Luthuli ni jina la Mtaa wa Ikulu

Luthuli ni jina la Mtaa wa Ikulu

Joined
Jan 10, 2012
Posts
63
Reaction score
26
Jina la mtaa wa ikulu zamani lilikuwa ni Luthuli (mtaa wa kwenye geti la kuingilia) ingawa kwa sasa ni Barack Obama (ocean road) kama inavyoonekana kwenye anuani ya ikulu, hii ndio historia ya Luthuli:

Inkosi Albert John Lutuli (commonly
spelled Luthuli ;[a] c. 1898 – 21 July
1967), also known by his Zulu name
Mvumbi , was a South African teacher
and politician .
Luthuli was elected
president of the African National
Congress (ANC), at the time an umbrella
organisation that led opposition to the
white minority government in South
Africa.

He was awarded the 1960 Nobel
Peace Prize for his role in the non-
violent struggle against apartheid .

He was the first African, and the first person from outside Europe and the Americas,to be awarded the Nobel Peace Prize.
 
2005_protea_albert_luthuli_1-10oz_reverse.jpg
 
Watawala wa nchi hii wameona ni bora wamtukuze mmarekani obama kuliko kuendelea kumuenzi mwafrika mwenyetu lituli!SHAME!
 
Kwa nini sisi hatuwaenzi watanzania wenzetu! Kwa nini barack obama isingeitwa mkwawa? Au jina la wapigania uhuru wa kwetu. Hii ni aibu kwa anuani ya taifa ina jina la mmarekani.
 
Jina la mtaa wa ikulu zamani lilikuwa ni Luthuli (mtaa wa kwenye geti la kuingilia) ingawa kwa sasa ni Barack Obama (ocean road) kama inavyoonekana kwenye anuani ya ikulu, hii ndio historia ya Luthuli:
haya tumeelewa lkn wengine hawatakuelewa maana umeQuote direct KIZUNGU tupe kiswahili chake km ulivyoanza.
Tupe na Historia ya Obama na Ocean Road mm nitajazia Toure Drive na Shekilango
 
Ni sababu ipi iliyofanya Ocean Rd ibadilishwe iitwe Obama Rd? Ni jambo gani kubwa alilofanya huyu jamaa ndani na nje ya Tanzania mpaka tumpe heshima barabara ya Ikulu iitwe kwa jina lake?
 
haya tumeelewa lkn wengine hawatakuelewa maana umeQuote direct KIZUNGU tupe kiswahili chake km ulivyoanza.
Tupe na Historia ya Obama na Ocean Road mm nitajazia Toure Drive na Shekilango

Tasfiri ni : Albert John Luthuli 1898-1967 alikuwa ni mwalimu na mwanasiasa wa Afrika ya kusini. Na alishika nyadhifa kadhaa ANC ikiwa ni pamoja ma mwenyekiti wa chama. Alikuwa ni mpinga ubaguzi wa rangi na alikuwa mwafrika wa kwanza mweusi kushinda nishani ya amani ya Nobel akiwa mtu wa kwanza nje ya bara europa na amerika kushinda hiyo nishani.
kwa heshima hiyo mwalimu nyerere akampa huo mtaa wa kwanza hapa nchini jina lake.
Barack obama alizawadiwa mtaa na kikwete baada ya kutembelea tanzania.....hakuna la maana alilofanya kwetu wala kwa afrika....bado weusi wanauliwa na kubaguliwa nchini mwake yeye akiwa Rais
 
Kama jina la Ocean Road limebadirishwa kuwa Barak Obama. Kwa nini Hospitali ya Ocean Road haijabadirishwa kuitwa Barak Obama Hospitali? Maana Ocean Road haipo tena.
 
Hilo jina halina miaka mingi litabadilishwa tu ngoja mkweeere atoke .
 
..kwa mtizamo wangu, Mwai Kibaki, na Barack Obama, hawakustahili kupewa majina ya barabara za Dsm.

cc idawa, Ukwaju
 
Last edited by a moderator:
Hilo ni jina Barack Obama road ni la muda huu ambapo majambazi wanaikalia ikulu yetu,akiingia rais makini anabatilisha upuuzi wote huo.Kwa kipi hasa alichofanya Obama kustahili heshima kubwa kama siyo mihemko tu ya viongozi wetu.Makosa yaleyale kuiita barabara inayopita mbele inayopita mbele makazi ya viongozi wetu wastaafu jina la Kibaki ambaye ni drug dealer.Sijui akili zetu tumeziweka wapi? kwa kweli.
 
Akija mwingine naye atabadili vilevile wala siyo tabu
 
Tutaliweka kwenye katiba nalo ili si kila punguani akitia timu ikulu basi anatoa zawadi za maeneo yetu kupewa tu majina ya kiongozi yoyote bila kuzingatia kama anastahiki au la. Hata hivyo tuna maeneo mengi ya pembezoni maeneo mengi yanayotakiwa kuendelezwa huko tuwapeleke wakafungue barabara zenye majina yao huko.Siyo kubadilisha majina ya barabara ambazo kumbukumbu ya heshima zilizotukuka ya viongozi wetu wa kiafrika,na kutunza heshima ya Mwl.Nyerere ni katika kipindi chake hizo barabara hizo zilipewa hayo majina.Sijui hili limekaaje kiitifaki kwa kweli.
 
jaman c mnajua tena vyandarua vinakotoka?? sasa ilibid tumbembeleze tupate vngne zaid vya kuzungushia wigo mboga mboga..!
 
Hata wakitaka Sokoine Drive waiite jina la Rais wa China sawa tuu.
 
Ni sababu ipi iliyofanya Ocean Rd ibadilishwe iitwe Obama Rd? Ni jambo gani kubwa alilofanya huyu jamaa ndani na nje ya Tanzania mpaka tumpe heshima barabara ya Ikulu iitwe kwa jina lake?
Akishapatikana anayejielewa hayo majina yatabadilishwa....! Achana naye huyo.
 
Back
Top Bottom