Lusinde aishangaa serikali ya CCM asema kama wameshindwa kuhudumia shule wazigeuze Hotel

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mbunge wa Mtera bwana Livingstone Lusinde ameishangaa serikali ya chama cha mapinduzi kwa namna ilivyotelekeza shule za primary na sekondari katika jimbo lake na ameshauri kama wameshindwa ni bora watangaze shule hizo zigeuzwe hotel.

Amesema hayo alipokuwa kwenye kikao na baraza la madiwani wa jimbo lake.

Concern

Naona sasa CCM wameanza kubanwa na mfumo wa uendeshaji wa nchi na wakiwa bungeni huwa wanadhani kuwa ni wapinzani tu ndio wanaumizwa na kusahau ugumu wa maisha na miundombinu inatutafuna wote wapinzani na wasio wapinzani.
 
Lusinde!!anawezakuwa na maana nyingine,,haishi maskhara huyo mwehu,usishangae akiituhumu cdm kwa kufanya ccm iwe ilivyo.
 
Mzee wa kibajajii....so wazigeuze hotel ili akajisevie menyu...so clever
 
Shule ziwe Hoteli?!! Mbunge kama huyo ukimpa wizara ya ellimu itakuwaje. Hapo wala huitaji kumfanyia vipimo kuijua akili yake.
 
lusinde,mulugo,muhongo,nchimbi na nchemba kwetu sisi ni wale wanaotangulia kushuka kaburini kupokea mwili wa maruhum.
 
Mbunge wa Mtera bwana Livingstone Lusinde ameishangaa serikali ya chama cha mapinduzi kwa namna ilivyotelekeza shule za primary na sekondari katika jimbo lake na ameshauri kama wameshindwa ni bora watangaze shule hizo zigeuzwe hotel.

Amesema hayo alipokuwa kwenye kikao na baraza la madiwani wa jimbo lake.

Concern

Naona sasa CCM wameanza kubanwa na mfumo wa uendeshaji wa nchi na wakiwa bungeni huwa wanadhani kuwa ni wapinzani tu ndio wanaumizwa na kusahau ugumu wa maisha na miundombinu inatutafuna wote wapinzani na wasio wapinzani.

...hoteli!?...nani ataenda kwenye hayo magofu kupata msosi...labda wageuze kuwa kilabu za pombe za kienyeji...
 
Huyu jamaa huwa hashirikishi mdomo na ubongo katika kuongea.
Sasa embu fikiri kuchoka kwa shule na kuzigeuza kuwa hotel kuna uhusiano gani?
 
Mbunge wa Mtera bwana Livingstone Lusinde ameishangaa serikali ya chama cha mapinduzi kwa namna ilivyotelekeza shule za primary na sekondari katika jimbo lake na ameshauri kama wameshindwa ni bora watangaze shule hizo zigeuzwe hotel.

Amesema hayo alipokuwa kwenye kikao na baraza la madiwani wa jimbo lake.

Concern

Naona sasa CCM wameanza kubanwa na mfumo wa uendeshaji wa nchi na wakiwa bungeni huwa wanadhani kuwa ni wapinzani tu ndio wanaumizwa na kusahau ugumu wa maisha na miundombinu inatutafuna wote wapinzani na wasio wapinzani.

Mimi ninamsoma. Ni kweli ukiangalia hakuna nia ya dhati ya kuboresha kiwango cha elimu nchini. Kuanzia raisi mwenyewe hana upeo wa kuelewa umuhimu wa elimu sahihi kwa maendeleo na mustakabari wa taifa. elimu leo inapimwa kwa idadi ya shule na si qualities za shule. Mfumo wa elimu unabadilishwa ili wanafunzi wengi wafaulu bila kuangalia wanachokifaulu ni kitu na chenye kiwango sahihi kwa mahitaji ya Taifa na Kimataifa katika dunia ya utandawazi. Tumeshuhudia mara nyingi walimu wa vodafasta na wengine wanafunzi wamemaliza A level wanakwenda kufundisha bila kuangalia uwezo, uelewa na ukomavu wa walimu hawa katika kuelimisha. Kumbumka Education siyo kujua 2 = 2+0. Inamambo mengi yanayohusiana na physical and mental capacity, development and growth ya huyo anayesomeshwa. Mwalimu awe na uwezo wa kujenga na kuinterpret concepts mbali mbali zilizo ndani ya context ya msomeshwaji na viwango vya kimataifa na mahitaji ya taifa.

Tumeona mitihani inakuwa multiple choice tu ili watoto wafaulu!. Wafaulu kufanya nini na kwa maslahi gani ya nani?.

Raisi mwenyewe kwa kuwa anatoka katika utamaduni usiothamini elimu, naye amehawilishwa hivyo hivyo na anafanya bora liende. Tumeshuhudia akituteulia waziri wa elimu asiyeweza hata kusoma!. Hivi ni nini hii?

Kwa ujinga huu, tunajikuta tunakizazi cha wasomi waliochini ya kiwango disaini ya kina Mulugo Mulugo tu sasa hao ndio watakaopewa dhamana ya kuratibu na kusimamia sera na mipango ya maendeleo ya Taifa. TUMEISHA!.

Ni naungana na Bwana Lusinde kwa kusema ni afadhali kutokuwa na shule kabisa tujue moja kulilko huu unafiki wa kijinga unaofanywa na Serikali wa kuanzisha vituo vya kukulia watoto halafu vibatizwe jina la shule. Shule ni mahali pa elimu. Sasa kama watoto wanakusanywa kwa miaka ys shule ili wasiwe wazururaji mitaani, hatuwezi kuita ni shule. Waachwe wakae na wazazi wao nyumbani wapate elimu ya asili kwa wazazi wao badala ya kuwapotezea muda katika shule ambazo hazipo. Kwa kweli serikail ya ccm na kikwete ni janga kuu kwa taifa letu.
 
Asijifanye kushangaa, hapo chama chetu kilikuwa kinatekeleza zile sera alizotuelezea mwenyewe akiwa kule Arumeru.
 
Unakumbuka shuka asubuhi? Wabunge wenye maono na wenue nia ya dhati ya kuwakomboa Watanzania kwenye hili giza la ujinga wakiongea bungeni udhaifu wa Serikali ya Ccm wewe na mwenzako Mwigulu mnatoka na mipasho.sasa jiandae kurudi kwenda kuuza utumbo wa mbuzi
 
Mtambo wa matusi,made in mtera,manufactured date:30/10/2010 expire date: 01/10/2015. Ccm vilaza industry
 
huyu jamaa ni kilaza, hayo ni mambo ya kusema bungeni na kwenye vikao vikubwa vya chama.
Anawaambia madiwani wafanyeje?
Wao ndo wanatunga sera ya elimu au ndo wanapanga bajet ya wizara?
 
Back
Top Bottom