Maadili ya ndoa yamepungua, wanaume hatuna raha

Maadili ya ndoa yamepungua, wanaume hatuna raha

bora kizazi chetu kinapita....nna wsws siku zijazo wanawake watakuwa wanapeleka posa kiumeni,,, ikiwa kwa sasa hivi wanajitolea mahari wenyewe....kikubwa tujaribu kuwakuza wanetu ktk misingi ya kiimani zaidi.
 
Birdman,

Heshima kwa sasa imepungua kwa sababu yale majukumu ya mwanaume mwanamke anayaweza kwa sasa wote ni watafutaji.

Umesema usiombwe pesa za matumizi na ilhali unataka heshima vitabu vya dini viko vizuri kabisa na hata hao wanawake hata awe na pesa vipi but huwa anajivunia akutunzwa na kupendwa na mmewe. So ukitaka heshima hua jukumu lako kama mwanaume.

Ndoa ni ya watu wawili na wote mnahitaji kuifurahia sio mmoja ndio asacrifice happiness yake.
Kula 5! Wao wanaamini mwenye haki ya kuwa na furaha kwenye ndoa ni mwanaume pekee! Mwanamke ni moja ya chombo cha kumfurahisha
 
Unajiita kichwa afu hela ya matumizi hutaki kutoa unategemea nani akutunzie mke na familia yako?

Unajiita mwanaume, halafu majukumu ya kiume huyataki unachotaka tu uheshimiwe thubutuuuu jiheshimu tu mwenyewe hakuna wa kukuheshimu
 
Uheshimiwe una nini cha kukupa Heshima??????? Fanya mambo mwanamke akikuona anapiga goti anapokea briefcase anasema this is my man!
 
Wanaume wengi wanajisahau kama wao ni vichwa.

Utakuta mume hajui watoto na mke wanakula nini, wameenda shule, wamelipa ada yaani yeye hajui kitu chochote kuhusu familia

Mama afanye biashara ndo alitunze familia, halafu una lalamika uheshimiwi? No jitambue kwanza kama baba na kichwa cha familia halafu fanya mjukumu yako yote, utalambwa hadi miguuni
 
wanaume wenyewe mna kauli mbiu siku hizi mnasema....mwanamke sura na umbo zuri....tabia mtavumilia ....sasa mvumilie
 
unajiita kichwa afu hela ya matumizi hutaki kutoa unategemea nani akutunzie mke na familia yako???
unajiita mwanaume afu.majukumu ya.kiume huyataki unachotaka tu uheshimiwe thubutuuuu jiheshimu tu mwenyewe hakuna wa.kukuheshimu


hahaaaa makavu live....
 
unajiita kichwa afu hela ya matumizi hutaki kutoa unategemea nani akutunzie mke na familia yako???
unajiita mwanaume afu.majukumu ya.kiume huyataki unachotaka tu uheshimiwe thubutuuuu jiheshimu tu mwenyewe hakuna wa.kukuheshimu
Shikamoo dada,u av said well....tena na zamzam yakununua luku lol
 
Wanaume Wa Siku Hizi Ni Laini Laini Na Wepesi Wa Kulia Lia,Unajiita Kichwa Afu Huwezi Kutimiza Majukumu Yako??
 
Uheshimiwe una nini cha kukupa Heshima??????? Fanya mambo mwanamke akikuona anapiga goti anapokea briefcase anasema this is my man!

Najua kuna changamoto nyingi sana kwenye suala hili aliloleta mtoa mada.lakini kuanza kudhani kwamba ili mtu apewe heshima ni hadi awe na kitu ni kuongeza tatizo sana!
 
Tatizo wanaume mnataka kushindana na mwanamke ...kusahau majukumu yako, kumpa majukumu mama makubwa , kutukuza marafiki kuliko mkeo na familia ...kama uongozi wako ndani ta nyumba upo kama wa mkuu wetu mzee wa tabasamu aiseee utajuta
 
Wanaume Wa Siku Hizi Ni Laini Laini Na Wepesi Wa Kulia Lia,Unajiita Kichwa Afu Huwezi Kutimiza Majukumu Yako??

wanaume wanahesabika ila wavaa suruali idadi ndo kubwa namie ni mmoja wao make kama ni suruali hata mi nnavaa
 
beijing is inversily proportional to raha ya mwanaume ya ndoa?
 
Siku Hizi Madada Mnajua Kujitetea Naona Mnatiririka Tu Ili Muonekane Mko Safi Kumbe Matatizo Mnayaanzisha Wenyewe
 
Iv mwanamme kama unanitunza vzr......unanipa heshima yangu kama mke.....hatugawani bili za umeme na maji!!!!!
HIVI KWANINI NISIKUHESHIMU KAMA MUME NA BABA MWENYE NYUMBA?
Lakin mwisho wa mwez unataka ufanye auditing ya Mshahara wangu iv ww unazan mm ntakuheshim kama mume.....give me freedom na uniheshim kama mke hata uo Mshahara wangu utauona na wala hutauulizia
 
Jamani lakini sio wote. wengine ndoa ni Paradiso ndogo, hata kama mume atakusaidia baadhi ya kazi zako ni sehemu ya upendo.
Misingi ya ndoa, inabainisha kwamba mwanaume wengine ni kichwa cha nyumba.Hivyo basi ni jukumu la mwanamke - msaidizi kuhakikisha kwamba kichwa kinafunction bila vikwazo ndani na nje ya nyumba.

Wajibu wa kwanza ni kumpa mume faraja kwa kila jambo jema na kutoa ushauri kwa mumewe. Sio kupinga faraja ni ya kimwili na physical and moral support.

Zingine zipo, lakini katika makundi hayo mawili,sasa nyinyi wanawake tukiishiwa mnahama mji,tukichoka na nyie mnadai mmechoka,mbona dini zote zina maadili sawa.

Wanawake wamekuwa viumbe wa ajabu siku hizi vyanzo vya stress na karaha katika kila nyumba. Mnajilinganisha na waume zenu kihali who said ni haki yenu, mwanamke aliumbwa amsaidie, amnyenyekee na awe kama mama mlezi wa mumewe.

Mume ni sawa tu na mtoto, ila mamlaka tofauti hisia na mahitaji ya kifikra ni yale yale - tubembelezeni tuwafae. Mume ni mfame wa kaya, ndivyo ilivyo, haitobadilika asilani, ni mamlaka tuliyopewa na Mola.

Jamani nawakilisha kwa waliooa mwonyeshe mkeo hili angalizo akumbuke kuamka mapema kabla hujaaamka na ole wako wanaoendekeza tabia ya kukubali kuletewa chakula na housemaid usile ni dhihaka.

Kesho wewe mwanamke mzee akirudi toka kazini, whether wewe pia ulikuwa kazini ama la, mpe offer ya massage 30 minutes na sketi yako la jeans ama suruali la blanketi ama kilimpulini mpe msichana wa kazi, mume anavaliwa satin, cotton, silk ama polyester na please chupi za A4 size achia wasio na mabwana.

Fanya hivyo mzee atakuwa na furaha na nyumba yako yenu itabadilika, na wewe mwanamke uliokuwa kichwa maji mwanzoni utakuja kutoa ushuhuda hapa,acha kumdai mumeo pesa ya matumizi omba pesa ya kuanzisha mradi.

Hiyo ni sehemu ya kwanza tutaendelea siku nyingine.
 
happy amos hapo ndio umesema nini sasa. Hebu soma ulivyoandika mwenyewe hapo kisha jiulize kama kweli ulikuwa serious.
 
Last edited by a moderator:
Wanawake siku hizi wamekuwa wababe noma. Hii Beijing thing inaharibu mila zetu
 
Back
Top Bottom