Lukuvi ajikongoja kusaidia Polisi Iringa pikipiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi ajikongoja kusaidia Polisi Iringa pikipiki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Oct 22, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]


  JESHI la Polisi mkoani Iringa limepata msaada wa pikipiki nne kwa ajili ya vituo vyake vidogo vinne vinavyokabiliwa na tatizo la usafiri katika jimbo la Ismani, wilayani Iringa. Vituo vitakavyonufaika na msaada huo uliotolewa na Mbunge wa Ismani, William Lukuvi (CCM) ni pamoja na Migori, Ismani, Idodi na Pawaga. Kabla ya kupatiwa msaada huo, askari wa vituo hivyo walikuwa wakilazimika kutumia usafiri wa baiskeli na wakati mwingine kutembea kwa miguu umbali mrefu kuwasaka wahalifu.

  Akiukabidhi msaada huo kwa niaba ya Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu wa Bunge, msaidizi wa Mbunge huyo Thom Malenga alisema una thamani ya Sh milioni 5. Malenga alisema Lukuvi ametoa msaada huo ili kuimarisha ulinzi kwa wananchi wa jimbo hilo kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi. Alisema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Mbunge alizopata kutoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana baada ya wananchi wa jimbo hilo kumwomba msaada huo wa pikipiki kwa ajili ya kuongeza nguvu ya ulinzi. “Wakati wa kampeni wananchi wa Jimbo la Ismani walipata kumwomba Mbunge wao Lukuvi msaada wa pikipiki hizo kutokana na askari waliopo katika vituo vinne vya jimbo hilo kuchelewa kufika katika maeneo yenye matukio ya uhalifu,” alisema.
   
Loading...