Lukuvi agonga kikombe kiujanja na kutoa msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi agonga kikombe kiujanja na kutoa msaada

Discussion in 'Celebrities Forum' started by semmy samson, Mar 21, 2011.

 1. semmy samson

  semmy samson Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LUKUVI4.jpg

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), William Lukuvi, akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawalali na Rose Nyerere (katikati) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndega wa Wasso, Liliondo, jana asubuhi. Rose alitua na ndege nyingine akiwa na mdogo wake anayeumwa, Mazembe Nyerere.Waziri Lukuvi na msafara wale walielekea kijijini Samunge kwa Mchungaji Ambilikile Masapile

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), William Lukuvi, amekiri kuwa mkusanyiko mkubwa wa watu wanaokwenda kunywa dawa kijijini Samunge, Loliondo mkoani Arusha ni tukio la kihistoria ambalo halijawahi kutokea kabla na baada ya Uhuru wa Tanzania.

  Waziri Lukuvi alitoa kauli hiyo jana kijijini hapa, alipokwenda kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyotoa kwa niaba ya Serikali siku kadhaa zilizopita kuhusu uboreshaji wa mazingira ya utoaji huduma.

  "Jamani kama kuna mtu ambaye anapuuza hiki kinachoendelea hapa Loliondo kwa kweli ni vigumu kumuelewa, haiwezekani watu wote hawa waje huku wakati hakuna kitu.

  "Kwa kumbukumbu zangu sahihi, sikumbuki ni lini katika nchi yetu kuliwahi kutokea mkusanyiko mkubwa kama huu wa watu wa rika zote, wenye vipato, elimu na utaifa tofauti kama hili la kwa Mchungali Ambilikile, huu ni muujiza.

  "Kama nilivyokwisha sema hapo awali, sisi kama Serikali kamwe hatutaingilia huduma ya huyu mzee, lakini kwa sababu watu ni wengi sana hapa hatuwezi kukaa pembeni, ni lazima tuje tusaidie kuboresha mazingira ili wananchi wengi iwezekanavyo wapate hii huduma," alisema.

  Waziri huyo alitumia fursa hiyo kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kuimairisha ulinzi na kulinda amani, hasa kwa kuzingatia umati mkubwa wa watu na mazingira duni kiutendaji yaliyopo kijijini Samunge.

  Mbali na pongezi kubwa kwa Jeshi hilo, alimsifu Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawalali pamoja na wasaidizi wake kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.

  Katika ziara hiyo jana, Waziri Lukuvi alikutana na kupeana mkono na Mchungaji Mstaafu Ambilikile Masapile, na kisha alipewa dawa akanywa pamoja na mkewe na wageni wengine.

  Lukuvi, alimwomba Mchungaji Masapile, aeleze mambo ambayo angependa Serikali iyafanye.

  Akijibu swali hilo, Mchungaji Masapile ambaye huzungumza taratibu, aliiomba Serikali imsaidie kumpatia sufuria kubwa tatu na maturubai ya kutosha.

  Alisema sufuria hizo ni kwa ajili ya kuchemshia dawa na maturubai ni kwa ajili ya kuwasaidia maelfu ya watu wanaofika kupata dawa, hasa wakati huu wa mvua kubwa. Pia aliomba apatiwe tanki kubwa la kuhifadhia maji. Samunge kuna mfumo wa maji safi na salama ya bomba. Sufuria anazoomba zina uwezo wa kuhifadhi lita zaidi ya 400 kwa kila sufuria moja.

  Kwa sasa Halmashauri ya Ngorongoro, imetoa gari linalotumika kusomba kuni, na pia kuna gari la kuhudumia wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura kutoka kwenye msururu mrefu mno wa magari.

  Bila kuchelewesha mambo, Lukuvi alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Loliondo, Sh milioni moja kwa ajili ya kununulia sufuria na tanki la kuhifadhia maji.

  Aidha, alisema wiki ijayo Serikali itapeleka maturubai na viti ili viweze kusaidia maelfu kwa maelfu ya watu wanaomiminika nyumbani kwa Mchungaji Masapile kunywa dawa.

  "Kwa kweli huyu mzee ni mtu wa Mungu, jamani hana makuu kabisa, nimeuliza gharama za masufuria na matanki ya maji nimeambiwa hazizidi Sh milioni moja, kwa hiyo nimekabidhi fedha hizo.

  "Naondoka kwenda Dar es Salaam kukutana na wenzangu kwa ajili ya kushughulikia suala la mahema na viti kwa ajili ya watu kupumzika, kwa sababu wengine ni wagonjwa sana hivyo hawawezi kusimama kwa muda mrefu wakisubiri dawa.

  "Mchungaji ameniambia uwezo wake ni kuhudumia watu 2,000 kwa siku, sasa itabidi kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa na wilaya tuweke utaratibu ambao kwa siku wataruhusiwa watu 2,000 kufika kwake na kunywa dawa.

  "Haileti maana mtu kushinda porini kwa siku nne hadi tano, kwa sababu kwa kufanya hivyo shughuli nyingine za maendeleo zinasimama. Kwa mfano gari nyingi zinazotumika hapa ni zile zinazobeba watalii, ni lazima tutafute utaratibu mzuri," alisema.

  Pia aliwaonya wenye magari mabovu, ambao kutokana na tamaa ya pesa wamekuwa wakibeba abiria kuwapeleka kwa Mchungaji Masapile, kuacha kuyatumia.

  Alisema magari hayo yamekuwa yakiharibika au kupinduka na kusababisha adha kubwa kwa wananchi.

  Alisema ataagiza magari yote yanayokwenda kijijini Samunge, yakaguliwe na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kabla ya kuanza safari ili kuhakiki ubora, na gari likishakaguliwa litapewa namba maalumu.

  Jana watu wa kawaida na watu maarufu waliendelea kumiminika Samunge.

  Miongoni mwao waliokunywa dawa jana ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Paul Rupia na mkewe; pamoja na Rosemary Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Rosemary alimpeleka mdogo wake, Mazembe Joseph Nyerere, ambaye anasumbuliwa na maradhi ya figo.

  Pia walikuwapo Watanzania wengi wenye asili ya Kiasia ambao wote, pamoja na watoto wao, walikunywa dawa.

  Hali ilikuwa ya shangwe kwa watu wote hao waliobahatika kuonana na Mchungaji Masapile. Wengi walimshika mkono na kutaka kupiga picha naye.

  Leo, makamanda wa polisi wa mikoa karibu yote nchini wanatarajiwa kuwapo Samunge kwa ajili ya kujionea hali halisi na kumalizia safari yao kwa kupata dawa.

  Msururu wa magari ni mrefu, na kwa taarifa za jana ulikuwa umefikia urefu wa kilomita 20.

  Habari hii imeandikwa na Manyerere Jackton, Masyaga Matinyi na Eliya Mbonea, ambao kwa zaidi ya wiki moja sasa wapo Samunge wakiripoti tukio hili kubwa na la aina yake kuwahi kutokea nchini.
   
 2. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  asanteeee maajabu yanaendelea
   
 3. comred

  comred JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 1,393
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  lukuvi kashapata nw lets wait n c anaweza akawa makamba next..!
   
 4. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Duh! Chain ya Urefu wa km 20, foleni ya magari kama kutoka Gongo la mboto mpaka Ubungo mzee ametisha
   
 5. Muro

  Muro Senior Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mibaraka iendelee kummiminikia mtumishi wa mungu Mchungaji mwasapile
   
 6. semmy samson

  semmy samson Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo lazima aende maana akili yake imeanza kuchoka....ndo maana hata maneno yake yanakuwa kama ya mtu asiye na utimamu wa akili
  akienda kwa babu huyoo hataongea tena upuuuuzi...
   
 7. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kabakia shehe yahaya na Kakobe
   
 8. shemasi

  shemasi Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna uhusiano wa kichwa cha habari na habari yenyewe mkuu.mbona sijaona huo ujanja wa lukuvi kwenye kunywa dawa?
  hizi threads za kishabiki mpaka lini?
   
 9. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi serikali haioni umuhimu wa kutengeneza barabara? Itasaidia magari yasife kwa wingi na kurahisisha utoaji wa dawa kwa muda mfupi watu wasikae porini mno. Lukuvi shughulikia hilo si lazima yale tu aliokueleza "Babu". Ila umefanya vyema kuitikia mara moja suala la upatikanaji wa sufuria.
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mkuu huoni nini yeye kama ameenda kiserikali kuangalia mambo na hapo hapo kaamua kugonga kikombe ni janja yake kwanini aende huko binafsi angeweza tuma watu wake wa chini?
   
 11. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ujanja ni kuwa alienda huko akijifanya ameenda kukagua hali ya usalama na shida za Mchungaji kwa serikali, kumbe alikuwa anataka aonane na Babu mwisho wa yote apate KIkombe kama ambavyo alivyopata.!!!!
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Hadi muurudishe urais mlio mpoka Slaa.
   
 13. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na hii janja ya nyani...; issue kubwa hapa ilikuwa kugonga kikombe, hayo mengine ni longolongo tu
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280

  Sasa unadhani angewezaje kumshawishi wife kwenda kugonga kikombe?
   
 15. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kumbe almost 75% ya wanzania wa kawaida ni WAGONJWA! Viongozi ni karibu 95% ni wabovu! Lukuvi nilikuwa namuona kama ana afya njema kumbe ni matatizo kama Mrema!

  Heri Mrema alikuwa muwazi kuwa anaenda kupata dose, wengine wanaenda kwa gear tofauti tofauti. Mkuu wa kaya yeye alivunga anaenda kuzindua nyayo za binadamu wa kale kumbe akakunja kona kwa Babu kupata kikombe!
   
Loading...