M-Pesa Hoi ? Au Ndio Basi Tenaaa!

M-Pesa Hoi ? Au Ndio Basi Tenaaa!

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
Wadau JF nimegundua kwamba M-PESA ni mfumo duni sana kufanyia malipo kwa ajili ya bill mbalimbali ambao umenitia hasara na kuniharibia bajeti na ratiba mara nyingi.
Awali ya yote mfumo huu uko slow sana, hasa unaponunua umeme. Ukisha lipa bill tokens huja kati ya dakika 5 hadi siku kadha baadaye..

Zaidi ya mara 3 nimeambiwa fedha haitoshi siku ya pili ambayo ni mwezi mpya wakati umeme nimelipia labda masaa 10 kabla ya siku mpya kuanza.

Udhaifu mwingine, M-pesa hawarudishi fedha zako baada ya kuona muamala haujakamilika kwamba kiasi cha fedha kilicholipwa hakitoshi.

Tofauti na mifumo mingine kama Tigo-pesa, tigo wanakuletea tokens ndani ya sekunde 1 hadi 10 toka ulipie bill hususan, unaponunua umeme.

Tigo-pesa wanakurudishia kiasi cha fedha ulicholipa ndani ya kati ya sekunde 1 hadi 30 iwapo muamala haujakamilika kwamba kiasi ulichotoa hakitoshi.

Kutokana na mazonge ya m-pesa nimejikuta nikiharibu au nikipoteza muda na fedha. Mara kadha, napenda kununua umeme mwingi siku moja kabla au siku ya mwisho wa mwezi ili nipate unit nyingi za umeme kwa lengo la kujipanga kutafuta fedha za kutosha kununua umeme na kulipia (escrow account) yaani service charge ya kila mwezi. Kutokana na uhoi na ubovu wa huduma za M-Pesa nimejikuta nalala giza mara kadha.
 

Mwl. RCT umeniacha soremba kule kwenye jukwaa Tecn, kuhusu lile swala langu la keybord, nimejaribu kupress Ctrl,fn + shift but sikufanikiwa lakini nimejaribu Output USB nimefanikiwa sasa bado inanipa shida sana maana haiwezekani kutembea na laptop na keybord, msaada tafadhari.
 
Mwl. RCT umeniacha soremba kule kwenye jukwaa Tecn, kuhusu lile swala langu la keybord, nimejaribu kupress Ctrl,fn + shift but sikufanikiwa lakini nimejaribu Output USB nimefanikiwa sasa bado inanipa shida sana maana haiwezekani kutembea na laptop na keybord, msaada tafadhari.
  • Nipe model ya PC yako; Mfano dell inspiron 15 3542
  • Pia kama itawezekana Piga picha hiyo sehemu ya keypad kisha attac hapa.
  • Karibu
 
Back
Top Bottom