Lyatonga: Wabunge wa CCM wachawi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lyatonga: Wabunge wa CCM wachawi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Apr 20, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Jana akifunga Mjadala wa hoja ya Kamati yake Bungeni, Muheshimiwa Ryatonga Mrema huku akizungumza point kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kwa namna ya kipekee kabisa akionyesha namna Serikali hii ilivyoshindwa kutekeleza majukumu yake hata yale madogo kabisa ya kukagua Bati lililo juu ya nyumba ambayo watawala hawa wamo humo humo alifikia hatua ya kusema Kwamba Mawaziri wa CCM wanafanya kazi kama wachawi.

  Akamshona Waziri Mkuchika kwamba, anaficha taarifa za serikali kwapani, hataki kushare na watu ili wazijue na kuweza kumsaidia, na kiukweli, hata Jana Waziri Mkuchika alionyesha tabia za Kichawi, pale ambapo alisema analist ya viongozi wa halmashauri ambao wengine wamefukuzwa kazi, wengine wanakesi mahakamani na wengine wako Jera, kuna Mbunge mmoja akamueleza aisome, Mkuchika kwa tabia za kichawi kweli kweli akaficha, akaishia kuonyesha vijikaratasi vya summary zake kwamba majina yamo humu.

  Wapili kuonyesha tabia za kichawi akawa Lukuvi, nae akasema report za mambo yote yaliyoahinishwa na CAG katika report yake ya mwaka 2009 (kama sikosei) zipo tayari na kama wabunge wangezipata wasingekuwa na maswali mengi namna ile, naye akaiinua report hiyo akisema hii hapa, Mkuu wa wachawi (according to Mrema) Mkuchika akawa anatikisa kichwa kuonyesha anakubaliana na Mchawi mwenzake Lukuvi.

  Huwa sina muda wa kuangalia Bunge, lakini kwa nilichokiona na kukisikia jana, ni wazi kabisa tunaongozwa na watu ambao thinking capacity na thinking quality zao ni za viwango vya watoto wa shule za msingi, sababu huko ndio kuna watu (nao ni kwa sababu ya utoto wao) ambao kuwafichia wenzao madaftari, au vitabu au kuficha wanasoma tuition kwa mwalimu gani mzuri ni jambo la kawaida kabisa. sasa hawa sijui wanaficha ili iweje wanapata faraja gani kuficha au ili waonekane wao wenyewe ndio wanafacts.
   
 2. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Jambo hili la kuficha nyaraka muhimu na kushindwa kuzitoa kwenye kamati husika halikuwa bahati mbaya bali lilitayarishwa liwe hivyo mahususi kwa kutegemea kuwa watakuwa wanapunguza maswali Bungeni kwa yatokanayo na majibu yale waliyoweka kwapani,

  Walijua 100% kuwa hata bungeni wasingesoma kile walichotayarisha kutokana na muda waliopangiwa kikanuni hivyo technically wamefanikiwa kuahirisha kutatua tatizo with many braa braaa wakisahau kuwa Hansard inatunza kila kitu kwani akili zao ni kama za mbuni.
   
 3. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lyatonga ana pointi mara nyingine
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Mbaya zaidi wamesababisha Wabunge vichwa kama ZITTO kuescalate issue kufikia hatua ya sasa ya kutafuta sahihi sabini. Huwa nikifikia hapa ndio nazidi kuona kwa uwazi zaidi ni kwa namna Gani Mungu anaingilia mambo yetu. Nani alitegemea Bunge letu kufikia kwenye hatua ya kupiga kura ya kutokuwa na Imani na waziri mkuu, hasa sasa, ni ghafla sana, lakini haiwezekani kwamba Ulimwengu huu mzima hakuna aliyekuwa hajui.

  Hili liwe ni funzo kwa watu wote sio CCM tu, kwamba Hakuna Uovu unaoweza kudumu milele. Sasa Masikini Pinda, sijui ataficha wapi sura yake.
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Jana alitisha, ila nadhani afya yake haijatengemaa, sababu alionekana kama karukwa na akili namna fulani hivi, alipoambiwa muda wake umekwisha, sijui kama alikuwa anaelewa anaongea nini at that Moment.
   
Loading...