Lunar Eclipse: June 15, 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lunar Eclipse: June 15, 2011

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JoJiPoJi, Jun 14, 2011.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  Mwezi.jpg

  Wakazi wa Uingereza kesho Jumatano watapata fursa ya kuona kupatwa kwa mwezi ambapo mwezi unatarajiwa kugeuka "mwekundu kama damu" kwa takriban dakika 100. Hata hivyo, wanasayansi wa taasisi ya mambo ya anga ya Marekani (NASA) wanaeleza kuwa wakazi wa Ulaya hawatofaidi vizuri tukio hilo kwani linatarajiwa kutokea kabla ya mwezi kuchomoza (kwa majira ya Ulaya)

  Tukio hilo linatarajiwa kuanza saa 12 na dakika 24 jioni kwa muda wa majira ya joto hapa Uingereza (1824 British Summer Time) na kuendelea hadi saa 6 usiku (0000 BST) lakini kwa Uingereza litaanza kuonekana saa 3 na dakika 19 usiku (2119 BST).

  Wakazi wa maeneo ya nusu ya mashariki ya bara la Afrika, eneo la Mashariki ya Kati, Asia ya Kati na magharibi mwa Australia wataweza kuliona tukio zima (yaani dakika hizo takriban 100 za kupatwa kwa mwezi). Hata hivyo, wakazi wa Marekani hawatoliona tukio hilo kwa vile litatokea majira ya mchana kwa mida ya huko.

  Kijiografia, asili ya mwanga wa mwezi ni mionzi ya jua. Tukio la kupatwa kwa mwezi ni pale Dunia, Jua na Mwezi zinapokuwa mstari mmoja, na kivuli cha Dunia kinaangukia kwenye Mwezi kamili. Uwekundu kama damu katika tukio hilo la kesho ni matokeo ya miale ya jua kupita Duniani kisha kuangukia kwenye uso wa mwez
  i.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  yule babu wa mwisho wa dunia ashapata point nyingine ya kuwakamata watu hapa
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Na lazima atajionasibu na tukio hili.
   
 4. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  thank kwa info...
   
 5. s

  samalanga Senior Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  babu wa mwisho wa dunia atawadanganya wasio soma vitabu vya mwenyezi Mungu,mfano Bibilia inatuambia hata Yesu hajui ,Babu anatoa wapi hayo kuweni makini Uganda mchungaji alichoma waumini wake kwanini asijichome yeye kwanza????
   
 6. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  afrika mashariki itakuwa saa ngap?
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhhhhhhh
   
 8. D

  Danniair JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kesho tarehe 15/6/2011 mwezi utapatwa katika nyota Mshale katika nyuzi 24[SUP]o[/SUP]23[SUP]'[/SUP]. Sakata hili litaanza hapa kwetu saa 2:24:34 usiku na kuisha saa 8:00:45 usiku wa manane. Ifikapo saa 4:22:30 mwezi utaanza kugeuka rangi kuwa mwekundu na ifikapo saa 5:12:37 usiku basi kuna mawili au utakuwa hauonekani kabisa (ukizingatia volcano iliyolipuka hivi karibuni na kutupa vumbi jingi sana angani), ama utageuka na kuwa kama damu iliyoganda. Ukiangalia tutakuwa na masaa 3:30 ya mwezi mwekundu na jumla ya masaa 7 ya tendo zima la kupatwa.

  Tutegemee nini basi, kwa wale waliozaliwa kati ya tarehe 13 juni hadi 20, na desemba 13 hadi 20 wakae chonjo kwani wana miaka saba ya machungu. Pia kwa wale wenye sayari ktk nyuzi hizi 20-28 Mapacha na Mshale (ikiwemo nchi yetu). Kubwa zaidi kutakuwa na ugunduzi mkubwa wa habari za uongo ambazo zilikuwa zikijulika kama za kweli, hii inaweza kuleta mtafaruku. Kwa kuwa Mars ndiye atakuwa bwana wa kupatwa huku ambako nako kunatokea ktk nyota ya moto - mshale, machafuko, vifo vya jumla, mioto, vitegemewe sana. Uzuri mmoja ni kuwa Mars akiwa ndiye bwana wa kupatwa ataonyesha na njia ya kutokea pia ktk matatizo hayo.

  Usiku wa kupatwa tunashauriwa kufanya haya; kuoga wakati wa kupatwa, kusali (andika sara yako kwenye karatasi safi kisha ichome moto, hapa nini maanisha unacho taka kitendeke ktk maisha yako, na usichotaka kitende kiandikwe kwa AMRI ya neno naachilia jambo hili na hili. mf. naachilia tabia yangu ya ulevi iende ilikotoka isirudi kwangu tena). Kula kabla ya saa 2:24:34.

  Katika usiku huu unashauriwa usifanye haya: tendo la ndoa, usigombane, usiseme uongo, usile.

  Mambo ni mengi sana kwa leo nakomea hapa.

  Najua majumbani magomvi sasa yameisha anza, lakini chukulieni magonvi hayo kama chachu ya kusonga mbele. Na magomvi haya hasa ni kuhusu watoto, majirani, elimu, n.k. Kwa wale walioharibikiwa na magari simu, computer msihofu ndo nyota ya mapacha inavyoliwa ambayo iko mkabara na Mshale.

  Siku njema.
   
 9. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa ulirithishwa mkoba na yule mlinzi wa watu? maana naona uliyoyaongea hayapishani sana na yule aliyetangulia!
   
 10. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  scientific proof...
   
 11. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Sayansi au ulozi na ramli?
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kaombe kurasa ktk gazeti la Nipashe sehemu ya nyota ukabe ile chanzi ya yule mnajimu feki aliyeshindwa kujua siku yake mpk mauti ilipomkuta.
   
 13. womanizer

  womanizer Senior Member

  #13
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unafaa sana kuwa mlinzi mpya wa mkulu
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  mtabiri, nimeona nyota ya Tanzania ni mapacha na mshale, nimefurahi kwasababu mapacha mbowe na Slaa wameupiga mshale CCM na sisiemu inakufa kibudu.
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  sosi???
   
 16. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  mh! Haya makubwa haya
   
 17. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mlinzi mpya wa Ikulu kapatikana! Hii habari inanifanya nijisikie vibaya. Watumishi wa Shetani tu hawa wote
   
 18. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,745
  Trophy Points: 280
  mmmmm ABARI HIZI BILA SHAKA ZINATOKA MWEMBECHAI .
   
 19. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,292
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ahsante sheikh yahaya mtoto kwa utabiri wako.
   
 20. D

  Danniair JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi si mtabiri hata sikurithishwa mkoba, ila mnamo Julai 16, 2000 kupatwa kwa mwezi ktk Mbuzi 24[SUP]o[/SUP]19[SUP]'[/SUP] kuliniharibia future yangu yote hata sasa ndo naanza kusimama. Nilinyooshewa vidole na kila aliyeniona.

  Nilipoteza kazi na elimu yangu ya digrii pia. Sikuweza kusaidika, si kanisani si kwa akina sangoma. Nilijiuliza sana sana hata nikaanza kufuatia kifungu kimoja kimoja cha biblia kadri nilivyovuviwa.

  Naikumbuka sana Waamuzi Ya 5:20, Yer 33:20, Zab 19:1-3, Zab 81:1-4, Yoel 3 Mathayo 26 n.k ndipo nilijikita kuangalia kuna nini ktk anga kumbe kuna vitu vingi kama isemavyo Zab 19 (planetary aspects), kwa hiyo niligundua kuwa kumbe past yangu ilikuwa inekunjwa kama karatasi, na nikajifunza jinsi ya kutumia mawe (gems) kuepukana na madhara ya aspects. Kutoka 28:15-30.

  Baada ya kuijua siri hii ndipo nikaanza kufanya "remedies" na sasa naanza kusimama dede, kabla nilikuwa nadanganywa tu na wanazuoni oh! funga na utoe sadaka nyingi mara kalete kuku, wapi na wapi , mbingu ilikuwa imepokea hukumu yangu tayari na kuniweka gizani (natural jugdement). Ezekiel 32:7-10 (nyota zako zitiwapo giza na Yahu nani atakuwashia mwanga?) Mat 6:22.

  Asanteni
   
Loading...