Lumbesa inatuongezea umasikini Mbeya

Lumbesa inatuongezea umasikini Mbeya

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
380
Reaction score
534
Sasa hivi Mbeya ni kama serikali iko likizo kwa jinsi wafanyabiashara wanavyopora wakulima mchana kweupe.

Ukiangalia Lumbesa ya gunia la viazi huwezi kubisha kwamba mkulima hapati chochote. Yaani heka moja ungeweza kupata gunia za viazi 70 kwa sababu ya Lumbesa utaambulia gunia 52!

Viongozi wa chama na serikali wapo, vizuizi vya ukaguzi mazao ya shambani vipo sijui wanafanya kazi gani?
Mnao husika amkeni saidieni wakulima wa viazi wafanyabiashara wanatajirika wakulima wanazidi kuwa masikini!
 
Kwenye ishu ya lumbesa mkulima haimpunguzii chochote kwa sababu bei hutokana na ujazo ,kwa iyo ukitoa lumbesa hautauza bei kubwa kama unavyouza kwa sasa
Ila lumbesa inam fever mfanyabiashara kwenye mambo mawili 1. Ushuru
2. Usafirishaji
Ila mkulima anapata abachostahili
 
Sasa hayo si ni mambo ya vyama vya wakulima kukaa na kuamua jambo moja na kulisimamia kwa pamoja mkuu.

Hilo kweli ni la serikali kuingilia??
 
Siyo mbeya tu Kiongozi, mkulima Tanzania anaumia sana hasa kwenye hv vipimo vya kukadiria ujazo!

Ifike mahala mazao yote ya mkulima ya uzwe kwa ujazo kipimo cha kilogram!!

Mfn: njegere inapimwa kwenye gunia lile la net nyekundu, ile net inatanuka balaaa inashindiliwa na wanaume haswa!
Mahali hata mkulima angepata gunia kawaida ndogo 20, anaambulia gunia 5 za net 🤔🤔
 
Sasa hivi Mbeya ni kama serikali iko likizo kwa jinsi wafanyabiashara wanavyopora wakulima mchana kweupe.

Ukiangalia Lumbesa ya gunia la viazi huwezi kubisha kwamba mkulima hapati chochote. Yaani heka moja ungeweza kupata gunia za viazi 70 kwa sababu ya Lumbesa utaambulia gunia 52!

Viongozi wa chama na serikali wapo, vizuizi vya ukaguzi mazao ya shambani vipo sijui wanafanya kazi gani?
Mnao husika amkeni saidieni wakulima wa viazi wafanyabiashara wanatajirika wakulima wanazidi kuwa masikini!
Sugu yupo mtumieni vyema
 
Hivi ni mbeya tu Kuna wakulima mkuu? Lumbesa ni kwa wakulima wote sema zinatofautiana
Mkuu Lumbesa ya Mbeya ni hatari. Yaani na robo ya gunia! Lakini inawezekana wenzetu wameridhika kwa sisi Mbeya hatutaki.
Wakulima wa Njombe ndiyo wanaendekeza lumbesa!
 
Back
Top Bottom