Lukuvi abaini wanaouza maji machafu ya chupa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. William Lukuvi, amebaini watu wanaojaza maji ya yasiyo safi na salama katika chupa za maji na kuyasambaza mtaani kwa ajili ya kuyauza baada ya kufanya ziara katika soko la Ilala Boma.

Bw. Lukuvi alibaini maji hayo baada ya kuwakuta watu hao wakiyajaza kwenye chupa za maji hayo na kuyatembeza barabarani.

Watu hao wamekuwa wakiyajaza maji hayo kwa muda mrefu bila watumiaji bila kugundua na wamekuwa wakinunua na kunywa wakidhani ni maji safi na salama kitu ambacho hatari kutokana na kusababisha magonjwa ya kuambukiza.

Bw. Lukuvi aliwataka watu hao kuacha tabia hiyo mara moja kwani nembo wanazotumia ni za kampuni ambazo zinalipa kodi kubwa na hivyo kuzihujumu kimapato.

"Watu hawa wanaofanya hivi wanawaharibia wale wanaotambulika kisheria na kwa kutengeneza maji hayo kwani wananchi watakosa imani na watu hao kwa kuwa kuna kundi dogo ambalo linataka kuharibu biashara ya wengi," alisema Bw. Lukuvi.

Hata hivyo alipotafutwa Bwana Afya wa soko hilo kuelezea tabia ni kwa nini watu haoa wamaeakuwa wakifanya shughuli hiyo wakati akijua inahatarisha afya za watumiaji hakuweza kupatikana kwa wakati huo.

Pia Bw. Lukuvi hakuridhishwa na mapato yanayotokana na soko hilo kwani kiwango alichoelezwa ni tofauti na idadi kubwa ya wafanyabiashara walipo sokoni ukilinganishwa na soko la Buguruni linalokusanya sh. milioni 5 kwa mwezi ambalo ni dogo kwa ukubwa dhidi ya soko hilo.

Aliagiza Uongozi wa Manispaa ya Ilala kuweka mtu mmoja atakayekusanya ushuru wa soko hilo ili fedha ziweze kupatikana zote bila kupotea potea.

Bw. Lukuvi alisema serikali itaboresha miundo mbinu iliyochakaa katika soko hilo ikiwa ni, pamoja na kuweka sakafu na kuongeza matundu ya choo ili yaweze kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara wa soko hilo .
 
Back
Top Bottom