Lugola akalia kuti kavu ndani ya CCM

Lugola akalia kuti kavu ndani ya CCM

Wacha watoane macho

Sent using Jamii Forums mobile app
Instagram media - Bt2Krycj3b7.jpg


Hii laana haitomwacha
 
Nyani anataka kumuhoji Gendere kwa kosa la kula mahindi ya wakulima wakati wote ni walewale, tofauti yake mmoja mkubwa kwa umbo na mwingine mdogo kwa umbo.
 
Swala la Lugola bado alijaeleweka au alijawekwa sawa wana CCM kuanza kumuhukumu moja kwa moja.Wangesubili Takukuru ifanye uchunguzi itoe ripoti kilichofanyika source yake ilikuwa namna gani.Viongozi wa CCM Mara wangetoa mifano mizuri ya Mwalimu Nyerere aliyokuwa ikiitoa katika hotuba zake kama ya kutokiuka katiba,viongozi wa Serikali kutochota fedha nje ya budget zao na fedha hizo ziwe zimeidhinishwa na bunge
 
Mmawia,
Chadema mkoa wa Mara watapinga!
Ama kweli ccm mazimwi matupu! Suala la lugola linaihusuje ccm mkoa? Huu ni msimu wa kilimo mwambie mwenyekiti wenu aende shambani aache kutegea kwa kujificha nyuma ya lugola! Mara takukuru na Sasa ccm. Kwani mlikuwa wapi kabla ninyi watu? Au mpaka boss wenu anene ndio mfanyekazi?
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara kimesema kinaandaa utaratibu wa kumuita katika vikao na kumhoji aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ili awaeleze sababu zilizopelekea kuaibisha mkoa huo na Rais John Magufuli ambaye alimuamini na kumpatia nafasi ya uwaziri ili atumikie Taifa.

Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, Samuel Kiboye wakati akieleza namna ambavyo chama hicho kinakasirishwa na viongozi wanaopewa nafasi ya kumsaidia Rais katika wizara mbalimbali lakini mwisho wa siku wanaliingiza Taifa katika mikataba mibovu.

Ama kweli usitukane mamba kabla hujavuka mto.

View attachment 1339630

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila shaka atawajibu kwa kutumia vifungu vya ilani ya uchaguzi. Hajui tofauti kati ya ilani na katiba/sheria za nchi na alikuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Ama kweli ccm mazimwi matupu! Suala la lugola linaihusuje ccm mkoa? Huu ni msimu wa kilimo mwambie mwenyekiti wenu aende shambani aache kutegea kwa kujificha nyuma ya lugola! Mara takukuru na Sasa ccm. Kwani mlikuwa wapi kabla ninyi watu? Au mpaka boss wenu anene ndio mfanyekazi?
Nimesema hapa Chadema mtapinga!
 
Badala ccm mrudi kwenye katiba yawarioba eti mnataka kumuboji ,watanzania tunakazi kubwa watu hatujielewi inafika makosa yakikatiba yanatengenezwa kua yamtu binafsi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom