Ma-HR please help | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ma-HR please help

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by bornagain, Feb 6, 2012.

 1. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mimi ni mwajiliwa kwenye kampuni ya mwekezaji hapa Tanzania, mkataba wangu unasema km nitataka kuresign nitoe notice period yamwezi mmoja au nitoe mshahara wangu mzima wa mwezi mmoja km sitaweza kutoanotice ya mwezi mzima. Je kuna madhara gani kama nikipewa mshahara wangu tarehe25 ambapo ndo mshahara unatoka then kesho yake nikatoa resignation ya siku tanokwa ajili ya handover na pia nisiwalipe mshahara wangu wa mwezi mzima nikaondoka zangu? Na bear in mindthat sehemu nayoenda kufanya kazi wanatumuia NSSF so sitahitaji kuichuantaiendelezea huko ntakapokwenda kufanya kazi.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Kama unaondoka na unaenda fanya sehemu nyingine
  Kwa nini ufanye ukanjanja??
  Au huna mpango wa kufika mbali siku moja??

  Acha ukanjanja, kuna industries/professionals siku hizi wanawaweka kwenye blacklist
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  ni vyema ukiondoka mahali ondoka kwa heshima

  kama utaondoka tar 25 kuna tatizo gani ikiwapo notice leo?
   
 4. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unapo ondoka kwa kuaga unaongeza CV yako. Pia utaweza kuendeleza nssf yako upatapo kazi upya. Lakini kama huna baruwa ya kuacha kazi itakuwa ngumu kujulisha hisabu za sehemu zote ulizo fanya kazi. Jenga CV nzuri for a brighter future.
   
 5. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Asante sana wakuu kwa ushauri mzuri, naahidi kufuata utaratibu wote ili niondoke kwa heshima maana kuna kamsemo kuwa "do not shit on the pot just because you are leaving, you might come back to cook in the same pot"
   
 6. m

  muhanga JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwa kuwa unalijua hili mbona ulitaka kuharibu bure? kuaga ni uungwana tena hauhitaji kwenda shule, huyo muajiri kubali au kataaa kuna mahali amekuinua kwa hiyo si vema ukatimka kihuni as if umeiba. si kwa ajili ya NSSF ila kwa kuwa ni uungwana na ndio sheria/mkataba unakutaka ufanye hivyo.. ulisaini mkataba ukitaka kuondoka wewe uttoa notice au full salary in lleu of notice, na muajiri pia either akunotify mapema au akulipe mshahara, sas akwanini usiheshimu mkataba?
   
 7. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ni vizuri umepewa maelekezo aya na ufuate
  shida wafanyakazi uwa tunaondoka kwa vumbi sana,ihali unasahau uyo mwajiri wako ndio good reference yako uko unakoenda,mana lazima wajue apo new employment umetoka kwa lipi labda wakuibe wao!!
  mwishowe unakuta mtu anarudi "kwa siri" kuomba msaada kwa previous mwajiri,tuondoke kwa utaratibu tu km mikataba inavotuonyesha
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Act no 6.
  Section 41. Sub. Sect. 1 A contract of employment can be terminated on notice, the period of notice shall not be less than,
  Sub. Sect. 1 (a) Seven days, if notice is given in the first month of employment;
  (b) (i) 4 days, if the employee is employed on a daily or weekly basis
  (ii) 28 days if the employee is employed on a monthly basis.

  Bornagain,
  Kama bado unataka kufika mbali katika maisha hakuna sababu ya kupiga chenga, aga kwa upendo na amani tu uende ukiwa salama, utengeneze cv nzuri. Hata siku ukikwama huko unakoenda, ukirudi upokelewe tena.
  Vinginevyo ningekuambia Mtukane kiongozi wako, uitwe tu kwenye Disciplinary Hearing, then itakuwa Termination on the Ground of Misconduct, ambayo unaweza kuwa na faida kama uliajiriwa huna hata mwaka, na mwajiri anaweza kukulipa mshahara wa mwezi mmoja badala ya notice. lakini kama una muda mrefu itakuwa hasara ukiachishwa kwa utovu wa nidhamu (Misconduct), kwani utakosa Severance pay ambayo ni Mshahara wako wa Siku saba kwa mwaka mara Miaka uliyofanyia kazi.
  Suppose unalipwa labda 650,000/=, inabidi ugawanye kwa 30 mara 7 mara miaka labda 6 = 910,000/=
   
Loading...