Kweli Chadema hawafanyi makosa! Nilimcheki kamanda akihitimisha baraza la M4C jana huko Ndanda pale alipowakumbusha kuwa CCM ni marehemu na wawe makini kung'amua hilo. Niliachwa hoi na art aliyotumia na kuwaacha hoi halaiki iliyokuwa inamsikiliza. Kwa maneno yake mwenyewe alisema:
"Kupe; si mnamjua kupe? Kupe akishamndandia ng'ombe yeye basi keshamaliza safari. Ng'ombe anapelekwa gulioni kupe yupo; ng'ombe anauzwa kupe yupo; ng'ombe anachinjwa kupe yupo tu; ng'ombe anachunwa ngozi kupe yupo tu; ngozi ikianza kuchomwa ndo kupe anazinduka, 'alaa, huyu jamaa kumbe kachinjwa!'
Waosha magamba mpooo?
Kwani hujui ccm ni kupe?Sasa ndio nini hicho?
Mlitika= Mtikila , umechakachua tu kiaina lakini bila kuongeza wala kupunguza herufi jina lako ni mtikila

Yaani amefanya chini juu, juu chini. Halafu bado anabisha.Ukisikia ambiguity ndiyo hiyo hapo kwenye RED inayofuatiwa na BLUE. Sina haja ya kusema mengi kwa kuchelea mada husika kuitoa toka kwenye mwelekeo uliokusudia!!!
Hata mimi niliiona hiyo. Jamaa aliniipress sana. Afu umati ulikuwa nyomi mbaya. Makamanda naona wamejipanga sana safari yao ya kusini. nilisoma hapa JF hii ratiba ya Dr. wa ukweli, A.K.A. Prof. Slaa:
Katibu mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa ameelezwa kuwa mpiganaji asiyechoka kutokana na kazi kubwa anayofanya huko kusini tangu CDM ianze operesheni Okoa Kusini wiki moja iliyopita.
Taarifa kamili zinasema Dr Slaa amekuwa akihutubia mikutano mitatu kila siku ambapo kwa siku zote hali chakula chochote mchana kutokana na kubanwa na muda.
Baada ya mikutano Dr Slaa anaongoza mikutano ya ndani mpaka saa 6 usiku na kisha anakuwa wa kwanza kuamka na kuwaamsha vijana wake waanze siku nyingine ya mapambano.
Imedaiwa pia kabla ya kila mkutano Dr Slaa anazindua matawi katika mitaa yote ya eneo husika.
Source: Kamanda Mwesilwa Perfect aliyeko kikosi kinachoongozwa na Dr Slaa katika opere
Nahisi hii ndiyo ratiba ya makamanda wote huko kusini.
"Kupe; si mnamjua kupe? Kupe akishamndandia ng'ombe yeye basi keshamaliza safari. Ng'ombe anapelekwa gulioni kupe yupo; ng'ombe anauzwa kupe yupo; ng'ombe anachinjwa kupe yupo tu; ng'ombe anachunwa ngozi kupe yupo tu; ngozi ikianza kuchomwa ndo kupe anazinduka, 'alaa, huyu jamaa kumbe kachinjwa!'
Dah wanadamu wanamisemo! hii kali
Sasa ndio nini hicho?
Majembe ni mengi sana, hadi 2015 mengine mengi yatafahamika tena ya ukweliAisee hata mimi nilikuwa sijawahi kumsikia kabla. Dogo jukwaa analimudu.
Mkuu watu kibao waligoma kuwa wajinga. Kamanda alikusanya kadi za magamba karibu ajaze sandarusi na kuwakabidhi Kadi za Ukombozi