Lulu aomba kesi yake ihamishiwe Mahakama ya Watoto

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,321
33,126

6398070.jpg

Lulu akiwa anaingia Mahakamani jana
Tuesday, May 08, 2012 12:52 PM
ELIZABETY MICHAEL ‘lulu’ jana aliiomba Mahakama ya Hakiumu Mkazi Kisutu kuhamisha kesi kwenye mahakama ya Watoto kwa kuwa umri wake hauruhusu kesi hiyo kusikiliziwa katika Mahakama hiyo
Hayo aliyasema jana wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa na kuzua minong’ono na mijadala na kuzuka kwa utata kuhusiana na umri wake

Lulu anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba aliyefariki mwezi uliopita
Lulu anatetewa na mawakili wapatao watatu ambao wanaongozwa na Keneth Fungamtama akisaidiana na Wakili Peter Kibatala na Fulgence Masawe.

Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa, mteja wao huyo ana umri wa miaka 17 hivyo, kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika Mahakama ya Watoto.

Mawakili hao walidai wana uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa ambacho kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa huyo.

Wakili Fungamtama alisema Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Kipengele namba 21, kinatamka wazi kuwa mtoto ni Yule aliye chini ya umri wa miaka 18

Hivyo kwa upande wa Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliwaomba wapewe muda zaidi kuhusiana na uchunguzi wa hilo na upepelezi dhidi ya mashitaka hayo yanaendelea hayajakamilika

Na kutilia mashaka cheti hicho kwani cheti kilichowasilishwa Mahakamani kinasomeka kama Diana Elizabeth wakati mshtakiwa ametajwa mahakamani hapo kwa jina la Elizabeth Michael.
“Tunaomba tupewe muda tuweze kuchunguza zaidi kuhusu umri wa mshtakiwa”

Hata hivyo Wakili mtetezi wa Lulu alijibu hilo na kudai kusomeka kwa Diana Elizabeth ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili.

Hakimu Mkazi Augustina Mbando mara baada ya kusikiliza mashauri kutoka kwa pande zote mbili na mazingira ya kesi ilivyo na ilivyogusa jamii, hatuwezi kufanya hoja yoyote hadi upelelezi utakapokamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21, mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa tena.
Awali ilidaiwa kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba.
Lulu aomba kesi yake ihamishiwe Mahakama ya Watoto
 

Utata umri wa Lulu kusikilizwa Mei 28
James Magai
MAOMBI ya uchunguzi wa umri wa muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji, yamepangwa kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mei 28, 2012.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Hata hivyo, umri wake halali umezua utata kiasijambo ambalo limewalazimu Mawakili wanaomtetea kuwasilisha maombi mahakamani wakiitaka mahakama ifanye uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.

Maombi hayo yaliwasilishwa Mahakama Kuu na mmoja wa mawakili wake, Peter Kibatala, Mei 17.

Habari ambazo Mwananchi lilizipata jana kutoka mahakamani hapo na kuthibitishwa na Wakili Kibatala zinasema kuwa maombi hayo yamepangwa kuanza kusikilizwa Mei 28 na kwamba yamengiwa kusikilizwa na Jaji wa Dk Fauz Twaib.

Katika maombi namba 46 ya mwaka 2012, mawakili hao wanaomtetea msanii huyo wanaiomba Mahakama Kuu itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.
Jopo la mawakili hao maarufu linadai kuwa linaamini kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo kwa sasa ndio bado inayoshughulikia kesi hiyo, ina mamlaka ya kufanya au kuamuru ufanyike uchunguzi wa umri mshtakiwa huyo.

Lakini pia wanaiomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi Mahakama Kuu yenyewe ifanye uchunguzi huo.

Mawakili hao walifikia uamuzi wa kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu baada ya maombi ya Mahakama ya Kisutu kujiondoa katika kuyashughulikia.

Akifafanua juu ya maombi hayo Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Raisi wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) alisema kuwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 kifungu cha 113 inaruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa mshtakiwa.

Wakili Kibatala alisema lengo la uchunguzi huo ni ili mahakama iweze kujiridhisha kama mshtakiwa ni mtoto au ni mtu mzima kwa lengo la kujipa angalizo juu ya maslahi ya mtoto.

"Baada ya uchunguzi huo mahakama ikijiridhisha kuwa ni mtoto basi mwenendo wa kesi hiyo utaendeshwa kwa maslahi ya mtoto kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria hiyo ya mtoto," alisema Wakili Kibatala.

Kwa mujibu wa Wakili Kibatala kifungu hich ambacho huelezea ulinzi wa maslahin ya mtoto katika uendeshaji wa kesi kwa watoto wanaokinzana na sheria.
Kabla ya kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu, mawakili hao mawakili hao waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 7,2012 wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa bado ni mtoto.

Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwamba kwa maana hiyo yeye bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.
Kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo wakili Kenedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18 kama inavyotamkwa mahakamani.

Alidai kuwa hata cheti cha kuzaliwa walichokiwasilisha mahakamani kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa hivyo kuwa na umri wa miaka 17.

"Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inatafsiri kuwa mtoto ni yule aliyekuwa na umri chini ya miaka 18 hivyo katika suala la mteja wetu alipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto," alidai Wakili Fungamtama.

Hata hivyo upande wa mashitaka kupitia kwa wakili Elizabeth Kaganda ulipinga maombi hayo na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na hivyo kuomba wapewe muda zaidi.
Wakili Kaganda pia alidai kuwa hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa huyo linasomeka kama Diana Elizabeth wakati mshtakiwa huyo ametajwa mahakamani hapo kama Elizabeth Michael.

Akijibu hoja hiyo, wakili Fungamtama alikiri jina hilo kusomeka Diana Elizabeth na kusema kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa wakristo kuwa na majina mawili

Katika uamuzi wake, Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema kesi hiyo bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote.
Hivyo Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo, aliutaka upande wa utetezi uwasilishe maombi hayo kupitia Mahakama Kuu.

Mbali na Kibatala na Fungamtama ambaye pia anaitetea Kampuni ya kufua umeme wa dharua ya Dowans dhidi ya Tanesco, mawakili wengine katika jopo hilo ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Joaquine De- Melo.

De-Melo ambaye amewahikuwa Rais TLS, pia ni mshindi wa wa tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King. Jopo la mawakili hao wanaomtetea msanii huyo linahitimishwa na Fulgence Massawe kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)

Msanii huyo bado anaendelea kusota rumande kutokana na kesi inayomkabili kutokuwa na dhamana na kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Mei 21 mwaka huu.
Utata umri wa Lulu kusikilizwa Mei 28
 
Jamani, hapa naona ni waste of resources like money and time? kuna haja gani ya kuanza kupeleleza umri wa lulu kwa siku zote hizo? na kama kweli they need fairness basi wampime DNA itawaambia umri au hata mifupa yake mbona biologically by using technology you can detect? Haya labda fedha hizo hakuna lkn je yeye kuwa na umri mdogo au mkubwa kutathibitishaje kosa? mimi nionacho ni kwamba hana kesi ya kujibu bali sasa wanamuweka tu kwa sababu za kiusalama.

Fulgence najua unaweza kabisa kumsaidia hako kabinti katoke huko ila sasa na wewe usiishie kumtetea tu bila kutoa makosa ya wazazi wake ambao wanatakiwa washtakiwe kwa malezi mabovu kwa mtoto ambaye taifa linamgharamia.
 
Mzizi mkavu eti mimi natamani sheria imuweke huru huyu binti lakin iwatie hatian wazazi wake kwa kosa la kutoa malez mabaya kwa mtoto na kumsababishia matatizo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom