,nadhani ni tamaa zaidi inaweza kumuongoza mtu eti kwa kuwa fulani anaishi hivi basi na mimi niwe hivyo lakini unashindwa kujua labda anaishi kulingana na jamii yake.

Halafu haujasema jinsi fikra zetu zinavyoathiriwa,toa angalau mifano
 
utafiti

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
12,797
0
Inategemea unafuata maadili ya aina gani, mfano maadili ya jamii iliyokuzunguka, mfano mdogo;- kule kwetu kijijini ukipishana na mzee anaelingana na baba yako kwa umri akiwa amebeba mzigo inabidi umpokee na umpelekee nyumbani/anakoenda. Kama ni mgeni utasema huko "huru" ila kwa tuliozoea ni kama "kawaida" tu
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,785
2,000
kila jamii ina tamaduni na maadili yake,utamaduni ni kama samaki ndani ya maji,mtoe kwenye maji uone anavyotapatapa
 
kibali

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
460
500
Hebu twende sawa, hebu toa mifano ya kitu ambacho wewe kwako unaona ni kawaida kinakupa raha ambacho kwa mtazamo wako umeona kinakupa amani ya moyo!
 
kibali

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
460
500
Labda kama sijakuelewa lakini kama nimekuelewa ni hivi huwezi kuishi unavyotaka ili nafsi yako iridhike kwa sababu umezaliwa na umeishi katika jamii inayokuzunguka,kuna kanuni na sheria za jamii husika kumbuka jamii inauhusiano na Mungu kwa wale wanaoamini Mungu,na kwa wasioamini Mungu nao pia kuna miungu wao sasa huwezi kuishi unavyotaka inje ya misingi ya jamii yako,nadhani ni tamaa zaidi inaweza kumuongoza mtu eti kwa kuwa fulani anaishi hivi basi na mimi niwe hivyo lakini unashindwa kujua labda anaishi kulingana na jamii yake.

Halafu haujasema jinsi fikra zetu zinavyoathiriwa,toa angalau mifano
Amelionglea hili jumla jumla ndio maana tunashindwa kuelewa ni vip fikra zinavyoaadhiriwa na maadili" maana kama fikra zinakutuma uwe mwizi ili moyo wako ufaurahi basi then useme maadili yankukosesha uhuru litakua jambo la taoafuti kabisa
 
Unachanganya imani ya dini na maadili...je watu wasiokuwa na dini na hofu ya mungu unataka kuniambia hawana madili?fikra zinaathiriwa kwa mfano mtu kuhofia kufunga ndoa na mtu wa dini tofauti kwa hofu jamii na wazazi watalichukuliaje suala hilo!
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,027
1,500
Muulize Kiranga gharama ya kuwa 'free spirit', tutakuzodoa hata kwa chakula unachokula. Sio rahisi kivile.
 
Last edited by a moderator:

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,815
2,000
Unachanganya imani ya dini na maadili...je watu wasiokuwa na dini na hofu ya mungu unataka kuniambia hawana madili?fikra zinaathiriwa kwa mfano mtu kuhofia kufunga ndoa na mtu wa dini tofauti kwa hofu jamii na wazazi watalichukuliaje suala hilo!
Hata wasio na dini nao wanamazingira yao,wewe pia uliongelea upande wa imani ndo maana nikagusia,lazima utambue maadili yanatofautiana kulingana na mazingira husika,kuna wengine kumuheshimu mume mpaka upige magoti,hauruhusiwi kuoga bafu analotumia mkwe wako lakini kwa wengine haiko hivyo na ukifanya kulingana na mazingira uliyokulia na maadili uliyofundishwa watakuona mtu wa ajabu kwani wao hawajazoea

Vivyo hivyo katika kufunga ndoa na mtu wa dini tofauti ingawa wewe unaona ni uhuru lakini si uhuru mfano rahisi ni huu hapa wakristo wamelelwa na wanafundishwa mke mmoja kwa mume mmoja,kwa waislamu ni tofauti wao ni mume mmoja kwa wake wanne,maana yake ni kwamba kama muislamu anataka kuolewa na mkristo lazima afuate mfumo wa huyo anayeolewa naye vivyo hivyo kwa upande mkristo kuolewa na muislam.

Unaziona athari ni kwa sababu umeenda tofauti na maadili ya jamii yako lakini ungeenda sawa na maadili ya jamii yako wala usingezioa hizo athari,hata Adam na Eva walipokuwa bustanini waliuuona uovu baada ya kula tunda walilokatazwa
 
gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
8,853
1,500
Wakati mwingine tunaishi kutokana na jamii husika, kuishi maisha huru sio rahisi hasa ukiwa katika jamii zinafuata maadili fulani. Nitoe mfano wa mavazi kulingana na mazingira; ukiishi nchi za kiarabu, kama mwanamke..utake usitake lazima uvae kutokana na mazingira, sidhani kuwa wanawake wote wanaoidhi nchi za kiarabu wanapendelea kujikanda nguo mwili mzima "wakati wote" lakini hawana uhuru wa kufanya hivyo. Lakini wale wanaoishi ulaya na magharibi wana uhuru, kwa hiyo inabaki uchaguzi wa mtu kufanya atakalo.

Wengi wangependa kuishi watakavyo, lakini sio rahisi kuishi utakavyo kwa sababu uko mwenye jamii, ingekuwa unaishi pekeyo, hapo sawa. Lakini ili ukubalike katika jamii Ni lazima uendane na nini jamii husika inataka, na ndio maana zikawekwa angalau kanuni, sheria zinazoiongoza jamii..
Nakubali kuna baadhi ya nchi kama hizo ulizotaja zina maadili makali juu ya mavazi ma matendo yao..lkn je hao wanaojifanya wafata maadili ndio wakiukaji wakubwa nyuma ya pazia...kwasababu hawaishi na zile kanuni wanazotaka wanafata mkumbo tu na ndio maana wengi wao huishia kuenda kinyume na maadili hayohayo...Hofu ya kwamba jamii itawatenga na kuwasinya inawatawala,uoga wa kwamba watapata reputation mbaya unafanya watu wasijiamini kufanya yale yanayowaridhia!
 
Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,815
2,000
Amelionglea hili jumla jumla ndio maana tunashindwa kuelewa ni vip fikra zinavyoaadhiriwa na maadili" maana kama fikra zinakutuma uwe mwizi ili moyo wako ufaurahi basi then useme maadili yankukosesha uhuru litakua jambo la taoafuti kabisa

Ndiyo maana nikamuuliza zinaathirir vipi? kama jamii inakataka mchepuko na wewe unapenda ndo athari yenyewe,au maadili ya jamii hayaruhusu kuzaa nje ya ndoa na wewe unapenda ndo athari hizo
 
kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,364
2,000
Haya maadili yamewekwa/yapo ili kuweka harmony kwa wote mfano upo nyumba ya kupanga au hizi nyumba zilizoshonana uswahilini ukafungua mziki mpaka juu/mwisho. Hapo utasababisha shida kwa wengine lakini wewe unaishi utakavyo.
Cc. gorgeousmimi
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom