Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mgombea wa Urais anayetarajiwa kupata ushindi mkubwa Tundu Lissu leo ataitetemesha Chato na viunga vyake katika kampeni zake zilizoivuta Dunia.

Taarifa kutoka ndani ya Team yake ya Kampeni kabla ya kuhutubia mkutano wa Hadhara atautembelea Uwanja wa ndege wa Chato uliozua gumzo nchini kote kutokana na Ujenzi wake.

Tundu Lissu amepata uungwaji mkono mkubwa kutoka Makundi yote ya Jamii hususan Wafanyakazi ambao wanalaani kupitishwa kwa sheria Haramu ya kupora Mafao yao. CCM na Serikali yake walipitisha sheria ya kuzuia Mafao ya Wafanyakazi hata Kama ameacha kazi akiwa na miaka 30 haruhusiwi kupewa haki yake ya mafao mpaka afikishe miaka 60.Sheria hii Haramu imelaaniwa na kila mfanyakazi na Tundu Lissu ameapa kuifutilia mbali Mara tu baada ya kuapishwa.

Ingawa Chato ni nyumbani kwa mgombea Urais wa CCM Lakini kwa muda mrefu CHADEMA imekuwa na uungwaji mkono mkubwa na inao wafuasi wa kutosha.Mmoja wa makamanda mashuhuri wanaotokea Chato ni mwanamama Husna Amri ambaye anajulikana nchi nzima kwa ujasiri wake.

Tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika mapokezi na Mkutano wa Kampeni hapa Chato.

PIA SOMA
Uchaguzi 2020 - Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe
-------------------------- --------------------
Yanayoendelea saa 4 Asubuhi




Mgombea wa Urais Tundu Lissu amekutana na wanachama nje ya Hoteli aliyofikia mjini Kahama kabla ya kuondoka kuelekea kwenye kampeni.

Lissu amesema Jana usiku mgombea Ubunge CHADEMA Jimbo la Chato alivamiwa na kuharibiwa Mali zake na maharamia wanaifanyia hivyo ili kumtishia asiende Chato.

Lissu ameonya hatatishika na ataingia Chato na kufanya mkutano Mkubwa wa Kampeni.Lissu ameitaka Dunia kutega masikio kuelekea Chato leo jioni.

Kabla ya kuhutubia Chato jioni hii Lissu anatarajiwa kufanya kampeni maeneo ya Mbogwe na Bukombe

Picha hapa Chini ni Lissu akiwa Chato.

IMG-20201012-WA0072.jpg
IMG_20201013_193420_313.jpg
IMG_20201013_193424_533.jpg
IMG_20201013_193428_208.jpg

Video haoa chini ni Lissu akiwa Bukombe

Video hapa Chini ni Lissu akiwa Runzewe
 

Attachments

  • VID-20201013-WA0050.mp4
    8.1 MB
  • VID-20201013-WA0067.mp4
    37.4 MB
Nahisi watamzuia kutembelea huo uwanja.Na kwakuwa huko ni nyumbani kwa mgombea yule,nina wasiwasi pia anaweza fanyiwa hujuma katika kampeni zake huko lengo kuhakikisha hapati watu au ashindwe kuhutubia.

Ni imani yangu Lissu haendi kufurahia uwanja,bali anaenda kufanya tathimini physically ya huo uwanja kwa kuingilia kilichojengwa (kupata picha ya kilichojengwa) na ulazima wake pamoja na umuhimu wa kujenga uwanja katika eneo hilo.

Ushauri:Tundu Lissu vaa helmet muda wote ukiwa huko Chato na kuwaambia wananchi kila mtu awe mlinzi kwa kumtupia macho alie jirani yake katika mikutano na misafari atayofanya huko Chato(kwenye msafara wa mamba, hata kenge wamo).

Nasema hivi kwasababu,teyari dalili zinaonyesha kuwa lolote linaweza kutokea leo hii, hivyo ni bora kuchukua tahadhari zote zinazowezekana kuchukuliwa.
 
Leo mwanachato watuambie je Chato international airport imewanufaisha vipi?

Je, tangu 2017 mwanachato gani ameutumia huo uwanja? barafu alipiga kelele sana humu JF kuhusu huu uwanja tangu 2016.

Usije baadae ukageuka ni malisho ya mifugo.

Watumbie je taa za barabarani zimewaletea vip maendeleo au zimekuwa kama sehemu ya kuongozea maguta ya punda?

Vipaumbele binafsi vya mtu kuvifanya kuwa ndo vibaumbele vya Taifa ni hatari kwa kuwa huzaa "white elephant project"
 
Kuna watu sijawahi ona, uwanja wa Chato uwanja wa Chato, hivi Chato ni wananchi wa wapi? Wao hawana haki ya kuwa na uwanja? Mbona mnakuwa wapumbavu kiasi hiki?

Mnatukana kila siku Chato utafikiri wao hawatakiwi kuwa na uwanja. Kwa taarifa yenu wananchi wa Chato si wajinga, muulizeni mgombea wenu alichokipata Buselesele na Katoro hadi akasitisha kwenda Chato, haya yote ni siasa mbovu isiyo na staha, hata kama unachallenge tumia lugha rafiki, don't be so biased to that extent, watu wa Chato amewatukana sana, Buselesele na Katoro yalikuwa maeneo ya upinzani lakini kutokana na dharau za Lissu matokeo yake CHADEMA leo inazomewa, Lissu asingezomewa Buselesele kwa namna ile, Awe na akiba ya maneno kwani anaowatukana wanasikia .

Inashangaza sana unatukana halafu bado eti unaenda kuwaomba kura, unatukana barabara kujengwa huku unazitumia, unatukana ndege huku unazipanda huo ni U CHICHIDODO.

Hopeless kabisa , let's stay tuned leo.
 
121 Reactions
Reply
Back
Top Bottom