" Kama tunafikiri tumehuzunika na hukumu dhidi yangu ya kuvuliwa ubunge , hekima na busara sio kukaa chini na kuanza kulia bali twendeni kwa hasira zetu tukawakomboe wengine na mateso ya ukandamizaji kama huu na sasa huu ni wakati wa kufanya siasa ya ukombozi nchi nzima bila kurudi nyuma , najua matokeo yake mnaweza msiyaone mapema lakini ukweli ni kwamba haki imekaribia kutwaa taifa hili , tutachoka sana lakini kuchoka kwetu kuna maana kubwa , wapo waliofurahi sana kwa sababu ya ushabiki hao wanahitaji huruma yenu na mafunzo kwani hawaioni kesho vizuri, lakini watambue kuwa sio lazima uwe Mbunge ili uweze kufanya siasa ya ukombozi , kama ambavyo Martin Luther , Malcom X na wengine hawakuwahi kuwa Wabunge ila walifanya kazi ya ukombozi wa Nchi zao , hata hivyo Arusha poleni sana . Lema ( maneno yake baada ya kuvuliwa ubunge)