Lwakatare kuendelea kusota rumande

Lwakatare kuendelea kusota rumande

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,573
Mtuhumiwa wa ugaidi ndugu lwakatare ataendelea kusota rumande baada ya dpp kutokubaliana na uamzi wa mahakama ya rufaa kumfutia baadhi ya mashitaka kinyume na sheria,dpp ametaka apate ufafanuzi toka kwa jaji kaduli ni kifungu gani cha sheria kilichomwachia lwakatare na ile hali ushahidi upo wazi kuwa lwakatare amehusika na hilo tukio la ugaid.sorce ofisi ya dpp na mahakama ya rufaa,haya jamani safari inaendelea.

=============

DPP amng'ang'ania Lwakatare
na Happiness Katabazi | Tanzania Daima | Mei 23, 2013


MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amewasilisha ombi katika Mahakama ya Rufaa nchini, akiomba itengue uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wa kumfutia mashitaka matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.

Dk. Feleshi aliwasilisha ombi hilo juzi kwa njia ya maandishi, ambapo katika maombi yake anaiomba mahakama hiyo iitishe mwenendo wa shauri lililotolewa uamuzi huo na Jaji wa Mahakama Kuu, Lawrence Kaduri Mei 8, mwaka huu na kuupitia upya na ifute uamuzi huo kwa kuwa una makosa kisheria.

Kwa mujibu wa hati ya madai, Dk. Feleshi anadai Mahakama Kuu haikuombwa kumfutia mashitaka Lwakatare kama Jaji Kaduri alivyotoa uamuzi huo, bali aliiomba mahakama iitishe majalada ya kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18 na 20 mwaka huu.

"Kwa kuwa Ofisi ya DPP ipo kwa ajili ya kusimamia utawala wa sheria, haijaridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliomfutia mashitaka matatu Lwakatare, hivyo tunaiomba mahakama hii iitishe mwenendo wa kesi ulioamuliwa, kwani tunaamini kisheria jaji alikosea kutoa uamuzi ule, kwani Lwakatare hakuwa ameomba afutiwe mashitaka yanayomkabili," alidai Dk. Feleshi.

Hata hivyo hadi jana mchana uongozi wa Mahakama ya Rufaa ulikuwa bado haujapanga majaji wa kusikiliza ombi hilo.
 
tupe undani wake zaidi kwa nini DPP hataki anahisi mahakama imekosea au anajenga hoja gani zaidi.
 
Yule ni gaidi akiachiwa arudi mtaani lazima ataendelea kuwalisha watu sumu tu
 
Nimeishangaa sana mahakama kuu kubadilisha yale mashtaka, ule ugaidi upo wazi kabisa na una ushahidi wa wazi usio na shaka ndani ake
 
DPP anahoji jaji kaduli kazingatia nini kufuta mashitaka ya lwakatare na ile hali ushahidi upo wazi, DPP ameenda mbali zaidi kwa kudai kwamba kunakitu baina ya jaji kaduli na CHADEMA haoni sababu za kumwachia mtuhumiwa kwa ushahidi ambao upo wazi.
 
Ngoja naye akae kidogo kama alivyokaa Ponda bahati nzuri wote wana maradhi ya kisukari.
 
Mtuhumiwa wa ugaidi ndugu lwakatare ataendelea kusota rumande baada ya dpp kutokubaliana na uamzi wa mahakama ya rufaa kumfutia baadhi ya mashitaka kinyume na sheria,dpp ametaka apate ufafanuzi toka kwa jaji kaduli ni kifungu gani cha sheria kilichomwachia lwakatare na ile hali ushahidi upo wazi kuwa lwakatare amehusika na hilo tukio la ugaid.sorce ofisi ya dpp na mahakama ya rufaa,haya jamani safari inaendelea.
toa upuuzi huu hapa tafadhali.kajipange na kama hujui mambo ya sheria kaa nayo mbali kama tembo wanavyokaa mbali na kinana.
 
toa upuuzi huu hapa tafadhali.kajipange na kama hujui mambo ya sheria kaa nayo mbali kama tembo wanavyokaa mbali na kinana.

tukana tu lakini ukweli utabaki daima sasa wewe unapomtukana mtu aliyepost bila wewe kuto hoja zako hatukuelewi,au wewe unataka nini.
 
Ndugu yangu nadhani huna uelewa wa kutosha kuhusu taratibu za mahakama, kwa kukusaidia tu ni kuwa mahakama itaendelea kufuata maamuzi ya mahakama kuu hadi hapo hiyo rufaa ya dpp itakaposikilizwa na kuamua vinginevyo maana ingekuwa taratibu ziko kama unavyosema Leme asingeingia bungeni hadi rufaa ya ccm isikilizwe au kafumu alipokata rufaa kupinga maamuzi ya mahakama kutengua ubumge wake angeendelea kuwa mbunge lakini kisheria haiko hivyo hivyo post yako haina mantiki
 
Hivi Mwigulu alienda nchi gani hivi karibuni kwa mafunzo?alienda kujifunza nini?
 
Last edited by a moderator:
DPP anahoji jaji kaduli kazingatia nini kufuta mashitaka ya Lwakatare na ile hali ushahidi upo wazi, DPP ameenda mbali zaidi kwa kudai kwamba kunakitu baina ya jaji kaduli na CHADEMA haoni sababu za kumwachia mtuhumiwa kwa ushahidi ambao upo wazi.
 
Kwa kweli jaji aliingia choo cha kike maana haiwezekani watu hawajatoa ushahidi waote na kuonyesha kweli ni ugaidi yeye anafuta kesi....mambo yangekuwa lahisi namna hii gerezani kungekuwa hakuna watu na wala kungekuwa hakuna haja ya kusikiliza kesi maana majaji wanaweza hukumu bila kusikiliza ushahidi
 
DPP ----- tu hana anachokijua, kazi yenyewe kapewa kishkaji, hivi na hawa magamba wanavyoihusisha chadema n la tuhuma ya Lwakatale wanamaanisha nini? au kukamatwa KInana na pembe za ndovu katumwa na ccm? au Mwigulu kufumaniwa na mke wa mtu kule Igunga ni sera ya ccm, ama kweli viongozi wote wa ccm wanafikiri kwa kutumia makalio.
 
Back
Top Bottom