Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina amesema wananchi wa Meatu hawakuchagua tu Mbunge wa Jimbo, bali wametoa Mbunge wa Taifa anayetetea kila aina ya mtanzania, wakiwemo wanyonge wasio na sauti, na kukemea mafisadi na wala rushwa
Akizungumza na wananchi wa Mwandoya, Wilayani Meatu, Mpina amesema kauli hiyo ya heshima ilitolewa na Rais Samia mwenyewe, ambaye baada ya kufanya ziara nchi nzima, alihitimisha mkoani Simiyu, na kusema wazi kuwa Mbunge wa Meatu ni Mbunge wa Kitaifa – jambo ambalo halijawahi kusemwa kuhusu Mbunge mwingine.
“Rais alipokuja, alizungumza na wana Kisesa na Meatu na kusema wazi kuwa mmechagua Mbunge wa Taifa. Sasa hili si kombe la Mpina peke yake, ni kombe la wana Kisesa wote,” alisema.
Ameongeza kuwa mafanikio hayo ni uthibitisho wa kazi kubwa inayofanyika jimboni na kitaifa. “Tumewatetemesha mafisadi, wala rushwa – nchi nzima imetikisika,” amesema Mpina na kuwataka wananchi kuhakikisha hawamuangushi kwa kutunza heshima hiyo.