Ma celebrities wa Bongo ni Kiio cha jamii????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ma celebrities wa Bongo ni Kiio cha jamii?????

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Sumba-Wanga, Dec 10, 2011.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Just thinking aloud...... Mimi ni msanii kioo cha jamiii! Nimekumbuka hiyo clip na kuifananisha na Celebrites wa Bongo. Most of these celebrities wame relax, wanaona kama vile wamefika mwisho (Ray the greatest). Wengine ni catalogues, vinguo vya nusu uchi na kujirusha sana (Wema, Auntie Ezekiel, Irene). Ukisikia kuna shughuli wamealikwa, basi kaa tayari uone moto wao!!!!!. Sasa hapo ni mwisho wa upeo wao wa kujua majukumu yao kwa jamii? Ukiangalia dhana ya msanii kioo cha jamii, unanona kuna mengi zaidi wanatakiwa kufanya. Kwanza, kwa wale wanaovaa nusu uchi, basi ndio taswila ya kwa jamii? Okay hili ni dogo sana na sio mUhimu. Nimeweka hii thread hapa ili niwakumbushe kwamba u celebrities hauishii kwenye matanuzi pekee, lakini jambo la muhimu zaidi ambalo nadhani ni wachache sana wamelifanya (Jokate, Kanumba, Hoyce Temu), ni kuwa balozi wa jambo fulani katika jamii. Kwa mfano, Irene, Auntie ezekiel, Wema ambao ni maarufu sana kwa mavazi ya nusu uchi angeweza kuwa balozi wa Condoms! Angevaa nguzo zake za nusu uchi, lakini angeweza ku capture mind of the people at the right time kwa kuwakumbusha watumie condoms....... Wengine kama wakina Ray e.t.c wangeweza kuhamasisha hifadhi ya mazingira na mengine....Juzi juzi ilikuwa ni World Aids Day, Celebrities wetu wangeweza kujikusanya na kutoa ujumbe kwa jamii........ Hata ma miss wetu utawaona wako busy kutembelea watoto wa mitaani wakati wanatafuta U-miss, baada ya hapo hutawasikia tena, wanakuwa busy kugombaniwa kama mpira wa corner na ma pedejee wakware huko mitaani! Nina imani kwamba kama wangefanya hivi, bas wangekuwa na impact kubwa sana kwenye jamii, tofauti na walivyo watu wa matanuzi kwa sasa. Najua matanuzi ni right yao ya kikatiba, lakini kama celebrity.... more is expected from you...Kama hamjui, basi tafuteni ma promoters/managers ambao watawaelekeza nini cha kufanya. Hata wale ma Celebrities wa Hollwood wana managers..... Hao niliotaja ni mfano tu, the list is endless
   
Loading...