Ma-manzi wa Dar na fake lifestyle

Ma-manzi wa Dar na fake lifestyle

Mkuu natokea mkoani kabisaaaa....na huwa tunajulikana kabisa sijui kwanini....nina mifano hai mingi sana huwa kila nikija Dar hata nikikaa Bar nashangaa narukiwa na warembo mara atauliza hiki kiti kina mtu au vipi.....na hapo kuna wengine viti vingine vitupu...au sijui tunavyovaaga suits za mikoani na joto lile Bar na hapo unaonakana umeshushwa na 'SU'
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Sio wanawake wote wana njaa kiasi hicho mkuu. Nadhani kuna alivyoviona kutoka kwako ambavyo ndio vilimshawishi na kuona kwamba hawezi kosa kitu.

Ila yataka moyo aisee. Ndugu wapo watu wa karibu wapo unaanzaje kumuomba pesa mtu usiyemjua aisee.

Pia upande wa pili wa shilingi kama unacho msaidie tu mkuu ili babake apate kutoka huko aliko. Hahahaaa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wacheza ngumi hulipwa,
Yeye anapiga ngumi wamchangie wengine kazi kweli,
Akae Rumande itapendeza.
 
Sasa wewe kashakwambia mzee wake yuko Central we unamuuliza tena kituo gani!

Anyways yawezekana alikuwa anataka akupige ila pia usiache kuangalia uwezekano wa kuwa ana shida kweli, unajua mtu unapokuwa na shida huchagui mahali pa kuomba msaada hasa hasa kama shida yenyewe ni dharula na yahitaji uharaka.
 
Sasa wewe kahakwambia mzee wake yuko Central we unamuuliza tena kituo gani!

Anyways yawezekana alikuwa anataka akupige ila pia usiache kuangalia uwezekano wa kuwa ana shida kweli, unajua mtu unapokuwa na shida huchagui mahali pa kuomba msaada hasa hasa kama shida yenyewe ni dharula na yahitaji uharaka.
Babake kashindwa kulipa 25% ya mnada, msaidie. Mtoto wa Dr L.S
 
Hivi ninyi mmekuwaje

Kwan mpaka muwe mmekaliana uchi ndo akuombe hela?

Ni dhambi kukuomba km rafiki?
 
Back
Top Bottom