Ma-MC mnatusababishia shida sana kwenye familia zetu, Tabia hii ni mbaya mno

Last Seen

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
223
549
Habari za Asubuhi wana-Jukwaa.

Kabla ya yote nawapongeza ma-Mc kwa juhudi zao wakipambania chakula kiende kinywani...

Nimesikitishwa sana baada ya kuonekana kwenye video fupi iliyopostiwa na MC fulani bila idhini yangu, tulikuwa tunacheza na watu wengine tuliokutana ukumbini... SIJAPENDEZWA!

Ma-MC ifike mahali wawe wanaomba idhini kwa wahusika, akiridhia sawa asiporidhia si sawasawa kuipandisha kwenye mitandao ya kijamii. Tuna wake, watoto na nafasi kidogo katika jamii.

Unakuta mdada kavaa nguo ya sherehe, anafurahia ndugu, rafiki kaoa/kaolewa bahati mbaya akatumia kilevi kikamkolea, akijiachia kucheza tuu...kesho yuko kwenye page ya MC fulani.

Jipromotini bila kudhalilisha wengine.

Huyu MC ntakula nae sahani moja!

Nahitaji anilipe Fidia ya bilioni moja kwa kadhia zote nilizozipata baada ya kupost video ile.
 
Endeleeni kujifungia kifamilia, mkija public mjiheshimu mkifanya kituko mtajikuta whatsapp grps Tz nzima
Wakati mwingine hawa ma-MC hata tukio la kawaida wanaweka kwenye mitandao na unajua kila mtu ana tafsiri tofauti juu ya jambo, hapo ndio tafrani inapoanza, sio swala la kutokujiheshimu, watu mnapokua kwenye sherehe maana yake mnafurahi na kucheza sasa mtu unachukua video unaweka kwenye mitandao bila kujua mapokeo ya jamii na tafsiri zake sinaweza kuathiri familia kiasi gani

Else watu wakae kwenye sherehe kama vile wapo msibani, hakuna kufurqhu,kucheza wala kujiachia
 
Habari za Asubuhi wana-Jukwaa.

Kabla ya yote nawapongeza ma-Mc kwa juhudi zao wakipambania chakula kiende kinywani...
Unakuta mdada kavaa nguo ya sherehe, anafurahia ndugu, rafiki kaoa/kaolewa bahati mbaya akatumia kilevi kikamkolea, akijiachia kucheza tuu... kesho yuko kwenye page ya MC fulani.
 
Jiheshimu kwanza wewe mwenyewe usifanye kituko mbele ya jamii haswa katika kipindi hiki cha teknolojia ya simu (video)

Kuna siku niliwahi kusimamishwa na trafiki tukawa kama hatuelewani (ubishi kidogo) jioni si nikakutana na video kwenye group la familia watu wanasema huyu si fulani ilikuwaje
 
wakati mwingine hawa ma mc hata tukio la kawaida wanaweka kwenye mitandao na unajua kila mtu ana tafsiri tofauti juu ya jambo, hapo ndio tafrani inapoanza, sio swala la kutokujiheshimu, watu mnapokua kwrnye sherehe maana yake mnafurahi na kucheza sasa mtu unachukua video unaweka kwenye mitandao bila kujua mapokeo ya jamii na tafsiri zake sinaweza kuathiri familia kiasi gani

Else watu wakae kwenye sherehe kama vile wapo msibani, hakuna kufurqhu,kucheza wala kujiachia
Kama ni kucheza tu pana ubaya gani? Si ndio maana ulicheza hadharani. Lazima kuna kitu kitakuwa hakiko sawa ndio maana hofu yakushika
 
Hao ma-MC hawajui kitu kinaitwa privacy? kuweka picha ya mtu au tukio la kifamilia mtandaoni bila idhini ya wahusika hiyo ni breach of privacy, na huyu jamaa yupo sahihi kusema anaweza kumshtaki.....
 
wakati mwingine hawa ma mc hata tukio la kawaida wanaweka kwenye mitandao na unajua kila mtu ana tafsiri tofauti juu ya jambo,
Wote tuna macho na ufahamu tukio la kawaida haliwezi kukutia hofu ya kupostiwa.
 
Habari za Asubuhi wana-Jukwaa.

Kabla ya yote nawapongeza ma-Mc kwa juhudi zao wakipambania chakula kiende kinywani....
Sheria ya taarifa binafsi na faragha inakuja hivi karibuni, unaweza kujikuta unakula bilioni kadhaa kwa kukudhalilisha.

Kisingi sheria itahitaji idhini kwa kila taarifa binafsi ya mtu
 
Back
Top Bottom