Maadhimisho ya nane nane mwaka huu yamefutwa?

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,159
9,359
Leo ni siku ya Wakulima Nchini! Siku hii huhitimisha wiki moja ya Maonesho ya Kilimo Nchi nzima ambako Wakulima naWafugaji hukutana na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Seekta yao!

Cha ajabu mwaka huu hakuna chochote kilichofanyika sijui kumetokea Nini!?Au Corona?!

Kama ndivyo mbona 77 ilifanyika ,mbona Mwenge unaendelea,mbona Matamasha ya Zuchu na wengine yanaendelea...kwa Ujumla misongamano ipo Kama kawaida.

Sasa ni kitu gani kimesababisha kusiwe na tukio hili muhimu mwaka huu?

Huku nchi yetu ikitegemea Kilimo kwa zaidi ya 65%?

Au ni dharau kwa Sekta hii?
 
Miaka yote yalipofanyika mkulima alifaidikaje? Kukosekana kwa maonesho hayo mwaka huu nini kilipungua? In short 7.7 na 8.8 hayanaga tija zaidi ya kuuza sura!
... you're right! Kama kuna public holiday za kipumbavu ni 7/7 na 8/8! Yote yako directly connected na chama la kijani hayana tija! Wafute hizi takataka warudishe mashujaa.
 
Mkuu kwa sisi wakulima yaalikuwa na tija kubwa sana ...tulijifunza na kupata mawazo mapya na solo la mazao yetu ...Nina mashaka na uelewa wako kwenye hii mada!
 
Yaani wiki ya Wakulima wewe hapo unakiona ni hiyo Holiday tu!
 
Nilipoenda 88 nilijifunza kuwa kuna mifimo mizuri ya umwagiliaji ya kutumia pump za solar.(Lorenz pump).

Wamecjemsha sana kufuta nane nane.

Nane nane kuna connection nyingi sana kama unaenda kimalengo.

Kama unaenda kutafuta malaya huwezi ona faida.
 
Mkuu kwa sisi wakulima yaalikuwa na tija kubwa sana ...tulijifunza na kupata mawazo mapya na solo la mazao yetu ...Nina mashaka na uelewa wako kwenye hii mada!
Achana na siasa za JF. Wadanganye wa saizi yako! Kama hayo mafunzo yana tija imekuwaje hadi leo nchi bado iko kwenye jembe la mkono il hali kila mwaka wanahudhuria maonesho ya nanenane?

Worse enough maonesho yenyewe kimkoa yanafanyika makao makuu ya mkoa, wakati wananchi wapo vijijini huko, hiyo teknolojia wataonea wapi? Ujingaujinga tu!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nilipoenda 88 nilijifunza kuwa kuna mifimo mizuri ya umwagiliaji ya kutumia pump za solar.(Lorenz pump).
Wamecjemsha sana kufuta 88.
88 kuna connection nyingi sana kama unaenda kimalengo.
Kama unaenda kutafuta malaya huwezi ona faida.
Baada ya kujifunza ulifanya nini? What transformation did you make? Tofautisha kwenda nanenane kuangalia events na real practice! Hiyo lotenz pumps uzitumiaje baada ya maonesho? Au baada ya nanenane ndo nitolee as usual?!
 
Kwa kusema hivyo unataka kutuambia aliyehailisha kutofanyika kwake alikuwa sahihi?.
Sahihi sana! Nothing ever came out of nanenane. Nothing! Kule watu wanaendaga kuuza samani za ndani, baloon za watoto, bia na nyama choma. Ufuska kwa mbaaali pia!
 
Baada ya kujifunza ulifanya nini? What transformation did you make? Tofautisha kwenda nanenane kuangalia events na real practice! Hiyo lotenz pumps uzitumiaje baada ya maonesho? Au baada ya nanenane ndo nitolee as usual?!
Nilikuwa nsha nunua pump ya petroli. Ninakusanya mtaji kwa sababu pump ya petroli inanigharimu sana ntaavhana nayo. Nimebadili mtazamo kuhusu umwagiliaji.
 
Sahihi sana! Nothing ever came out of nanenane. Nothing! Kule watu wanaendaga kuuza samani za ndani, baloon za watoto, bia na nyama choma. Ufuska kwa mbaaali pia!
Kwa hio hamtaki wakulima wakafurahi walau siku 1 kwa mwaka?
 
... you're right! Kama kuna public holiday za kipumbavu ni 7/7 na 8/8! Yote yako directly connected na chama la kijani hayana tija! Wafute hizi takataka warudishe mashujaa.
Inaonekana exposure yako ni ndogo sana

Wakati mwingine ni bora mkae kimya kuliko kuongea upuuzi,, eti 77 au 88 ifutwe

Haya maonesho hukutanisha wazalishaji na wauzaji Bidhaa mbalimbali zenye ubunifu tofauti na zingne zilizokosa platform ya kufahamika vyema machoni pa watu, hvyo wanatumia haya maonesho kujifunza kutoka kwa stakeholders , kuongeza ujuzi na kupata connections mbalimbali za kimasoko

Watu hupata deals nyingi sana baada ya haya maonesho
 
... you're right! Kama kuna public holiday za kipumbavu ni 7/7 na 8/8! Yote yako directly connected na chama la kijani hayana tija! Wafute hizi takataka warudishe mashujaa.
wewe sabasaba ina umuhimu japokuwa sijawahi kwenda nilikuwa nikiangalia kwenye tv tu.hata nane nane nayo sikukuu nzuri.nilipokuwa o level nilihudhuria sikukuu ya nane nane pale morogoro.nilijifunza mengi..mfano ufugaji wa samaki na Bata....nikatembelea na kituo Cha mamlaka ya hewa tukaelekezwa jinsi anemometer inavyofanya kazi
 
... mkuu when was that? Duna imebadilika; yote hayo ukiwa umepunzika kitandani pako unayaona tena kwa njia ya video kupitia simu janja yako. Ni lazima tuende na mabadiliko tuache kuishi kwa mazoea.
 
Mkuu kwa sisi wakulima yaalikuwa na tija kubwa sana ...tulijifunza na kupata mawazo mapya na solo la mazao yetu ...Nina mashaka na uelewa wako kwenye hii mada!
Kuuza nguo za mitumba88 zinamsaidia nini mkulima?
 
Sahihi sana! Nothing ever came out of nanenane. Nothing! Kule watu wanaendaga kuuza samani za ndani, baloon za watoto, bia na nyama choma. Ufuska kwa mbaaali pia!
Katika maisha unaona kile unachokiangalia, unapata kile unachotafuta.
Nane nane umekuwa ukitazama samani za ndani, bia, nyama choma na ufuska kwa mbaali na uliyaona hayo.

Kwa wale waliokuwa wanatafuta breed mpya za wanyama, mbolea, ushauri wa kilimo na ufugaji waliyapata hayo waliyoyaangalia.

Uwepo wa bia pia si tatizo maana mtu katoka kijiji cha mbali kuja kununua trekta amefanikisha kununua akikaa akanywa bia kuna tatizo? Hivyo hivyo uwepo wa huduma za vyombo vya ndani na mambo mengine si kigezo cha msingi cha kusema hizi sherehe hazifai.

Mke wa mtu na mama kaenda kupata ushauri kutoka kwa wataalam wa ufugaji, ameshaupata, akinunua karai kurudi nalo nyumbani kuna tatizo?
 
Back
Top Bottom