M4C yashika kasi Geita

kanta

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
343
Reaction score
65
Makamanda wa CHADEMA Geita wapo kwenye kata ya Kalangalala wakipiga kaziya kutoa elimu ya Uraia.

Wanasema CCM kwa njia za kistaarabu hawataki kutoka,wametumia vibaya rasilimali za hii nchi hivyo wanaogopa kutoka kwa kuwa watafikishwa mbele ya sheria na kufungwa.Wanasema serikali makini lazima itokane na watu makini,serikali ya CCM si makini.
 
Kazi njema makamanda.mkipata muda muwe na mnamtumia na kamanda mawazo.huyu ni mwiba kwa ccm kanda hii ya ziwa
 
Na nyie Chadema sasa mnakomoli! Leo Slaa yuko Tunduma (Mbeya); Kigaila yuko Mbeya Mjini anaendesha mafunzo ya makada wa chama; Mnyika, Mdee na makamanda wengine wako Mlandizi (Pwani); Tundu Lissu yuko Iringa; makamanda wengine wanaojulikana na wasiojulikana wamesambaa vijijini nchi nzima - kuanzia Ruaha, Arusha, Lushoto, n.k. CCM wana haki ya "kuelimishwa". Na hapo tunaambiwa mpango mzima ndio kwanza bado; Kanda hazija-take off inavyotakiwa; si itakuwa supper.
 
Hakika kila kona ni kuyabana masisiem maana yanajampa hovyo hovyo tu...kizazi hiki kiamke na kiukatae udhalimu...
 
Imekaa vizuri...Viongozi wa majimbo wapewe Ratiba ya kila mwisho wa wiki kufanya mikutano kwenye majimbo yao...kazi ya kunadi sera za CDM na pia kuwaelimisha wananchi haki zao ni muhimu sana kuelekea kwenye uchaguzi mkuu 2015...
 
Huyu ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Geita ambaye amevua gamba na kuvaa gwanda mapema mwaka huu akihutubia umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa M4C.Hakuna kulala mpaka kieleweke.
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1368295364365.jpg
    115.7 KB · Views: 151
Nimeishi sana Geita naifahamu vilivyo na nimetoka huko kuja hapa Dar katikati ya mwaka jana,ni vigumu sana kwa CHADEMA kuchukua kata ya Kalangalala kwa sababu kwenye eneo hilo bado watu wana ushabiki wa mdomoni lakini sio wa moyoni.nasema hivyo kwa sababu mwaka wa Chadema kuchukua jimbo hilo ilikuwa ni uchaguzi wa mwaka 2010 uchaguzi uliomuingiza madarakani Donald Max,huyu Max alikuwa hapendwi hata ha WanaCCM wenzake na walitoa ushirikiano Mkubwa sana kwa CDM lakini mwisho wa siku wakashindwa,natambua kwamba Max harudi Bungeni uchaguzi ujao lakini jimbo ni vigumu kwenda CDM isipokuwa litachukuliwa na mtu mwingine kupitia CCM.
 

Aliyekua Katibu wa CCM Wilaya ya Geita Bw.Ntinonu akihutubia umati mkubwa wa wananchi.
 
chadema achieni ccm ipumue,kila kona ya nchi jamani!
 
Hii ndio timu yenyewe ya M4C geita,hakuna kulala mpaka kieleweke,CCM ipo ICU,hawalali kwa dababu ya CHADEMA?
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1368295725567.jpg
    114.8 KB · Views: 127
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…