Lulu nimemisi uraiani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lulu nimemisi uraiani

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Aug 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  MCHEZA sinema wa Bongo aliye nyuma ya nondo katika Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaama kwa madai ya kuhusika na kifo cha Msanii Steven Kanumba, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa amepamisi sana uraiani.
  Akizungumza na mwandishi wetu Agosti 13, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako kesi yake inaendelea kutajwa, Lulu alisema amemisi vitu vingi vya uraiani, ikiwemo mitaa ya Sinza na Kinondoni alikozoea kwenda kujiachia, pia anawakumbuka sana mashosti wake akina Diana Kimaro ‘Pacha wa Lulu’.
  “Nimekumisi sasa… (anataja jina la mwandishi), pia nimewamisi watu wote huko uraiani, nimewamisi mashosti wangu jamani, nimemisi sehemu nilizokuwa napenda kutembelea,“ alisema Lulu.
  Lulu akionesha uso wa uchangamfu alisema anafurahi sana anapoona watu wanaofika mahakamani hapo ni baadhi ya marafiki zake na ndugu.
  “Ukikaa kule (gerezani) unawakumbuka watu wengi, sasa ukija hapa (mahakamani) unapowaona watu mbalimbali unaowafahamu kidogo unafarijika, unakuwa mwenye amani siku hiyo,” alisema Lulu.
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Kesi yake ni ya kuuwa bila kukusudia? ama ameshitakiwa kwa kosa gani?shida yake ndo huo ucelebrity,kila mtu anamjuwa.Otherwise wangeshamtoa kitambo wakware.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Anyone would baby gal! You will never know the value of freedom lest you loose it!
  jmushi1, alienda Kapteni Komba kumuona tu alivyosakamwa nahisi hana hamu! Its nice to be faceless!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  LULU.jpg ​[​IMG]  [​IMG]
  Maisha ya Lulu uraiani.
  [​IMG]
  Maisha anayoishi sasa.
  Na Mwandishi Wetu
  MAZINGIRA ndani ya Gereza la Segerea jijini Dar yamemlazisha msanii wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu' kubadili tabia bila ya kupenda, Amani linakuhabarisha.

  Lulu ambaye ni mshukiwa namba moja katika kifo cha msanii wa filamu nchini, Steven Kanumba, hivi sasa analazimika kuvaa nguo ndefu na kutinga hijabu tofauti na alivyokuwa uraiani.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo katika makabrasha yetu, msanii huyo kabla ya kukumbwa na tuhuma hizo, akiwa uraiani aliwahi kufanya mahojiano na waandishi wa Global Publishers na kudai kuwa hawezi kuvaa nguo ndefu kwa kuwa zinamuwasha mwilini.

  Hata hivyo, imebainika kuwa hayo yalikuwa ni maneno ya rejareja ya Lulu kwa lengo la kujitetea kwa mapaparazi.
  Haya yote yamekuja kufuatia msomaji mmoja kupiga simu ofisi za Global akihoji kuhusu habari ya staa huyo kudai nguo ndefu zinamuwasha.

  "Jamani mimi naitwa mama Diana, naishi huku Tabata. Kuna wakati mliandika madai ya Lulu kwamba anasema akivaa nguo ndefu anawashwa mwilini, siku hizi kila nikiangalia picha zake za mahakamani namwona amevaa nguo ndefu. Je, hawashwi?

  "Nauliza kwa sababu hivi karibuni mliandika Lulu apata gonjwa baya gerezani, nikafikiri lilitokana na kuwashwa," alisema msomaji huyo.
  Hata hivyo, alifahamishwa kuwa ugonjwa uliompata msanii huyo gerezani hautokani na kuvaa nguo ndefu.

  "Kwa sasa Lulu anatinga nguo ndefu za kila aina na wala halalamiki kuwashwa," paparazi wetu alimjibu mwanamke huyo.
  Kesi inayomkabili msanii huyo itaendelea tena katika Mahakama Kuu Juni 11, mwaka huu na anatarajiwa kutinga akiwa na nguo ndefu nyingine


   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280

  LULU.jpg ​[​IMG]

  • [​IMG]Lulu akiwa mahakamani.

  5.JPG ​[​IMG]


  ...Akiwa chini ya ulinzi mkali ndani ya mahakama.
  2.JPG ​[​IMG]

  Askari waliokuwa kwenye gari wakiwa tayari kumlinda msanii huyo.
  Maaskari...............jpg ​[​IMG]

  -
  Maaskari wakiwa na silaha zao tayari kwa lolote.
  Akishuhwa kwenye gari.JPG [​IMG]

  .Akishushwa kwenye gari.  Richard Bukos na Sifael Paul  IMEBAINIKA kuwa staa wa picha za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anawapa wakati mgumu askari magereza na polisi kufuatia ulinzi mzito wanaolazimika kumpatia wakati wa kumpeleka mahakamani na kumrejesha mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam, Amani linafunguka.
  Baada ya wiki kadhaa mambo kutulia na ulinzi kuwa wa kawaida tofauti na siku ya kwanza alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jumatatu wiki hii hali hiyo ilijirudia ambapo Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kifo cha Steven Kanumba alifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiwa na ulinzi wa kutisha.
  Amani lilimshuhudia Lulu akishushwa mahakamani hapo akiwa mtuhumiwa pekee kwenye basi huku akisindikizwa na askari magereza wanawake zaidi ya kumi.
  Mbali na askari magereza wanawake, kulikuwa na difenda la magereza lenye king’ora lililokuwa limejaa askari magereza wanaume na polisi wa kawaida.
  ULINZI MAHAKAMANI
  Mara baada ya ‘Kalulu Kadogo’ kufikishwa mahakamani hapo walipokezana na polisi wa mahakamani na katika kufumba na kufumbua, kila kona kulikuwa na askari waliokuwa wameimarisha ulinzi nje na ndani ya eneo hilo.
  Maafande hao walishuhudiwa wakiwa wamevaa majaketi yasiyopenya risasi (bullet proof), kofia za chuma huku wakiwa na ‘mabunduki’ aina ya SMG zilizokuwa zimejaa risasi na mikanda ya risasi za ziada.
  Wakati baadhi wakitanda ndani ya mahakama wakiwa wamemzunguka Lulu, wengine walizagaa nje huku wakizuia watu kukatizakatiza ovyo.
  WAOMBA MAMBO YAISHE
  Amani lilizungumza na baadhi ya askari hao wa kike ambao walionekana kutamani kesi hiyo iendeshwe haraka ili mambo yaishe kutokana na mshikemshike wanaokutana nao wakati wa kumpeleka Lulu mahakamani na kumrejesha gerezani.
  Kuna baadhi waliokwenda mbali wakidai wanatamani hata kuhama vituo vyao vya kazi kutokana na mikikimikiki wanayokutana nayo wanapotakiwa kumpeleka Lulu mahakamani.
  Ilidaiwa kuwa inapofika siku ya kumpeleka Lulu mahakamani, hulazimika kusitisha udhuru wowote kama kuwa wagonjwa hivyo kuzishangaza familia zao kwani wanapoulizwa kulikoni wanasema ni siku ya staa huyo na kila askari anakuwa ‘stendibai’.
  Kwa muda wa saa mbili mahakamani hapo huku mawakili wakibishana juu ya umri wa Lulu, ratiba zote zilisitishwa kwani shughuli ilikuwa ni hiyo tu.
  ‘AMA KWELI ANAWATESA ASKARI’
  “Ama kweli Lulu anawatesa hawa askari, kila mmoja yuko ‘bize’ na suala la ulinzi wake,” alisikika dada mmoja aliyefika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo.
  KESI YAPIGWA KALENDA
  Baada ya mawakili hao kushindwa kufikia muafaka wa umri kama ni miaka 17 au 18, kesi hiyo ilipigwa kalenda hadi Juni 11, mwaka huu ndipo utata wa umri wa Lulu utakapopatiwa ufumbuzi ili kuruhusu kesi hiyo ianze kusikilizwa.
  TUMEFIKAJE HAPA?
  Lulu ni mshukiwa wa kwanza katika kesi ya kifo cha aliyekuwa mpenzi wake na staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake maeneo ya Sinza Vatican City, Dar.


   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kiranga komo!

  Ngoma ikivuma sana mwishowe...
   
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Huwa napenda swaga zake za jela....angekuwa anavaa hivi yasingemkuta labda.
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi magereza na mahabusu zetu hazina nafasi za mke na mume au girl na boyfirend kuonana wakiwa wawili tu? Kama ipo basi Lulu asaidiwe jamani kupata hiyo basic need!!!!!
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Kwenda mahakamani anavaa rosary lakini kabla shingoni kaweka mashanga yasiyoeleweka!!
   
Loading...