Lukuvi amtia korokoroni mkurugenzi Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Lukuvi3%286%29.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, amemcharukia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hilo, Bakari Kingobi na kumtaka asitoke nje ya mkoa huo kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi hapo atakapohakikisha ujenzi wa vizimba katika jengo la machinga Complex unakamilika na wafanyabiashara ndogodongo wanaanza kulitumia.
Hata hivyo, Lukuvi alisema wakati Mkurugenzi huyo amezuiwa kwenda sehemu yoyote nchini na nje ya nchi, watendaji wa Jiji hilo wahakikishe wanashirikiana ndani ya siku hizo wawe wamekamilisha miundombinu yote ambayo bado haijakamilika ili wafanyabiashara hao waanze kufanya shughuli zao.
Lukuvi aliamua kutoa maelezo hayo baada ya kuonekana kukasirishwa na maelezo ya Mhandisi wa Jiji, Musa Natty, ambaye alimueleza kuwa ujenzi wa vizimba ndani ya jengo hilo haujakamilika ambapo hadi wakati huo kulikuwa na vizimba 377 kati 4500 vinavyohitajika.
Wakati akitoa maelezo hayo, mhandisi huyo alieleza kuanza kwa shughuli za biashara katika jengo hilo kunategemea na kukamilika kwa vizimba hivyo pamoja na kufikiana makubaliano kati yao na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Dawasco.
Baada ya kupata maelezo hayo, Lukuvi alionekana kuwa mbogo na kuamza kumuhoji Mhandisi huyo.
“Unajua sikuelewi, hivi kitu gani kinachochelewesha kukamilika kwa vizimba hivi hadi leo, unaniambia kuna vizimba 377 tu?” alihoji Lukuvi.
Mhandisi: “Mkuu, kutokana na kazi yenyewe kuwa kubwa, lakini nakuahidi hadi Juni 20 tutakuwa tumekamilisha kujenga vizimba vyote.
Lukuvi: “Sasa hata kama ukikamilisha ujenzi huo, wafanyabiashara hawa wataanza kazi ikiwa kuna miundombinu mingine haijakamilika?
Mhandisi: Kimya.
Baada ya majibizano hayo, Lukuvi alimgeukia Kingobi na kumueleza hatokubali kupitisha kibali cha kusafiri kwenda nje ya nchi au mahali popote nchini kwa kipindi hicho hadi hapo kazi zote zitakapokamilika na wafanyabiashara hao kuanza kuuza bidhaa zao ndani ya jengo hilo.
Alisema amechukua hatua hiyo kutokana na kuchoshwa na siasa alizozieleza kuwa zinaweza kusababisha hali ya kutoaminiana kati ya Serikali na wananchi wake.
Pamoja na hayo, aliutaka uongozi wa wafanyabiashara hao kuhakikisha hadi ikifika Juni 20 mwaka huu wawe wameshafanya mgawanyo wa sehemu za kufanyia biashara ikiwa pamoja na kupangilia aina ya biashara kulingana na ghorofa zilizokuwemo.
Ziara ya Lukuvi imekuja baada ya kazi ya kuwahamishia wafanyabiashara hao kwenye jengo hilo kukwama kila mara na kuzusha manung'uniko kutoka kwa wafanyabiashara hao.



CHANZO: NIPASHE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom