CHAMVIGA
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 7,687
- 2,238
Wingu zito.
Mtanzania aliyenaswa na M23
Jumatano, Julai 24, Na Ratifa Baranyikwa
*Waasi hao sasa wadai wako tayari kumwachia huru huku wakimtaja Nyerere kuwa fahari yao. WINGU bado linaendelea kutanda, kuhusu ukweli na uhalisia wa madai ya kundi la waasi la M23 la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, linalodaikumshikilia askari anayedaiwa kuwa na uraia wa Tanzania.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la MTANZANIA Jumatano kuhusu madai hayo ya M23, unaonyesha kuwapo na ukakasi na utata mkubwa kuhusu taarifa hizo ambazo zilianza kusambazwa katika mitandao ya intaneti kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hata hivyo, wakati maswali yakiongezeka kuhusu sakata hilo, waasi hao wa M23 ambao wamekuwa wakipambana kumng'oa kutoka madarakani, Rais Joseph Kabila bado wanaendelea kupata kigugumizi kueleza iwapo askari wanayemshikilia alikuwa miongoni mwa wanajeshi wa Tanzania wanaounda kikosi cha kulinda amani nchini Kongo au la.