CCM ndo wanaisoma namba!
CCM ndo wanaisoma namba!
Wee nawe hata hujielewi Moshi imeingiaje hapa wivu mwingine bana aliyepewa kapewa tu wee endelea kushikilia vibuyu na ulozi ukiusubiri utajiri na mendeleo Moshi falsafa ya hapa kazi tu ilianzia toka enzi za mababu zetu angalia kihoro kisikuuwe karibu.
Watu wametishwa. Watu wametishika. Makada watakosa za watoto ada. Kujenga kutasimama. Miradi itapigwa radi na kuishia kuwa ahadi. Chama kina utawala wake. Chama kina Mwenyekiti wake. Si huyo Rais wa Tanzania. Kwanini majipu ya chamani nayo yapaniwe kutumbuliwa?
Tumepata taarifa, isiyo na ya kuvutia sifa,kuwa jamaa anataka kupewa nafasi ajinafasi kuyatumbua majipu ya chamani. Lakini, ameombwa asubiri wakati wake ufike. Makada wanakipenda chama kwa 'maslahi yanayoleta uhai'. Yakikaushwa ghafla,hapatatosha. Lakini, Ofisi Ndogo za CCM Lumumba hapakaliki. Hakuna raha ila karaha kusubiri pigo la ghafla.
Makada nchi nzima wanamuunga mkono Rais kutumbua majipu pengine lakini si chamani. Chamani kunafukuta kwa hofu ya 'bifu' kuporwa mnofu. Makada wanatumikia chama na wao wenyewe. Wanatamani wale waminywe na wao wasiguswe ili wasisuse. Hawataki sera ile ifike humu chamani.
Serikalini sawa, chamani si sawa. Double standards!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
mambo meku
Hamieni kule walikoenda wale wengine.
Awamu hii tutajua tu kutofautisha kati ya shuka na pazia.
Pelekeni ufataani wenu Ufipa, Lumumba yupo kiboko yenu Kinana.
Mtapaota sana.
CCM ndo wanaisoma namba!
Hahaaaaaa hii umehack kwa mafunzo ya Mkorea aliyekuja kugushi matokeo uchaguzi Mkuu? Ccm haipokei order toka Moshi,kila mteuzi ana madaraka yake ya kuongoza. Kama yapo majibu huko Ccm jitayarisheni kuyapokea yaje yatumbuke huko. Wameshaambiwa wanafiki waondoke. Kwa kasi hii ya Magufuli hata haitaji nguvu ya chama sisi wananchi tuko nyuma yake
waliompenda wanamchukia, waliomchukia wanampenda
Mkuu PC yangu siku hizi haionyeshi kitufe cha likeCCM ndo wanaisoma namba!