Unafahamu mshahara wa mbunge?
Unafahamu mshahara wa wazir?
Unafahamu motisha za mbunge?
Unafahamu motisha za waziri?
Kama hujui chochote kati ya hayo niliyokuuliza, una haki ya kubwabwaja hapa JF kuhusu nyumba ya thamani ya Billion 1 (TZS).
Napenda kukutaarifu kwamba mimi ni Afisa Utumishi Daraja la Kwanza na muajiriwa wa mojawapo ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mimi ni mmoja wapo ya watumishi wachache wizarani kwetu tunaostahili kusoma waraka wa Serikali kuhusu mishahara au mabailiko ya mishahara pamoja na nyaraka kuhusu stahili zozote za watumishi wa serikali wabunge na mawaziri wakiwemo.
Nakutaarifu kwamba ninafahamu mshahara wa mbunge,mshahara wa waziri, waziri mkuu, jaji mkuu, majaji,spika, naibu spika, katibu mkuu kiongozi na watumishi wote waserikali kuu na halmashauri isipokuwa sifahamu mshahara wa rais na makamu wa raisi na mishahara ya SMZ, pamoja na mishahara ya agencies za serikali.
Aidha ninafahamu stahili motisha za kisheria wanazopata wabunge , mawaziri na watumishi wengine wa Serikali kuu na halmashauri.
Nakutaarifu kwamba sibwabwaji chochote. Nimeongea kitu chenye mantiki na kama ni kweli vyombo husika nilivyovitaja vifanye kazi yake.
Acha kuteteatetea kila kitu sasa kazi ya PCCB na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi ni nini? pamoja na kwamba vipo butu.
Muda mrefu nawaona hawa watu wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma wanadili na wale viongozi wanaoshindwa kujaza fomu kwa wakati na kuwapeleka kwenye baraza la maadili.
Ni muda muafaka sasa kwa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kufuatilia ukweli wa taarifa zinazojazwa kwenye fomu za maadili ya viongozi.
Ukweli ni kwamba viongozi wengi wanajaza taarifa za uongo, wengi wanaficha/ hawataji baadhi mali wanazomiliki kwa sababu nyingi zimepatikana kwa njia ambayo si halali.
Ndugu, acha kutumiwa na kuwa na fikra mgando , kama ni mhusika eleza ukweli wa hiyo taarifa, sio kuleta maswali ya kizushi