Lusinde aivua nguo Serikali mbele ya Kinana

Lusinde aivua nguo Serikali mbele ya Kinana

Kinana na Lusinde wote walewale tu,akili zao dakika tatu mbele
 
Kumbe nae gurudumu 3 anajua chama chake kuwa ni cha kinafiki kwa ahadi hewa....
 
Kibajaj hajafanya maendeleo yeyote ya maana kule Mtera na watu wengi wanaliwania jimbo lile hivyo ili kupata njia ya kutokea inabidi lawama zote za kushindwa kwake kuleta maendeleo azirushie kwa serikali ya mkwereeeee!!

Hebu tusaidiane kidogo, hivi mbunge analeta maendeleo ama ni muwakilishi wa wananchi wa enoe husika bungeni? Nivuavyo mimi mbunge kazi yake ni kuisimamia na kuishauri serekali. Huwa ninapata shida unaposikia eti mbunge hajaleta maendeleo yoyote. Kazi ya kuleta maendeleo inaletwa na serekali kupitia kodi zet na mbunge kazi yake ni kuhamasisha tu au kuwakikilisha wananchi wake bungeni hasa kusemea matatizo yao.
 
Livingstone Lusinde ni bomu ambalo linaweza kuripuka wakati wowote iwe kwa maslahi ya CCM na serikali yake au upinzani, hajawahi kuongea jambo lenye kuleta mantiki na kuimarisha chama chake. Kwa sababu chama hakijengwi kwa matusi muda pekee ndio utatuambia
 
Huyu Lusinde ni mnafiki mkubwa ameongea hayo maneno kwa sababu uchaguzi ni mwaka huu serikali inayoisema ndo hiyo ya chama chake ccm?
 
naomba video ya lusinde akiongea kwenye huo mkutano
 
wakati huu ni wa chama cha CCM kujitenga na Serikali yake - lawama zote ziende kwa watendaji wa Serikali ili chama kibakie salama kuelekea uchaguzi mkuu wa October. Mjini hapa...
 
Bora amefunguka macho kidogo .................. Ingawa kwetu usukumani hali ni mbaya, lakini kwa hawa akina MBUKWENI hali inasikitisha sana. Ni zaidi ya ufukara. Sidhani kama LeMutuz huwa analala kule unless huwa anaenda kwa CAMPING!!
 
Mbunge wa Mtera kwa tiketi ya CCM,Livingstone Lusinde aka Kibajaji ameivua nguo Serikali ya CCM. Akihutubia mbele ya Katibu Mkuu Kinana jimboni kwake Mtera,Lusinde amesema wananchi wamechoka kudanganywa. Amesema Serikali imezoea kuwadanganya wananchi juu ya mambo ya maendeleo huku Rais akiagiza michango ya lazima ya maabara.

Lusinde alitangaza na kuwataka wananchi wa Mtera kugomea agizo la Rais Kikwete juu ya michango ya maabara. "Ametamba alivyotaka mbele ya Kinana na Kinana hakumjibu wala kuweka mambo sawa. Amesema kuwa Serikali inadanganya watu. Hakika ameonesha jinsi CCM ilivyoshindwa kutekeleza Ilani yake" alisema shuhuda toka Mtera.

Katibu mkuu Kinana umebariki haya ya Lusinde?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

LUSINDE HIZO MBWEMBWE TU Ulikuwa wapi siku zote unangoja siku KINANA Anakuja ndipo unasema hayo mbona ulisema ktk sakata la ESCROW Serikali yako chini ya CCM Imefanya mengi pamoja na kuwabembeleza wananchi wajenge Maabara .
......Ulikuwa wapi muda wote wa ubunge,
.......Mwenzetu ,Ndugu yetu Lusinde,
.......kwaheri mwakani,Mtela byebye.

AGWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.CHIKULUMBA.
 
Wekeni picha ya lusinde. Wengine hatumfaham
 
Angesema hivi mpinzani angeambiwa ana chuki binafsi na Kikwete. Sasa huyu sijui watakuja na kauli ipi!? Au wataishia kujibaraguza tu kama hawajasikia lolote.

Mkuu huyo alikuwa anatia msisitizo kauli za Kinana kuwa kuna mawaziri mzigo. Kama mawaziri wanaweza kuwepo mizigo basi wapo maRC, DC na wakurugenzi ambao nao ni mizigo. Maana halisi ni kuwa serikali yote imejaa mizigo. Ila nanihii afanye Kuku akifanya bata kananihii. Subiri kama anamuiga Kinana ataipata yeye ni bata tuu ndani ya ccm
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Rais aliyeahidi, Kinana anayeiagiza serikali na Lusinde anayelalamika wote hao wako CCM. Ni juu ya wananchi kugundua kwamba hao watatu wanawafanyia mchezo wa akili
 
Tatizo sio kuwa mwana CCM bali kubebewa akili. Nakukubali mh. Lusinde unajitambua, HONGERA SANAAAAAAAAA
 
CCM ina Democracy. Sio chadema. Mtu wnauhuru wa kuongea lile analoamini.

Kwani as for you, Lusinde amesema uongo? Huo ni ujumbe kwa serikali, hii ya CCM au yoyote ile itakayokuwapo kwenye System kwamba, nivyema kujitahidi kutekeleza ahadi.

Kibajaji angekuwa CDM, tayar kwa kauli hiyo "angeingizwa killing chamber".

Hongera Kibajaji kwa kutoa ya moyoni.

cc: VUTA-NKUVUTE
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom