Lyatonga Mrema tukueleweje?

Lyatonga Mrema tukueleweje?

==> Wee nae msanii kweli...Mrema ni mtu wa kum quote or kumsikiliza...!!??

==> Wee ndio una matatizo.... mwacheni mzee wa watu atleast mapunye yemepona kidogo...kama sio JK huenda asinge kuwa hai...aache kumsifia .??
 
Mabeberu waliwatumia vibaraka kupenyeza maslahi yao kwenye nchi zetu wakati wa vuguvugu la ukombozi.

Haiyumkiniki CCM inatumia sytle ya mabeberu kupenyeza na kutumia vibaraka kudhoofisha upinzani ili nchi isipige hatua za maendeleo

Mkuu kwa swala la MREMA binafsi naona...........NJAA......ndo mpango mzima.......huyujamaa hana uhusiano hata kidogo na mabeberu..............alitambua tu kucheza karata zake pale mambo yalipomuendea mrama...........kumbuka hata Lugha ya Malkia ilikuwa inampiga saana chenga ( natambua wanaotumiwa na mabeberu sio lazima waongee Kingereza)........hakuwa exposed kihivyo....
 
==> Wee nae msanii kweli...Mrema ni mtu wa kum quote or kumsikiliza...!!??

==> Wee ndio una matatizo.... mwacheni mzee wa watu atleast mapunye yemepona kidogo...kama sio JK huenda asinge kuwa hai...aache kumsifia .??
Anatumia kanuni ya BANIANI MBAYA.... eeh?
 
Mwacheni tu huyu msee wa Kiraracha jamani. Kama si JK, asingaliipata Vunjo, mzee mzima na uso uliobabuka akaenda kuipigia magoti cc ya ccm kule Dodoma ili aachiwe jimbo la vunjo. Kwetu wanasema; Mwanaume kulia ni pale anapopiga magoti. Mrema akapiga magoti akiomba lile jimbo. JK akamwonea huruma akapewe na mgombea wa ccm akapewa ukuu wa wilaya kama kifuta machozi. Game droo. Unategemea athubutu kufyatua tena yale mabomu yake ya 1995? Hapana, hapana. Akae pale bungeni mpaka adondoke kwenye kiti kwa usingizi. Hao ndio Nape anasema, wanasubiri.....tu. Mama Makinda na Job wakafanya ubabe wao, wakampa na "Ka-uenyekiti" we, unataka anyee bakulini??? Basi mwacheni, siku hazigandi jamani. Ataondoka with a big shame.
 
Wazee kama hawa hawana la kufanya baada ya kutoka hapo hivyo hadi wafe ndio utaona mabadiliko ya chama, kwani hawao tayari kuwaachia vijana, wameshasahau ya kuwa nchi hii ilianza kuongozwa na wao wakiwa vijana lakini sasa wanawapiga vita vijana. Tusubiri wafe tu.
 
yaani muda nilioutumia kutumikia NCCR ya Mrema wakati huo sikujua kama hatakuja kuwa ny.o.ka kuwang'ata wapinzani. Au ndio maana Mungu kampa magamba usoni??
 
Mrema atakumbukwa wakati akiwa NCCR-MAGEUZI.
 
Unakumbuka kwenye kila kikao cha Mbatia na taasisi yake(CHADEMA walisusia),Kikwete alimwambia waziri wake amtengenezee mafao mazuri ya kustaafu Bw Lyatonga?

hivi mkuu hicho cheo cha naibu waziri mkuu kilikuwepo kikatiba? maana yuanzie hapo kabla ya kuangalia mambo mengine.
 
Ndugu wana JF huyu mzee na yule mzee wa mapesa na profesa uchwara Lipumba kweli wana njaa kupitiliza kipimo. Hivi watu wazima kama wale kwa maisha ya kinafiki kama yale wanajionaje katika jamii maana ni aibu kubwa sana kwa binadamu kuishi na kusaliti kitu ambacho unakiamini ili kupata kamkate ka kila siku. Huyu mzee na kina mbatia ni CCM na ndiyo wapinzani wakuu wa vyama vya upinzani ni vyema wananchi wakawatambua na kuwakataa ili wakalambe makombo huko CCM maana ni watu hatari katika jamii. Shame on these WANAFIKIs.

Hey apo katika kusema Profesa uchwara kama unakosea hivi coz Chadema hakuna mwenye anafika kiwango chake yule jamaa si unakumbuka juzi tu alitoka Majuu
 

Mkuu kwa swala la MREMA binafsi naona...........NJAA......ndo mpango mzima.......huyujamaa hana uhusiano hata kidogo na mabeberu..............alitambua tu kucheza karata zake pale mambo yalipomuendea mrama...........kumbuka hata Lugha ya Malkia ilikuwa inampiga saana chenga ( natambua wanaotumiwa na mabeberu sio lazima waongee Kingereza)........hakuwa exposed kihivyo....
Mkuu, nilitumia lugha ya mfano hapo. Ni kwamba Mrema anatumika kama walivyokuwa wanatumika vibaraka enzi zile...

Angelikuwa mwasisi mzuri wa siasa za vyama vingi kama angeliondoa tamaa ndani yake na kuwatumikia watanzania kwa moyo mweupe.

Mrema amedhoofu kisiasa na ataingia kwenye vitabu vya historia kama msaliti as others
 
Back
Top Bottom