M/kiti CCM ajiuzulu, kisa - kuhudhuria sherehe Chadema! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

M/kiti CCM ajiuzulu, kisa - kuhudhuria sherehe Chadema!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Nov 29, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Makanyagio wilayani Mpanda mkoani Katavi, Chifu Mlela Mallac, amejiuzulu nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kwamba amekuwa akizongwa mara kwa mara na wanachama na baadhi ya viongozi wa chama hicho akituhumiwa kukisaliti.

  Mallac anatuhumiwa kuhudhuria sherehe ya kumpongeza mama yake kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani hapa mapema mwezi huu.

  Mwenyekiti huyo anatoka kwenye familia ya wanasiasa kwani baba yake, John Mallac ni Mwanyekiti wa Chadema Mkoa wa Katavi, wakati mama yake, Anna Mallac ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema.

  Mwanasiasa huyo pamoja na kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Makanyagio na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mpanda, lakini pia ni Chifu wa eneo la Mpembe lililopo Tarafa ya Mwese ambako alitawazwa kijadi kuwa mtemi wa eneo hilo mwaka jana.

  Katika mazungumzo yake ya simu na kisha akiwa dukani kwake maeneo ya barabara mbili mjini hapa, Mallac alikiri kujiuzulu nafasi hiyo, akisema kuwa kama mtemi ni mtu wa watu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, na pia kama mtoto alikuwa na haki ya kuhudhuria sherehe ya kumpongeza mama yake baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoani hapa mapema mwezi huu.

  Lakini alisema sababu kubwa iliyomfanya ajiuzulu nafasi hiyo ya kisiasa, ni kutokana na maadili mabaya kutoka kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kutoka ngazi ya Kata hadi Wilaya ambapo anawatuhumu kuwa hawana siri wala uwajibikaji unaotakiwa.

  Akifafanua, alisema hali hiyo ilijitokeza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Mbunge wa Mpanda Mjini ambapo baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM wilayani, alidai walikisaliti chama tawala kwa kumuunga mkono mgombea wa jimbo hilo kupitia Chadema.

  Katika uchaguzi huo, Said Arfi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa alishinda tena kiti hicho kwa miaka mitano ijayo; huku CCM wakishutumiana wenyewe kwa wenyewe wakimtafuta mchawi.

  "Viongozi na baadhi ya wanachama wa CCM wamegawanyika baada ya kushindwa kulirejesha jimbo hali iliyojenga chuki miongoni mwetu kusema kweli.

  Baadhi ya viongozi na wanaCCM wenyewe wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa nafasi ya ubunge tulidhani tuko pamoja kumbe baadhi ya viongozi wenzetu walikuwa wanafiki...Walitusaliti kwa kumuunga mkono mgombea wa Chadema," alidai Mallac.

  Katika barua yake kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Jacob Nkomola, Mallac alisema anajiuzulu ili kutoharibu jina na sifa yake kwa jamii inayomwamini na kumfanya awe Chifu wao.

  Chanzo: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=12101
   
 2. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Na Bado watajiuzulu wote Bora ya wewe uliamua kujiuzulu......''mshike mshike ndege tunduni mwenzenu mjanja amekimbia"

  Tutasikia mengi hasa pale mlipokubaliana mambo furahi na kutosana! hao ndio chichemi!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ccm pumba kweli. Sasa wanataka kumtenganisha na mzazi wake?
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Siasa za visasi na husuda ndo msingi wa CCM ya sasa
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Nov 30, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Chifu ukawahi kadi ya CHADEMA! Teh teh teh teh!
   
Loading...