M4C Masasi yadoda, yahitajika nguvu ya ziada

master gland

Senior Member
Apr 3, 2012
198
60
Wanabodi,

Leo kulikuwa na mkutano wa hadhara Masasi watu ni wachache mno (hawazidi 500)inavyoonesha wananchi wa huku bado hawajaupokeo wito wa M4C.

Inavyoonesha mkutano haukutangazwa ipasavyo -matangazo yalikuwa kupitia bodaboda hivyo wengi hawakuwa na taarifa ya mkutano.

Kwenye mkutano mwenyekiti wa CDM wilaya alitoa hamasa kwa wananchi kujitambua ili wapate ukombozi wa kweli.

Mwisho kadi ziliuzwa na wanachama wapya wapatao ishirini walipatikana.

Ila shortcoming kubwa kwa uongozi hakuna mwanachama yeyote mpya aliyeandikishwa kwenye daftari zaidi ya kuuziwa kadi tu.

MY TAKE
1. CDM TAIFA , bado wana kazi kubwa ya kupromote M4C hapa Masasi
2. Uongozi wa wilaya ujitathimini upya ili ufanisi wa kichama uonekane dhahiri
3. Usajili wa wanachama wapya uendeshwe kwa utaratibu unaoeleweka
4. Vijana wanaonesha kuamka hapa Masasi ila mikutano ya mara kwa mara ifanyike kuaamasisha muamko
 
Wana jamvi, mi nilidhani huku kusini baada ya ule moto kuwashwa na viongozi wa kitaifa nilidhani ulizima, kumbe ni tofauti leo nimepita maeneo ya Masasi huku Mtwara, kata ya Mkuti nimekuta M4C chini ya chini ya viongozi wa Wilaya tu.
Makubwa waliyosema:
1. Elimu ya uraia kuhusu propaganda za kidini, kanda na ukabila kama zinavyoenezwa na CCM.
2. Mbunge wao toka Masasi hawakumtuma kwenda kuomba condoms, bali wanahitaji namna atakavyohangaikia soko la korosho
3. Wamefafanua kuhusu suala la namna viti maalumu CDM vinavyopatikana hata mie nimejifunza nilikuwa sijui, jamaa ni walimu wazuri ingawa nasikia M/kiti wa CCM anaita kuwa hao jamaa ni vipanya vidovidogo lakini ankiri vinamsumbua

Nilivyomdadisi mmoja kuhusu huko vijijini akaniambia kiukweli kazi ngumu waliyonayo ni hapo kata za mjini lakini vijijini anasema kazi ni rahisi sana.

Binafsi nimefurahi kuwa M4C kumbe si lazima awepo Mbowe, Slaa au Kiongozi yeyeote wa kitaifa au maarufu, wakati mwingine inanoga kama inasimamiwa na kila mtu ndani ya chama.

kila la kheri wapenda mabadiliko
 
Ni kweli lakini inategemea unaangalia katika jicho gani, binafsi nimepita pale kama ni pale chini ya mti ulipokuwa ule mkutano, binafsi naona kuna hatua nzuri na viongozi wale wilaya wantakiwa kuungwa mkono ni hatua nzuri. Idadi ile ya watu kwangu mie naona i wengi kwa eneo kama la Masasi ambalo siasa za upinzani hasa CDM bado ni changa.

Viongozi wana uwezo wa kueleza baadhi ya hoja za msingi na kikubwa ni kwamba vijijini wanafanya vizuri. Jamani kwa CDM ambayo wakati mwingine huko chini wale vijana ngazi ya wilaya wanalazimika kutumia raslimali kidogo walizonazo, ule mkutano si wa kubeza kiasi hicho kwangu mimi ni mafanikio mazuri na jitihada zinatakiwa kuongezwa
 
Mkuu ,
Mimi binafsi nilikuwepo kwenye huo mkutano watu ni wachache muamko bado upo chini na jitihada za haraka zinahitajika ili kuwang`oa magamba hapa Masasi ila waliokuwepo walionesha kuunga mkono M4C na wamenunua kadi wapatao wanachama 20
 
Wana jamvi, mi nilidhani huku kusini baada ya ule moto kuwashwa na viongozi wa kitaifa nilidhani ulizima, kumbe ni tofauti leo nimepita maeneo ya Masasi huku Mtwara, kata ya Mkuti nimekuta M4C chini ya chini ya viongozi wa Wilaya tu.
Makubwa waliyosema:
1. Elimu ya uraia kuhusu propaganda za kidini, kanda na ukabila kama zinavyoenezwa na CCM.
2. Mbunge wao toka Masasi hawakumtuma kwenda kuomba condoms, bali wanahitaji namna atakavyohangaikia soko la korosho
3. Wamefafanua kuhusu suala la namna viti maalumu CDM vinavyopatikana hata mie nimejifunza nilikuwa sijui, jamaa ni walimu wazuri ingawa nasikia M/kiti wa CCM anaita kuwa hao jamaa ni vipanya vidovidogo lakini ankiri vinamsumbua

Nilivyomdadisi mmoja kuhusu huko vijijini akaniambia kiukweli kazi ngumu waliyonayo ni hapo kata za mjini lakini vijijini anasema kazi ni rahisi sana.

Binafsi nimefurahi kuwa M4C kumbe si lazima awepo Mbowe, Slaa au Kiongozi yeyeote wa kitaifa au maarufu, wakati mwingine inanoga kama inasimamiwa na kila mtu ndani ya chama.

kila la kheri wapenda mabadiliko
Kuna thread ingine ambayo inasema M4C Masasi imedorora,tumuamini nani?
 
Mkutano wa chama pinzani kupata watu 500 Masasi si hatua ya kubeza hata kidogo!!labda kama ulimaanisha 50 hapo ningejiuliza mambo mawili matatu viva CDM pamoja tutashinda.
 
good that the spanners are at work
Mkuu toa mawazo ya kujenga huo ``what do you mean spanners at work''?
I`m real reporting what happened what to do is how can be supported to make the significance achievements
That`s a reality without propaganda
 
Ongereni wana masasi mtwara si watu wa mwanza tunawatakia kila la kheri lakini kumbukeni ccm haiwezi kubadilisha maisha yenu mnatakiwa mjipiganie wenyewe sisi huku tumekwisha silimu kila kitu safi yaani mteremkoooo
 
hatua sio mbaya kwa 500 tukazeni kamba 2015 ni karibu sana hata kama CDM haifahamiki sana masasi lakini kikubwa ni kukomaa ili tupate watu wengi zaidi
 
Ongereni wana masasi mtwara si watu wa mwanza tunawatakia kila la kheri lakini kumbukeni ccm haiwezi kubadilisha maisha yenu mnatakiwa mjipiganie wenyewe sisi huku tumekwisha silimu kila kitu safi yaani mteremkoooo

Unamaanisha nini kulinganisha na watu wa Mwanza......kwa taarifa tu jiji la mwanza ndilo jiji pekee Tanzania ambalo CHADEMA wameshika halmashauri
 
Kiukweli uongozi wa cdm wilaya hapa Masasi wanafanya kazi nzuri sana ukilinganisha na uongozi uliopita. Kwa juma si chini ya mikutano mitatu ya hadhara inafanyika. Tuwatie moyo viongozi wetu japo ndo kwanza kazi inaanza, kwa hapa walipofikia si pa kubeza! Viongozi wabunifu wanaoijua kazi yao vizuri. Hakuna chama cha siasa Masasi kinachofanya shughuli za siasa kama CDM... wengi tu mashahidi! Mwamko ni mkubwa sana kwa wananchi hasa maeneo ya vijijini!
 
Je Mtwara Ipo katika ile Ramani ya chadema iliyochorwa na Joshua nasari na ndugu Jakaya akapigwa stop kutokanyaga katika ardhi ile ya ahadi?
 
Je Mtwara Ipo katika ile Ramani ya chadema iliyochorwa na Joshua nasari na ndugu Jakaya akapigwa stop kutokanyaga katika ardhi ile ya ahadi?

Hapana nadhani haipo......ila mbaya zaidi haipo kwenye ramani ya maendeleo ya serikali ya CCM......Bandari ya Tanzania inatakiwa kuwa Mtwara.....Reli ya Mtwara ikapotezewa....bei ya soda inakimbizana na bia....korosho haziwanufaishi kivile....viwanja vya michezo ni duni.....vyuo ni matawi tu.....n.k.
Bora wajiunge na M4C..
 
Back
Top Bottom