Lugha yetu ni " Kiswahili " au " Swahili "?

bbwaoy

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
466
464
Heri,

Katika mapambano yangu yaku pata elimu somo la Kiswahili lilikua changamoto kwangu. Hivyo najifunza kila siku.

Nini tofauti yake? " Kiswahili " na "Swahili".

Wageni kutoka nje wata kuuliza swali: Do you speak Swahili?

Wazawa wata kuuliza: Una zungumza/kuongea Kiswahili?


Nini hasa tofauti yake?

Asanteni!
 
Ni Kiswahili una pose ma Swahili ni kama kusema ki-English

Kwaio "Swahili" ni kwa lugha ya kiingereza? Hahaha ... bado na hitaji kujifunza!

Kwa kifupi ni kwamba "Kiswahili " hutamkwa na kuandikwa "Swahili" kwa laugha ya Kiingereza?

Ngoja tupate majibu kwa wajao.
 
Lugha ni Kiswahili na kabila au tribe ni Swahili , unaulizwa " are you speaking Kiswahili and not Swahili , Swahili is a trible formed by small bantu tribles found in eastern and central part of Africa.
 
Lugha ni Kiswahili na kabila au tribe ni Swahili , unaulizwa " are you speaking Kiswahili and not Swahili , Swahili is a trible formed by small bantu tribles found in eastern and central part of Africa.

Huu ndo huwa unaitwa upotoshaji.. ni wapi hilo kabila la swahili lipo?? Uswahili ni utamaduni na wala sio kabila. Na neno 'tribe' haliandikwi 'trible'
 
Ki- Swahili
-Swahili

Ki- ni mofimu ambayo inaongeza taarifa zaidi

Na -Swahili ni shina la neno

-shina la neno ndilo hutoa taarifa za msingi

Mfano. -kula. Ni shina linalotoa taarifa msingi

Lakini tunaweza kuongeza mofimu(affix) mbalimbali ili kupata taarifa zaidi

Mfano ana-kula
Wali-kula

Kadhalika kwenye kiswahili

Shina -Swahili
Ki-swahili
Wa-swahili
M-swahili

Hivyo kutumia -swahili ni kumaanisha lugha moja kwa moja
 
Lugha ni kitu kigumu sn kama huto tuliza akili na kujifunza.

Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katka mazingira ya vituo vya biasharavya pwani ambako wafanyabiashara kutoka Uarabuni, Uajemi na Uhindi walikutana na wenyeji Waafrika. Lugha kuu ya kimataifa ya biashara hiyo ilikuwa Kiarabu.

wasemaji wa lugha za Kibantu, waliyapokea maneno mengi hasa ya Kiarabu katika mawasilia yao.

Kwa hiyo msingi wa Kiswahili ni (sarufi) na (msamiati) wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu.

pia kuna athira ya lugha mbalimbali kama kiajem,kihindi na kireno.

Kwa karne nyingi iliandikwa kwa herufi za Kiarabu (سواحلي sawaHili au لغة سواحيلية lugha sawaHiliya).

Kwahiyo (swahili)neno la kiarabu
 
Tuendelee kupata maoni kadha ... shukrani kwa wachangiaji mlio kwisha changia.
 
Back
Top Bottom