Niliangalia taarifa ya habari ya ITV Jana nikamwona Waziri Lukuvi akimtuhumu Makonda kwamba ametapeliwa, Pia ukisoma Post za Nape, yeye hamumunyi maneno. Anamchana Makonda wazi bila ya kupepesa. Nimeshangaa sana kumwona Waziri wa mambo ya ndani akiwa kimya
Anayoyaposti nape yalitakiwa yaongelewe na waziri wa mambo ya ndani, maana suala la kukamata na kuwataja watu hovyo hovyo bila ushahidi ni kosa la kijinai kisheria.
Kituko kingine nilichokiona, ni kijana mmoja naye ni mpenda sifa, ati Amemfungia mmiliki wa kona Bar ati kwa sababu kuna machangu doa wengi wanapenda kwenda kujiuza pale, huyu mwenye bar Ana leseni halali ya kufanya biashara husika, na amekuwa mlipa kodi kwa miaka Yote,
Cha kujiuliza, yeye Ana makosa gani mpaka afungiwe na bwana Hapi? Je Waziri wa viwanda na biashara hapo ofisini anafanya kazi gani ikiwa anaogopa kukemea upuuzi Kama huu?. Kazi ya kudhibiti machangudoa ni ya polisi ambao wanalipwa mishahara kwa kazi Yao. Au waziri Mwijage nae anamwogopa Hapi kwa sababu aliachiwa ofisi na Makonda alipokuwa likizo kwa hiyo naye anaonekana hawezi kuguswa hata akiboronga?
Huu ni mfano tu wa mawaziri waoga, Kwa style hii, hawa mawaziri watamsaidia vipi Raisi Ambaye kwa sasa anaandamwa kila upande kwa sababu ya hali mbaya ya maisha ya Watanzania iliyosababishwa na matamko Kama hayo yasiyo na tija yoyote kwa Taifa? Mwigulu Na Mwijage.
Jitafakarini, mnaogopa nini kuwaambia hawa vijana wafate taratibu?. Mkiendelea kuchelewa kuchukua hatua iko Siku hata Waziri mkuu ataingiliwa naye ataogopa, Heko Lukuvi Heko Nape.