Lukuvi amuombe radhi Mbunge wa CHADEMA Iringa-mjini

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Siku ya Ijumaa waliokuwa wakifuatilia Kikao cha Bunge kinachoendelea Dodoma, Mbunge wa CHADEMA Mh. Msigwa wakati wa kuchangia aliishauri serikali kupunguza matumizi ikiwemo kupunguza misafara ya Waziri isiwe mikubwa sana.Alisema alichokiona ilinga kuwa msafara wa Waziri Mkuu unakuwa na Magari zaidi ya 50, Baada ya kusema hilo alishambuliwa vibaya sana haswa na Wabunge wa CCM, yeye Lukuvi akasema msigwa ni muongo sana huku akikejeli kuwa hafai kuwa mchiungaji, na wengine wakisema waongo hawataingia ufalme wa MunguKejeli na dharau za kila aina zilitolewa siku hizo zikimlenga Mtumishi wa Mungu Mh. Msigwa.Nimeshangaa leo Mbunge wa Nkenge Mh. Assumpter akisema nawashangaa wengine wakilalamika kuwa msafara wa Waziri Mkuu unakuwa mkubwa sana, akasema sisi kwetu alikuja na Magari zaidi ya 50 na siku hiyo ilikuwa ni heshima kubwa sana kwa Waziri wetu mkuu tumpendaye, ni haki yake bwana.Itakuwa ni ungwana kama Mh. Lukuvi atamuomba msamaha Mh. Msigwa kwa maneno mabaya aliyomrushia siku ile ,pia wabunge wengine wamuombe msamaha Mh. Msigwa isije ikageuka wao ndo wasiuone ufalme wa Mungu kwa kumnena vibaya mtumishi wa Mungu, aliyoyasema leo Mbunge wa Nkenge yanadhibitisha kuwa Mh. Msigwa alikuwa sahihi.
 
Huyu kwanza LUKUVI ni fisadi wa elimu kile kitabu cha mafisadi wa elimu jina lake limo,jimbo la la ISIMA hakuna hata barabara moja nzuri hata kipande cha rami hakuna,maskini wamejaa wakutupa,huyu muheshimiwa anamatatizo ya akili.
 
tunapaswa kumdharau lukuvi, anadhani kufoka, kukejeli, au kubeza kunamsaidia kuokoa haiba ya pinda iliyopotea mbele ya jamii ya watanzania na Mungu Muumba. Ana roho mbaya sura yake inadhihirisha. hatutamwamini tena hata akituambia baiskeli ina magurudumu mawili.
 
Nilishasema mtoto wa kinyalu wa Mzee Vangimembe ni kihiyo! Mwalimu wa UPE, ana akili ya kuvukia barabara na ya kutambua kuwa hii ni mboga na huu ni ugali tu!!!!!!!!

Mchungaji wangu msamehe huyo kijana anayemiliki majini badala ya akili!!
 
Kama Mbunge wa CCM anathibitisha kuwa ni kweli Waziri mkuu anatembea na msafara wa magari 50, Lukuvi anauliza nini?

Nchi imekuwa inaongozwa kwa mazoea, na hata wabunge wengi wamefanya Dodoma sehemu ya posho, sasa chadema wanaonesha kwa vitendo ni kitu gani wanatikiwa kufanya, wao wanahamaki! Si mliomba kura wenyewe, jibuni mapigo. Na hao vimbelembele wanaonekana kutetea hoja zisizo na maslahi kwa taifa wajue 2015 tutapiga rewind ya nguvu. haponi mtu.
 
Kama anatetea watu wanaotokwa na mapovu sijui yeye anayetokwa na ute ute atakuja tetewa na nani? sasa anatafuta umaarufu wa sifa za kijinga!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom