Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
 
Mkuu si useme zaidi, au unakimbizwa? Hii habari ni nyeti sana, si ya kuileta kiharaka hivyo. Tuambie amefutiwa halafu kimekuwa nini? Hana kesi ya kujibu? Au imekuwaje sasa? Yupo huru?
 
Lwakatare amefutiwa mashitaka yote ya ugaiidi na judge wa mahakama kuu.
Amebakiwa na shitaka moja tu linalohusu madai.
 
Mkuu si useme zaidi, au unakimbizwa? Hii habari ni nyeti sana, si ya kuileta kiharaka hivyo. Tuambie amefutiwa halafu kimekuwa nini? Hana kesi ya kujibu? Au imekuwaje sasa? Yupo huru?

kafutiwa mashtaka mawili moja la ugaidi, kwa maama hiyo nadhani kesi itaendelea kisutu.
 
Mkuuu hebu weka nyama zaidi madai ya nini mkuu na hilo lililobaki lina dhamana
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo lina dhamana.

Asante kwa taarifa mkuu........Hoja hii inaungwa mkono?.......Ndiyooooooooooooooooo
 
adi nitakapoona katika TV akitoka mahakamani na akiwa nje kwa dhamana

yani CCM haweshi vituko kwa kupandikiza kesi za kishenzi,tunangojea kiroja cha Arusha sasa!!
 
Funguka mkuu,usitubanie uhondo huo..aibu yao magamba.
 
mahakama kuu ya tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chadema wilfed lwakatare.

Taarifa kutoka mahakama kuu zinasema mahakama kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo lina dhamana.


amen! Na iwe hivyo.....what a joyfull day!!
 
Tutampa Ukaribisho wa kishujaa hapa Kagera. Kwa kuwa kesi imepangwa Jumatatu basi akiletwa tu kesi inasomwa na dhamana anapewa fasta.
 
Back
Top Bottom