Tyta
JF-Expert Member
- May 21, 2011
- 12,767
- 10,539
Attachments
Last edited by a moderator:
Mbunge wa Mtera kwa tiketi ya CCM,Livingstone Lusinde aka Kibajaji ameivua nguo Serikali ya CCM. Akihutubia mbele ya Katibu Mkuu Kinana jimboni kwake Mtera,Lusinde amesema wananchi wamechoka kudanganywa. Amesema Serikali imezoea kuwadanganya wananchi juu ya mambo ya maendeleo huku Rais akiagiza michango ya lazima ya maabara.
Lusinde alitangaza na kuwataka wananchi wa Mtera kugomea agizo la Rais Kikwete juu ya michango ya maabara. "Ametamba alivyotaka mbele ya Kinana na Kinana hakumjibu wala kuweka mambo sawa. Amesema kuwa Serikali inadanganya watu. Hakika ameonesha jinsi CCM ilivyoshindwa kutekeleza Ilani yake" alisema shuhuda toka Mtera.
Katibu mkuu Kinana umebariki haya ya Lusinde?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hebu tusaidiane kidogo, hivi mbunge analeta maendeleo ama ni muwakilishi wa wananchi wa enoe husika bungeni? Nivuavyo mimi mbunge kazi yake ni kuisimamia na kuishauri serekali. Huwa ninapata shida unaposikia eti mbunge hajaleta maendeleo yoyote. Kazi ya kuleta maendeleo inaletwa na serekali kupitia kodi zet na mbunge kazi yake ni kuhamasisha tu au kuwakikilisha wananchi wake bungeni hasa kusemea matatizo yao.
Hivi kuna watu huwa wanamsikiliza Lusinde?