M-Pesa sio salama

Mm nina miak 10 natumia mpesa sijawah kukosea kutuma pesa, najiuliza how mnakiseaga
 


Ndugu yangu.....kwanza nitangaze maslahi mimi sio staff wa Vodacom ingawa nilishawahi kufanya nao kazi mwaka 2011 - 2015 (five solid years)

Umekosea kutuma pesa (nasema hili ni kosa la kujitajia kwa sababu mitandao almost yote wameweka ile menu yao ioneshe namba ya simu na jina la unayemtumia ili uhakikishe kabla ya kuthibitisha muamala kwenda); bado unawalaumu mtandao?

Umeuliza Vodacom wanashindwaje kumtrack.......kama mteja ameshatoa pesa, wewe ndo unatakiwa uwe unapiga angalau mara kwa mara ili wao Vodacom wawe wanaingia kwenye account yake kuangalia kama ameweka pesa ndo wairudishe kwako, otherwise hawawezi kublock account ambayo haina pesa maana ndo kwanza utakuwa umem-alert yule mpokeaji asiwe anaweka pesa kabisa kwenye Mpesa yake, so njia bora wanaiacha bila kuiblock ili awe free kutumia account yake miamala iwe inapita ili siku akijisahau na akaweka pesa, na wewe ukipiga ikakutwa mle ndo inareversiwa. (Kumbuka hapa ni ww unatakiwa kuwa unapiga na sio wao customer care uwaachie jukumu la kuwa wanamfuatilia kila siku maana wale wanapokea tu calls na kureport cases kwenye idara zingine......unless otherwise kama unataka ifuatiliwe specifically ya kwako tu basi uende na taarifa ya polisi na ufike kitengo cha Fraud & Forensic Investigation hapo hapo Vodacom ndo waanze procedure za kumtrace huyo mpokeaji

Umesema uko sure kwamba Voda wanamjua wakala ambaye mpokeaji ametoa pesa kwake, why washindwe kumtambua "mwizi wako"......nadhani ww ni mteja wa muda mrefu wa Mpesa na ulishawahi kutoa pesa kwa wakala, hvi ww ukitoa pesa kwa wakala akakupatia fedha zako ukaondoka (ingawa watarecord taarifa za muamala wako), je huyu wakala akibanwa anawezaje kujua ww ni wa wapi na unapatikanaje sasa? assume umetoka Dar kwa bus na unaelekea Dodoma, ukashuka Msamvu pale ukatoa pesa kwa wakala na ukarudi kwenye bus na kuendelea na safari. je huyu wakala wa Msamvu atakujuaje hata kama Voda watambana vipi,.....yeye zaidi ya kuwapa tu namba yako ya simu (ambayo hata ww mtumaji tayari ulikuwa nayo) anawezaje kusaidia sasa kama sio kumlaumu bure?

Mwisho umedeclare kwa maandishi makubwa kabisa kuwa MPESA sio salama!. Je kwa muamala wako mmoja uliokosea (kwa kujitakia) ndio umepata mandate ya kisheria ya kuutangazia umma kwa Mpesa sio salama? Je huoni kwamba hapa unaweza kuwa sued hata mahakamani kwa kutoa maneno yenye kutishia biashara za watu kwa kuandika kwenye forum inayosomwa na umma kuwa biashara ya fulani sio salama?

Najua upo ktk panic hasa kwa kuzingatia huenda muamala uliokosea ni fedha nyingi, ila ukishatulia na kurejelea ulichoandika hapa utaona umekosea big time!

USHAURI WANGU;
Toa taarifa police utaandikiwa RB kisha nenda nayo pale Vodacom makao makuu utaelekezwa kitengo cha Fraud and Forensic Investigation watafanyia kazi case yako. Kama upo mkoa tofauti na Dar basi nenda Vodacom Shop iliyo karibu na ww ukiwa na RB yako, wahuduma wa hapo Vodacom Shop watachukua taarifa yako na kuscan RB yako na kuituma ktk kitengo nilichotaja hapo juu na suala lako litafanyiwa kazi vizuri (hata kumpata mwizi wako physically) manake hiki kitengo kinashirikiana na jeshi la Polisi ktk kufanya ufuatiliaji wa watu kama hao.

Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…