Lulu azuiwa kuingia Ikulu

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,422
Imefichuka! Baada ya kuitwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kupongezwa kutokana na tuzo aliyopata nchini Nigeria, staa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alijikuta akihaha baada ya kuzuiwa kuingia Ikulu kutokana na kutokuwa na kitambulisho cha chama cha waigizaji.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Lulu alijikuta katika wakati mgumu kwani utaratibu wa wasanii kuingia Ikulu umebadilika, tofauti na serikali iliyopita kwani kwa sasa, wasanii wa filamu ni lazima wapitie kwenye Shirikisho la Filamu ‘TAFF’ kisha wizarani ndipo waruhusiwe kuonana na mhusika aliyemuita au anayetaka kumuona.

“Shughuli ilikuwa ifanyike Alhamis, Lulu alipofika wizarani akakutana na utaratibu huo mpya, si unajua yeye siyo mwanachama wa chama chochote cha filamu, ndiyo ikabidi aelezwe jambo hilo,” kilisema chanzo hicho.

Kutokana na utaratibu huo, Lulu akalazimika kurudi katika ofisi za mwenyekiti wa waigizaji mkoa wa Kinondoni (TDFAA), Ally Baucha ambapo alichukua fomu ya uanachama na kuijaza na kuirejesha siku hiyohiyo ya Alhamis iliyopita ili aweze kwenda kuonana na Waziri Mkuu siku iliyofuata (Ijumaa). “Yaani Lulu alihangaika kweli siku hiyo kwani hata siku ya kupokelewa pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hakuna msanii wa TAFF aliyekwenda kumpokea hata mmoja wala viongozi wake, hivyo hata alipopata mwaliko wa Ikulu ikashindikana kuingia bila ya utambulisho wa uanachama wa shirikisho na chama cha waigizaji mkoa anaoishi wa Kinondoni,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Mwenyekiti wa TDFAA, Ally Baucha ambapo alikiri kwamba ni kweli Lulu alikwenda kuchukua fomu harakaharaka na kuijaza na kuwa mwanachama ikiwa ni baada ya kupata mwaliko wa kwenda kupewa pongezi na Waziri Mkuu.

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba ni kweli kwa sasa hakuna msanii anayeruhusiwa kuingia Ikulu bila kupitia kwenye shirikisho na wizarani hata kama ameitwa na nani.
“Utaratibu umebadilika sasa, msanii hata kama ameitwa na kiongozi gani ni lazima afuate utaratibu huo ndivyo tulivyokubaliana, hivyo Lulu alishindwa kwenda moja kwa moja mpaka alipokwenda kujiunga kwanza na chama cha waigizaji na kutambulika na shirikisho ndipo nikawapeleka Ijumaa iliyopita na msanii mwenzake aliyeshinda tuzo pia, Single Mtambalike ‘Richie’ na kwenda kupongezwa kwa kutwaa tuzo hizo za kimataifa.

“Wasanii wanatakiwa kuufahamu utaratibu huo kwani hata wakipita moja kwa moja lazima watarudishwa tu kwenye shirikisho, wakati wao ukifika kama Lulu naamini watajiunga tu hatumlazimishi mtu,”alisema Mwakifwamba.

Hivi karibuni, wasanii hao wawili walishinda Tuzo za African Movies Viewers Choice (AMVC) zilizofanyika nchini Nigeria ambapo Lulu alishinda katika Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Mapenzi ya Mungu) huku Richie akichukua kwenye Kipengele cha Filamu Bora ya Kiswahili Afrika Mashariki (Kitendawili), tukio lililofanyika Nigeria wiki iliyopita.
 
Waziri nae, kwani lazima amwite ikulu? Angetafuta mahali faragha kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi wapongezane kimya kimya tu. Watu wako busy sasa hivi ndio kwanza March.
 
we we we, mtoe roho! nani yuko tayari?
 
Hapa kazi tu haturuhusu vicheche Ikulu kudadadeki
 
Ebu waache uongo,kwanza ofic ya waziri mkuu haipo ikulu,pili waziri mkuu toka wiki iliyopita yuko ziarani kanda ya ziwa..kapata muda lini wa kuonana na huyo eliza?
 
"Waziri mkuu ofisi yake iko Ikulu?"

Yeah, Ofisi ya Waziri Mkuu ipo Ikulu, upande ule wa barabara inayoenda soko la samaki Ferry, linatazamana na lile jengo la chuo flani cha serikali
 
Waziri nae, kwani lazima amwite ikulu? Angetafuta mahali faragha kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi wapongezane kimya kimya tu. Watu wako busy sasa hivi ndio kwanza March.
Alikuwa hana jipu la kutumbua huyo...
 
Imefichuka! Baada ya kuitwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kupongezwa kutokana na tuzo aliyopata nchini Nigeria, staa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alijikuta akihaha baada ya kuzuiwa kuingia Ikulu kutokana na kutokuwa na kitambulisho cha chama cha waigizaji.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Lulu alijikuta katika wakati mgumu kwani utaratibu wa wasanii kuingia Ikulu umebadilika, tofauti na serikali iliyopita kwani kwa sasa, wasanii wa filamu ni lazima wapitie kwenye Shirikisho la Filamu ‘TAFF’ kisha wizarani ndipo waruhusiwe kuonana na mhusika aliyemuita au anayetaka kumuona.

“Shughuli ilikuwa ifanyike Alhamis, Lulu alipofika wizarani akakutana na utaratibu huo mpya, si unajua yeye siyo mwanachama wa chama chochote cha filamu, ndiyo ikabidi aelezwe jambo hilo,” kilisema chanzo hicho.

Kutokana na utaratibu huo, Lulu akalazimika kurudi katika ofisi za mwenyekiti wa waigizaji mkoa wa Kinondoni (TDFAA), Ally Baucha ambapo alichukua fomu ya uanachama na kuijaza na kuirejesha siku hiyohiyo ya Alhamis iliyopita ili aweze kwenda kuonana na Waziri Mkuu siku iliyofuata (Ijumaa). “Yaani Lulu alihangaika kweli siku hiyo kwani hata siku ya kupokelewa pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hakuna msanii wa TAFF aliyekwenda kumpokea hata mmoja wala viongozi wake, hivyo hata alipopata mwaliko wa Ikulu ikashindikana kuingia bila ya utambulisho wa uanachama wa shirikisho na chama cha waigizaji mkoa anaoishi wa Kinondoni,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Mwenyekiti wa TDFAA, Ally Baucha ambapo alikiri kwamba ni kweli Lulu alikwenda kuchukua fomu harakaharaka na kuijaza na kuwa mwanachama ikiwa ni baada ya kupata mwaliko wa kwenda kupewa pongezi na Waziri Mkuu.

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba ni kweli kwa sasa hakuna msanii anayeruhusiwa kuingia Ikulu bila kupitia kwenye shirikisho na wizarani hata kama ameitwa na nani.
“Utaratibu umebadilika sasa, msanii hata kama ameitwa na kiongozi gani ni lazima afuate utaratibu huo ndivyo tulivyokubaliana, hivyo Lulu alishindwa kwenda moja kwa moja mpaka alipokwenda kujiunga kwanza na chama cha waigizaji na kutambulika na shirikisho ndipo nikawapeleka Ijumaa iliyopita na msanii mwenzake aliyeshinda tuzo pia, Single Mtambalike ‘Richie’ na kwenda kupongezwa kwa kutwaa tuzo hizo za kimataifa.

“Wasanii wanatakiwa kuufahamu utaratibu huo kwani hata wakipita moja kwa moja lazima watarudishwa tu kwenye shirikisho, wakati wao ukifika kama Lulu naamini watajiunga tu hatumlazimishi mtu,”alisema Mwakifwamba.

Hivi karibuni, wasanii hao wawili walishinda Tuzo za African Movies Viewers Choice (AMVC) zilizofanyika nchini Nigeria ambapo Lulu alishinda katika Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Mapenzi ya Mungu) huku Richie akichukua kwenye Kipengele cha Filamu Bora ya Kiswahili Afrika Mashariki (Kitendawili), tukio lililofanyika Nigeria wiki iliyopita.

Craap upuuzi mtupu
 
"Waziri mkuu ofisi yake iko Ikulu?"

Yeah, Ofisi ya Waziri Mkuu ipo Ikulu, upande ule wa barabara inayoenda soko la samaki Ferry, linatazamana na lile jengo la chuo flani cha serikali
Watu hawaijui ofisi ya waziri mkuu iko wapi. Sina hakika na habari hyo, lakini kwa suala la ofisi ya waziri mkuu kuwa ikulu, hilo nakubaliana, labda kama imehamishwa. Otherwise tuweke distinction maana ya neno ikulu. Kama ni ile compound yenye fence nyeupe karibia na soko la ferry na si vinginevyo, basi ni hakika ofisi ya waziri mkuu iko ikulu, mlango wake upo ile barabara ya daladala iendayo ferry, jirani kabisa na soko la samaki. Inatazamana na Chuo cha Utumishi.

Otherwise, wanaopinga watuambie Ofisi ya Waziri mkuu iko wapi ili siku na sisi tukinyakua ka tuzo tukaitwa huko tusije tukapotea njia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom