ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
Leo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, Ndugu Luhaga Mpina, pamoja na Mgombea Mwenza wake, Ndugu Fatma Fereji, watazungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Jengo la Maalim Seif, Dar es Salaam, kuanzia saa 4:00 Asubuhi.
#LindaKura
#MuhuniHasusiwi
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mpina, mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa ACT Wazalendo, Fatma Fereji, amesema:
“Nimefuatilia maisha ya siasa ya Mpina na nimeona kuwa kiongozi huyo ni chuma kisichoyumba. Yaliyomkuta Mpina si ajali ya kisiasa, Mwenyezi Mungu ana maono yake na leo yametuwezesha kuungana nasi.”
“Haishangazi Mkutano Mkuu wa Agosti 6 kumpitisha kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa asilimia 92.3 za kura. Sasa safari ya kutafuta mabadiliko imeanza na inaongozwa na jemedari Mpina.”
Mpina: Michango yangu bungeni ilitaka kupasua paa
“Michango yangu bungeni mnaijua na ninyi wahariri mmeshuhudia hoja nzito bungeni mithili ya paa kutoboka. Mwaka 2014, nikiwa pamoja na kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, na marehemu Mbunge Deo Filikunjombe, tulikesha wakiilinda ripoti ya uchunguzi kuhusu kashfa ya Tegeta Escrow ili isije ikaibiwa kabla ya kuwasilishwa bungeni. Manyang’au yalikuwa yanasubiri hapo nje, yangeiba yangebailisha ripoti ile. Sasa utaona mtu anagombea urais lakini hajawahi kupimwa kama hivi.”
Akizungumzia mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM
‘’Kuenguliwa kwa waliokuwa wabunge 28 kulitokana na nia ya kuondoa wabunge waliokuwa wakiuliza maswali na kutoa hoja bungeni. Wabunge hawa 28, ukiichukua orodha yao, ile cream yote iliyokuwa ikiuliza maswali bungeni wameondolewa, ili ufisadi upate nafasi, ili wake za mawaziri wapite, ili kufanikisha magenge yao yaendelee.”
Amewataja baadhi ya wabunge akiwamo yeye mwenyewe aliyekuwa Mbunge wa Kisesa (Simiyu), Godfrey Kunambi (Mlimba), Flatey Massay (Mbulu), Joseph Oleshangay (Ngorongoro), Josephat Gwajima (Kawe), Mrisho Gambo (Arusha), Christopher Olesendeka (Simanjiro). “Wabunge hawa 28, ukiichukua orodha yao, ile cream yote iliyokuwa ikiuliza maswali bungeni wameondolewa, ili ufisadi upate nafasi, ili wake za mawaziri wapiti, ili kufanikisha magenge yao yaendelee.”
Kuhusu taarifa za jina lake kukatwa, Mpina amefafanua:
“Taarifa za jina langu kukatwa zilianza kutangazwa miaka miwili iliyopita na baadhi ya viongozi wa CCM na baadaye baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge ilitangazwa na vyombo vya habari mapema baada ya vikao vya kamati za siasa ya wilaya na mkoa kumalizika, jambo ambalo ni kinyume na katiba na maadili ya CCM.”
Akizungumzia matukio ya watu kutekwa na kuuawa
“Haiwezekani watu waendelee kutekwa na kuuawa. Haiwezekani uhai na thamani ya maisha ya mwananchi yakachezewa. Hatuwezi kukubali hoja dhaifu kwamba kufa ni kufa tu. Haiwezekani vifo hivi vinatokea, halafu waziri, IGP, DCI, OCD na makamishina bado wako ofisini.
Huu mfumo mzima lazima ufumuliwe, lazima wasiojulikana wajulikane na waliopotea tuwapate.”
Kuhusu uhuru wa kuabudu:
“Haitatokea tena katika historia wananchi kunyimwa haki ya kuabudu, kufungiwa makanisa na misikiti, viongozi wa dini kuvamiwa na kujeruhiwa hadi kwenye makazi yao.”
Akitolea mfano, aliongeza: “Makanisa ya Glory of the Christ (Ufufuo na Uzima) yaliyoongozwa na Askofu Josephat Gwajima yalifungwa nchi nzima Juni 2025, na Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dk Charles Kitima alivamiwa na kujeruhiwa Mei 2025.”
Kuhusu utekelezaji wa miradi jimboni kwake, Mpina amebainisha:
“Nimesimamia na kuhakikisha ujenzi wa nyumba, madarasa, maabara, vifaa vya TEHAMA, madawati kwa bajeti ya serikali na kuingilia mbunge unapoona shule haina vifaa. Nimesimamia ujenzi wa zahanati 15 nikiwa nimekuta zahanati 12 na kituo cha afya kikiwa kimoja, sasa vipo viwili vinavyofanya hadi upasuaji.”
“Wakati nakua mbunge kulikuwa na mradi mmoja tu wa maji, nimesimamia na kuhakikisha ujenzi wa miradi mipya 8 ya maji na tumeweka pampu 1,150 za maji. Awali kulikuwa na barabara mbili tu na hakuna daraja hata moja, sasa kata zote na vijiji vyote vya Kisesa vimeunganishwa na barabara zenye jumla ya kilomita 861, madaraja 37, makaravati 909.”
“Nimekuwa nikisisitiza matumizi mazuri ya fedha zitokanazo na kilimo na biashara kwa maendeleo ya familia badala ya anasa. Leo nina furaha kuwa katika Jimbo la Kisesa wananchi wamejenga nyumba nzuri, jimbo linameremeta.”
Akizungumzia mchango wake kitaifa,
“Yapo mambo mengi niliyoshiriki na kusimamia kikamilifu na matokeo chanya kupatikana. Najivunia sana katika uwakilishi wangu bungeni kupitia maswali, kupitisha bajeti, utungaji wa sheria, upitiaji mikataba na maridhiano ya bunge. Mwaka 2021–2023 nilionyesha jinsi mapato ya serikali yanavyopotea na matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za umma yenye jumla ya zaidi ya trilioni 30.
Pia nilionyesha nchi inapoteza kila mwaka zaidi ya trilioni 42. Nilishiriki katika Tume ya Spika Anna Makinda kuchunguza kashfa ya Tegeta Escrow ya mwaka 2014. Sasa hivi tuna mikataba 43 iliyoingiwa na serikali bila kuambiwa bunge, na kama halijaambiwa bunge, wananchi hawajaambiwa.”
“Michango yangu imekuwa fikirishi ndani na nje ya bunge na imezisaidia mamlaka za ulinzi na udhibiti kuchukua hatua. Michango yangu ya mwaka 2021–2025 na wabunge wengine ilimfanya Rais Samia kufanya maboresho ya kodi. Nilipeleka mapendekezo yenye kurasa 235 kwa Tume ya Maboresho ya Kodi, na hawakukosoa ukurasa hata mmoja.
Mimi niliupinga mkataba wa APC+F siku ya kwanza wenye thamani ya trilioni 3, na hata Rais Samia baadaye aliufuta baada ya kuona hauna tija. Nimezaliwa kwenye familia ya CCM lakini chama kimepoteza mwelekeo na kukiuka misingi ya waasisi wake. CCM imekuwa na misingi ya kujisahihisha, lakini hii ya sasa imechoka, haina wazee wa kuisahihisha. Hii ya sasa ni kama vyuma chakavu.”
“Upendeleo umehalalishwa, mali za umma zimepotea bila kuwajibishwa, na mchakato wa uchujaji wa mwaka 2025 umevunja katiba kwa upendeleo. Tumeshuhudia kikao cha kuwaengua watia nia kikikaa usiku kucha kuwaondoa kina Mpina, lakini kikao cha kujadili ripoti ya CAG kuhusu upotevu wa fedha hakijawahi kufanyika hata siku moja.”
"Sisi Tanzania siyo masikini, sisi siyo masikini. Umaskini siyo fahari, na kwa namna hiyo nipo sehemu sahihi ya kutokomeza hili. Nagombea nafasi hii ikiwa ni ishara ya kuusuka uchumi wa nchi hii. Nagombea nafasi hii kama ishara ya kuleta katiba mpya ambayo imekuwa kilio kwa Wananchi.
Nagombea nafasi hii kama ishara ya kuondoa watu kushindwa kupata uhuru wa kuabudu hasa kwa makanisa yaliyofungiwa kama ya ufufuo na uzima''
Mpina ameongeza kuwa hawezi wala hategemei kuhama chama hicho hivi karibuni. Akijibu swali kama atarudi CCM amesema "ACT-Wazalendo inaenda kushika Dola na yeye kuwa rais, hivyo hawezi kuhama chama tawala kwenda chama kingine".
"Sheria za uchaguzi zinataka chama kiishie shilingi bilioni 25. Sijui kwa nini licha ya kuwa chama tawala wameamua kufanya harambee ya kuchangisha bilioni 100 huku wakijua kuna conflict of interest. Kuna walipa kodi wanaweza kuja kutafuta huruma za kutolipa kodi. Kuna mtu pale ametoa hela wakati anadaiwa bilioni 400 kwa miaka 5. Hakuna wa kumdai.
Sijui kwa nini wamechanginyikiwa waliposikia Mpina wa ACT amechukua fomu hadi wakaanza kufanya harambee na kuingilia mpaka ratiba ya tume na kuingiza jambo ambalo linacontradict mpaka sheria za nchi.
Nakumbuka Leginald Mengi, alikuwa rafiki yangu sana. Alifanya mabadiliko makubwa sana katika vyombo vya Habari na kuhakikisha vyombo vya Habari vinafanya kazi yake kwa uhuru zaidi.Nikiwa rais natamani sana iwe kama kipindi kile Cha Mengi kwa vyombo vya Habari kuwa na uhuru katika kufanya kazi”